Profesa Kabudi awasha moto Katiba Mpya

Tiba ya yote ni kubinafusisha TBC kisha mwekezaji aje na watu wake .

Zanzibar ndio wenye shida hawataki tatu hawataki moja wanataka mbili lakini wasiguswe. Yaani seti yao iwe kubwa kuliko ya Tanganyika ikiwa doted ndani ya duara zima la Zanzibar.
 
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amejibu baadhi ya hoja za watu wanaopendekeza muundo wa serikali mbili na kusema Serikali ya Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka serikali tatu mwaka 1984."

Aidha, amewashangaa wanaolibeza jina la Tanganyika kutumika serikalini kwa madai kuwa jina hilo siyo haramu kwa kuwa limo ndani ya Katiba ya sasa.

Alisema kuwa wakati huo madai ya serikali tatu yalitolewa na Zanzibar na kusimamiwa na Rais aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.

"Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza la Wawakilishi, Brigedia Mstaafu Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa Waziri Kiongozi), alikuwa akiongea kwa sauti nzito, kama ulikuwa ukimsikiliza, unasema muungano haupo," alisema Profesa Kabudi na kueleza kuwa Fakhi alisema: "Zanzibar siyo koloni la Tanganyika."

Alikuwa akichangia hotuba katika Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika mjini Zanzibar jana. Alieleza kwamba mjadala wa sasa wa muungano siyo mkali kama uliokuwepo mwaka 1983 na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla mzungumzaji kumaliza hotuba yake.

Katika maelezo yake, Profesa Kabudi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kuwa Fakhi alikuwa haongei kama mtu baki, bali aliagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

"Lugha ilikuwa ni kali," alisema.


Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal alisema kuwa masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
"Unawezekana kuwa muungano unatunyima fursa moja ua mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao, lakini wahakikishe wanawahudumia wananchi," alisema.

Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka CCM, wakiwamo Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu ya Katiba Mpya.

Kikwete pamoja na wajumbe hao kwa nyakati tofauti, walisema kuwa Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba haionyeshi uhalisia wa matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu muundo wa muungano.

Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal, alisema kuwa masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.

"Unaweza kuwa muungano unatunyima fursa moja au mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao lakini wanahakikisha wanawahudumia wananchi," alisema.

Akifafanua matumizi ya jina la Tanganyika kwenye Katiba ya sasa, Profesa Kabudi alisema: "Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya nne, 34, 64, 102 na 151, inaonyesha kuwa zipo mamlaka tatu. Mamlaka ya masuala ya muungano na mamlaka ya masuala yasiyo ya muungano katika upande wa Tanzania Bara (Tanganyika)."

Alibainisha: "Nataka niwaambie, leo ukienda kwenye Ibara ya 151 ya Katiba, Tanzania Bara imetajwa kuwa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, kwa hiyo hata Katiba ya sasa Tanganyika ipo, kwa hiyo Tanganyika siyo jina haramu."

Alisema anaamini kila taifa lina ujinga wake katika kutunga Katiba, lakini ujinga wa kizazi kimoja hauwezi kuwa wa kizazi kingine.
"Ujinga wa kizazi hiki, tusidhani utakuwa ujinga wa kizazi cha kesho, vizazi vijavyo vya Tanzania vitakuwa na ujinga wake."

Alifafanua: "Ni vyema kuwawekea misingi lakini waje kuishi na ujinga wao, kuliko kulazimisha ujinga wako, kwa sababu wewe ujinga wako ndiyo amali yako lakini kwa wengine siyo amali. Ulitegemea Waingereza wangekapigia mizinga kachanga ka siku moja?"

Hati ya Muungano


Akizungumzia hati ya muungano iliyozua sintofahamu hivi karibuni kwa madai kwamba haikuwepo, alisema msingi wa kikatiba na kisheria wa muungano wowote ni hati za muungano.

Alisema miaka ya 1980, suala lililokuwa linajadiliwa ni iwapo hati za muungano ni sehemu ya sheria za kimataifa au la. Baadaye ilibainika kuwa hati hizo ni mkataba wa kimataifa na kwamba unatawaliwa na sheria za kimataifa.

