Profesa Maji marefu "Picha yangu imetengenezwa" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Maji marefu "Picha yangu imetengenezwa"

Discussion in 'Jamii Photos' started by TIQO, Mar 22, 2012.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  "Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa jana ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.Vilevile ukurasa wa kwanza gazeti la Tanzania Daima.
  Source: Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nilkuwepo wakati picha ikipigwa hakuna cha kuunganisha picha wala nini maji marefu anajiabisha tu
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mchawi siku zote ni mchawi tu
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mchawi siku zote ni manipulator
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli basi gazeti la Mwananchi naliweka kwenye kundi la udaku kama Uwazi, Kiu, Ijumaa.
   
 6. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Potea kule...mshirikina mkubwa!
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Labda alikuwa anawanga kampeni za CHADEMA
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mambo ya Kinjeketile mwachie Kinjeketile. Joshua Nassari anakwambia walianza na mungu na watamalizia na mungu. Kama Prof Maji Marefu alidhani 'science' yake ingeziba lens za camera ili picha yake isionekane basi kapotea njia. Na asipojifunza ataabika kama kile kibibi kilichotunguliwa jangwani na wana-maombi.
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ulienda kufanya nini kwenye kambi ya CDM in the first place?
  Tunakufahamu wewe ni MGANGA WA KIENYEJI, Je ulikuwa umepeleja NDUMBA?

  Tulianza na MUNGU tutamaliza na MUNGU. Nguvu zako za giza haziwezi
  kushinda nguvu za MUNGU.
   
 10. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa nini hawakumchoma moto mchawi mkubwa huyo...alienda kufanya nini kule...
   
 11. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Awaroge basi waliompiga picha! Au hata ndumba hazijui nini anatuzuga tu kuwa ni mganga a.k.a mchawi?
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  wewe mwenyewe mdaku
   
 13. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Editors nowadays are increasingly turning to sensationalism in an attempt to woo purchasers so as to keep their business afloat. Even so, nobody has ever expected a reputable newspaper like Mwananchi to engage in such nasty tactics.
   
 14. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hajui Kusoma lakini nashukuru picha ameiona!
   
 15. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Professor wa anga!!!!! Unaruka juu bila kutumia petrol!!! Ni ajabu kwamba sisi wasomaji tulishindwa kabisa kung'amua kuunganishwa kwa picha hizo (Photo magic!). Lakini mbona picha iliyopigwa (Kuunganishwa?) na kuchapwa kwenye gazeti la Mwananchi ni tofauti ni ile iliyo kwenye gazeti la Tanzania Daima? Au mheshimiwa sana ulibadili pozi namna ya vicheko na mikao? Na je, hiyo picha ya kweli uliyopiga na Vincent mlipiga mkiwa wapi? Kama ni eneo la tukio, utakuwa ni kiumbe wa ajabu sana unaechekelea kifo!!!!! Nassari aliamuru watu wake wakuuwe halafu ukaona ni mzaha fulani, ukacheka saaaaaaaaaaana, kana kwamba ulikuwa na uhakika wasingefanya chochote. Je, baada ya kuona tishio hilo ni dhaifu kiasi hicho, ulianzaje kwenda kushitaki.
  UCHAWI SIO TU KUBEBA TUNGURI, UNAFIKI NI UCHAWI MBAYA KULIKO UCHAWI WOWOTE. Wana Koogwe vijijini, huyu ndio mliemtuma kuwawakilisha mjengoni.
   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuhabarisha, lakini ifahamike kuwa magazeti ni biashara lazima yavutie wateja.
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Baba, mwana, au roho? maana wengine ni miungu na si mungu!
   
 18. M

  Miruko Senior Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe unamwamini huyu Majimarefu? Picha hiyo itengenezwe Mwananchi, pia Tanzania Daima nao watengeneze inayofanana na hiyo, wakati wako kwenye vyumba tofauti vya habari? Tumia kichwa chako walau kidogo.
   
 19. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kama Maji marefu anafanya propaganda basi nafikiri ccm wamekosa mtu makini wa kutrain wana propaganda wake!
   
 20. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Itakuwa kapigwa biti na akina Wassira ikabidi ajibaraguze kwa kudai ni 'photo-shop material'..
   
Loading...