"Hili suala la kwamba hati zipo au hazipo siyo suala kubwa, suala ziliridhiwa? Ushahidi upo upande wa Tanganyika ziliridhiwa. Kwa upande wa Zanzibar kuna utata na hiyo kesi ipo mahakamani," alisema.

Alisema kutokana na utata huo katika Rasimu, wakapendekeza namna ya kutatua tatizo lililodumu kwa miaka 50 kwa kuandika kuwa hati ya maridhiano ya Tanganyika na Zanzibar kuwa msingi mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Kabudi ni professor wa nini hasa maana sijawahi kumsikia? au mbunge naye kama kuna anayejua anifahamishe maana anaongea kama mbunge wa ukawa au?

Le Mutuz System
 
Mimi nawashangaa sana hawa Wazanzibari CCM wakiwa kwenye BLW wakali kweli kama PILIPILI KICHAA kwamba wanataka serikali 3. Wakija Dodoma wapole sana kama PILIPILI HOHO wanataka serikali 2. Swali la kujiuliza Je, hawa Wazanzibari CCM wataendele kucheze hili shere hadi lini?
 
Wengi mmelisoma hili andiko la THE SO CALLED PROFESSOR kwa mihemko.
Binafsi sioni kama hotuba yenyewe INA hadhi ya kutolewa na professor.
Kama wewe ni professor unashindwa kuiona tofauti ya " TANZANIA BARA NA TANGANYIKA" lazima tuwe na wasiwasi na taaluma yako.
NO WONDER TUNAKUWA NA PRODUCT YA WASOMI WASIO NA ELIMU KAMA AKINA BEN SAANANE. kumbe walimu wenyewe ndio akina PALAMAGAMBA!!!!!!!!!!!!!!
 
Ningekuwa na uwezo wa kumshauri mwalimu wangu, dean wangu, na super visor wangu wa LL.B dissertation yangu, Prof. Palamagamba Kabudi, ningemshauri, aizamishe hii sense ya Tanganyika ndani ya vichwa vya CCM!. Hili ni suala tuu la kuwapatia elimu CCM, waelimike, waachane na ujinga wao wanaotaka kuulazimisha kwenye bunge maalum!.

Asante Prof. Kabudi, kulizungumzia hili.

Thanks.

Pascal.

Pascal huu ndo muda muafaka wa kuibua kipindi chako cha Kiti Moto.. wahoji wanaS3 na S3...ila usije na misimamo ya mpwa wako Pasco maana yule bana kuna siku uwa anachafua hali ya hewa na kukimbiaa...Ahasanta
 
Muungano wa Marekani hauna Kero wala Marais Wawili na Makamu wa Rais watatu sanjari na waziri mkuu na viongozi wengi Kama Muungano huu wa Ajabu uliosalia Duniani.muugano wao Rais ni mmoja tu na makamu wake,kisha Nchi zote zinaongozwa na magavana,Hakuna longo longo,Ulalamishi,Udini na Uchoyo wa Ardhi na Mafuta baharini, hata Michango ya Muungano hutolewa kwa wakati,na Zile Nchi ndogo ndogo hazina Utitiri wa wabunge na Viongozi kisha kutegemea Mishahara na posho kulipiwa na Nchi kubwa ! Kila Nchi imejipanga kulingana na watu wake,wapo makini muungano wao ni wa Ukweli si wa kinafiki hawana Wizara ya muungano wala Vioja Kama muungano wetu, Tatizo kubwa ktk muungano huu ni masilahi ya Wajanja ambao wapo tayari kwa gharama yeyote ili mladi Serikali mbili zibaki Waendelee kuvuna pesa , ingelikuwa ni busara sana Kama tunge copy staili hii ya Marekani angalau ingesaidia kuja na muungano nafuu kuliko ilivyo sasa muungano unaendeshwa kwa Hasara hauna faida kwa Watanganyika.

Pokea BONGE la like!!!
 
Pascal huu ndo muda muafaka wa kuibua kipindi chako cha Kiti Moto.. wahoji wanaS3 na S3...ila usije na misimamo ya mpwa wako Pasco maana yule bana kuna siku uwa anachafua hali ya hewa na kukimbiaa...Ahasanta
Asante Ben, kipindi ilikuwa kirudi siku nyingi, logistics zikikamilika, soon mtakiona hewani, ila ni kwa jina jingine!. Pasco achana nae kabisa, hana maana kabisa!, yeye kila siku anang'ang'ana na ukweli tuu, as if hajui siasa zetu ni za uongo uongo!. Afadhali yangu, kwenye ukweli nitasema, ila kwenye uongo nitajinyamazia!.

Paskali
 
Ulee muungano wa Nyerere na karume japo haukuwa na Hati ulikuwa muungano mzuri hakukua na Ujanja ujanja mwingi Kama Muungano huu wa sasa ambao umepenyeza mambo mengi Kienyeji kienyeji pasipo lidhaa ya Watanganyika matokeo yake Zanzibar wameibuka na Kuwa Nchi Kinyemela, tena kibaya zaidi Pesa ya kujijenga mpaka Kuwa Nchi inatoka Tanganyika,sasa Zanzibar wanawaona Tanganyika ni Mazoba na wapo million 44 lakini Wanapelekeshwa na Wazanzibar million 1.5 tu Kama Kondoo ! zimetumika pesa nyingi sana kwa ajili ya kuubembeleza Muungano ambao hauna faida kwa Watanganyika ,huku ZNZ akifaidika kwa mengi kwani Wamelundika Lundo la Watumishi wa Umma na Utitiri wa Wabunge kisha Wanategemea Mishahara itoke Tanganyika,kwa kweli ZNZ anainyonya Tanganyika hadi wamepitiliza sasa,cha ajabu Wazenji wanakula wakishashiba wanavulumusha Vuvuzela ili kuwapumbaza Watanganyika ambao walikuwa wamelala sasa wameanza kuamka ndio Maana wanaitaka Tanganyika irejeshwe haraka.

Funza
Nashukuru wewe umeulewa aina ya muungano tulio nao... muungano wa Changu Changu, Chako Chetu. CCM wameshindwa kuzuia hali hiyo Zanzibar na kuiruhusu kuwa nchi, sasa wanataka sisi tubebe upuuzi wao. Hatutaki - Tanganyika Daima.

Tunataka Muungano wenye usawa wa nchi mbili, na serikali ya muungano. Mapato na mchango kwa serikali ya muungano uwe kwa uwioano. Sio kuinyonya Tanganyika, halafu wanajidai eti wao ni koloni letu. Ni either waue ZNZ tuwe na serikali moja ya Tanzania au tuwe na serikali tatu.
 
Mimi nawashangaa sana hawa Wazanzibari CCM wakiwa kwenye BLW wakali kweli kama PILIPILI KICHAA kwamba wanataka serikali 3. Wakija Dodoma wapole sana kama PILIPILI HOHO wanataka serikali 2. Swali la kujiuliza Je, hawa Wazanzibari CCM wataendele kucheze hili shere hadi lini?

Kama umewaangalia wengi mi wajinga wajinga tu wachumia tumbo, hakuna cha maana wanachoongea pale zaidi ya kufikiria watajaza vipi choo.
 
Asante Ben, kipindi ilikuwa kirudi siku nyingi, logistics zikikamilika, soon mtakiona hewani, ila ni kwa jina jingine!. Pasco achana nae kabisa, hana maana kabisa!, yeye kila siku anang'ang'ana na ukweli tuu, as if hajui siasa zetu ni za uongo uongo!. Afadhali yangu, kwenye ukweli nitasema, ila kwenye uongo nitajinyamazia!.

Paskali,
Mkuu nimekuona leo TBC kwenye marudio ya kipindi fulani, nafikiri mlikuwa Mnazi mmoja. Unaelezwa na yule mama Umi kwamba hati za kuridhia muungano zipo za pande zote za muungano. Ulishindwa kumuuliza hata swali moja kwa hiki ambacho kimelalamikiwa hata na mzee Jumbe aliyekuwa mjumbe wa BMZ kwa miaka 20? Matter of fact, Pasco wa JF is doing better than you.
 
This time sujui ccm na usalama
wao wa taifa watamng'oa meno na kucha nani kwa maana kila kona ya nchi
mambo yamebana ba watu wanataka Tanganyika na Zanzibar yao...

Mm nipo tayari kung'olewa kucha na meno bila ganzi lakini Tanganyika yangu itarejea
 
Mkuu nimekuona leo TBC kwenye marudio ya kipindi fulani, nafikiri mlikuwa Mnazi mmoja. Unaelezwa na yule mama Umi kwamba hati za kuridhia muungano zipo za pande zote za muungano. Ulishindwa kumuuliza hata swali moja kwa hiki ambacho kimelalamikiwa hata na mzee Jumbe aliyekuwa mjumbe wa BMZ kwa miaka 20? Matter of fact, Pasco wa JF is doing better than you.
Mkuu Gagi, nakubaliana na wewe kabisa, mimi na Pasco wa jf ni watu wawili tofauti, mimi nafanya kitu kinaitwa "responsible journalism", nikipeleka kipindi TBC, nitauliza aina ya maswali yale tuu yakuvumilika TBC!. Responsible Journalism, ni uandishi/utangazaji wa uwajibikaji, hivyo nikipeleka kipindi TBC nakuwa responsible na TBCIISIM!. Pasco wa jf, hatumwi na yoyote, hamtumikii yoyote na hawajibiki kwa yoyote, yaani hayuko responsible kwa yoyote na yuko answerable to no one, hivyo anawezsa kusema lolote, chochote, popote, hajali kitu!, mimi najali!.
Paskali.
 
Mkuu Gagi, nakubaliana na wewe kabisa, mimi na Pasco wa jf ni watu wawili tofauti, mimi nafanya kitu kinaitwa "responsible journalism", nikipeleka kipindi TBC, nitauliza aina ya maswali yale tuu yakuvumilika TBC!. Responsible Journalism, ni uandishi/utangazaji wa uwajibikaji, hivyo nikipeleka kipindi TBC nakuwa responsible na TBCIISIM!. Pasco wa jf, hatumwi na yoyote, hamtumikii yoyote na hawajibiki kwa yoyote, yaani hayuko responsible kwa yoyote na yuko answerable to no one, hivyo anawezsa kusema lolote, chochote, popote, hajali kitu!, mimi najali!.
Paskali.
Utaniwia radhi mkuu wangu. Kama hii ndiyo responsible journalism, unafikiri kutakuwa na uhalali wowote wa kuendelea kuwa na nyie kama watumishi wa umma siku ccm ikiondolewa? Tunawafuatilia kwa uamkini msioweza kufikiria.
 
tunataka Tanganyika !!!!!!!!!!!!!!??
 
Pascally na wengine.....Kama uwasilishwaji wa Rasimu ungefanywa na Prof. Kabudi.....naamini pale Dodoma pasingelitosha, na ndio maana Deputy Speaker wa Bunge la JMT yuko very focused ktk hii issue, ujio wa mchakato, gharama na target all were wrong. Waamuzi hawakuwa ktk right track.....Professor Kabudi amenijibu kitu muhimu kilichoniumiza sana juu ya Waingereza na Tanganyika? Amethubutu kuifunua history ya nchi kwa umakini na dhati.....anachokosea Lissu ni maumbile yake kubeba sura ya jazba ktk uwasilishwaji wa hoja zake....ni maumbile, anahitaji Mshauri wa kumjenga udhibiti wa jazba na kuuvaa uhusika tuli, wenye lishe ya kweli ichagizwayo na minofu ya utajiri alojaaliwa wa hoja makini.

Prof. Kabudi aliwamiliki hadhira ile kwa hoja, upole, utafiti, vielelezo, kweli na udhati wake ulioikana papara na jazba.

Kabudi is someone needed by Samuel J. Sitta kuwaweka sawa wabunge juu ya rasimu.
 
Kuitambua Tanganyika kunazua hofu nyingi.
Lakin hofu zote zinatokana na watu kupenda utawala wa kudumu.
Mfano ni huu: Serikali tatu zitafufua upya wafu wawili ( TANU & ASP) hii maanayake nini? Hii iyasababisha kufa kwa kiumbe hai (CCM). Ikiwa hivo kitakachofata nini? Kitakachofata ni kutengeneza upya Katiba ya TANU yenye kuridhiwa na wengi. Baada ya hili kufanyika nadhani wote tunajua kitakachotokea!!? (Miungu watu katika Chama na Serikali watakua wamekatwa makali). So chakufanyika, ni kuipinga ibara hii ya muundo wa muungano kwa Nguvu zao zote.
 
Back
Top Bottom