Profesa anathibitishwa na taasisi gani?

kukumsela

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
721
907
Kama ilivyo ada katika taalumu kama Law kuna shule ya sheria, uhasibu kuna NBAA nk. Lakini licha ya kufahamu kuwa ili mtu awe Profesa especially Tanzania ni lazima awe na Shahada ya Uzamivu yaani PhD na kufanya tafiti mbalimbali na machapisho, naomba kujua kuna taasisi au tume ya kumthibitisha mtu kuwa Profesa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
naomba kujua kuna taasisi au tume ya kumthibitisha mtu kuwa Profesa?
Kwa vyuo vikuu vya serikali hiyo ni kazi ya Baraza la Senate la Chuo na mwisho kabisa Baraza la Chuo (yaani Council) ambaye ndiye "mwajiri" ingawapo kwa siku hizi utumishi/w.fedha ndio wanatoa mshahara moja kwa moja.
 
Kwanza nikurekebishe ya kwamba u Professor ni cheo na sio elimu. Elimu inaishia ngazi ya PhD. Kwa huku kwetu ukiwa na PhD cheo chako kitakuwa Senior Lecturer then ukipublish unakuwa Associate Professor na baadae Professor.

Je PhD inathibitishwaje? Kamati katika chuo husika inaundwa inategemea na chuo, lakini sehemu nyingi kunakuwa na external examiner mmoja na Internal either wawili au zaidi. Watapitia thesis yako then watashauri kulingana na utaratibu wa chuo. Baadae mwanafunzi unaitwa kupresent either kwa kamati tu au publicly kuhakiki kama kweli kazi hiyo ni yako. Baadae unapewa muda wa kufanya marekebisho kama yapo then baadae unatunukiwa PhD kutokana na ile report ya examiners.

Kama ulivyozungumza mleta mada kuwa kuna board mbalimbali za kitaalum, kwa maana hiyo Professor pia atawajibika kwenye board yake ya kitaaluma. Kama ni daktari, basi atawajibika kwa TMC and alike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ilivyo ada katika taalumu kama Law kuna shule ya sheria, uhasibu kuna NBAA nk. Lakini licha ya kufahamu kuwa ili mtu awe Profesa especially Tanzania ni lazima awe na Shahada ya Uzamivu yaani PhD na kufanya tafiti mbalimbali na machapisho, naomba kujua kuna taasisi au tume ya kumthibitisha mtu kuwa Profesa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Pamoja na yote yaliyo zungumzwa !Mimi nataka kujibu swali moja tu kati ya mengi uliyo uliza "Je,kuwa professor lazima uwe na PhD? Kwa asilimia kubwa kwa baadhi ya taaluma ni lazima lakini kwenye taaluma ya medicine siyo lazima !Nitafafanua

Master's degree ya kozi yoyote nje ya udaktari ni miaka mitatu huitwa Master's of medicine(MMED) !Ikiwa mhitumu wa kozi hii ata kuwa ni mkufunzi pamoja na Master's yake huitwa Lecturer Kama ilivyo kwa Mwenye PhD ,tofauti na taaluma nyingine ambapo akiwa MSc,MA ,MBA au MPH huitwa Assistant Lecturer!..MMED ambaye ni Lecturer baada ya publication hupata promotion na kuwa Sinior Lecturer Kama ilivyo kwa PhD holder.Lakini assistant Lecture hawezi kuwa Lecturer mpaka awe amesoma PhD!.Vilele baada ya publication huyu mwenye MMED kwa kuwa alikuwa Sinior Lecturer,Board ya chuo inaweza kumpa u-professor Ingawaje hakuwa na PhD

Only in Medicine !
 
Kwanza nikurekebishe ya kwamba u Professor ni cheo na sio elimu. Elimu inaishia ngazi ya PhD. Kwa huku kwetu ukiwa na PhD cheo chako kitakuwa Senior Lecturer then ukipublish unakuwa Associate Professor na baadae Professor.

Je PhD inathibitishwaje? Kamati katika chuo husika inaundwa inategemea na chuo, lakini sehemu nyingi kunakuwa na external examiner mmoja na Internal either wawili au zaidi. Watapitia thesis yako then watashauri kulingana na utaratibu wa chuo. Baadae mwanafunzi unaitwa kupresent either kwa kamati tu au publicly kuhakiki kama kweli kazi hiyo ni yako. Baadae unapewa muda wa kufanya marekebisho kama yapo then baadae unatunukiwa PhD kutokana na ile report ya examiners.

Kama ulivyozungumza mleta mada kuwa kuna board mbalimbali za kitaalum, kwa maana hiyo Professor pia atawajibika kwenye board yake ya kitaaluma. Kama ni daktari, basi atawajibika kwa TMC and alike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo mwanzo uko sawa, isipokuwa PhD in most cases inaruhusu wewe kuajiliwa kama Lecturer kama una vigezo vingine na sio Senior Lecturer. Mwisho hauko sawa kabisa kwani kama ulivyosema kuwa u-professor ni cheo na cheo hutolewa na mwajiri. Mwajiri wa chuo kawaida ni Council ya Chuo, lakini lazima Baraza la Senate (baraza la taaluma kwa chuo kikuu chochote) lijiridhishe kuwa una vigezo stahili. Wao wakishakubali hupeleka jambo lako kwa Council ambayo ki kawaida inapitisha na kuthibitisha kuwa Senate wamefanya kazi kama ilivyotakiwa. Council ndio hukuandika barua kuwa fulani bin/binti fulani sasa umepandishwa cheo kuwa associate prof au professor (kamili). Bodi za kitaluuma for regulartory purposes hazihusiki kabisa kwenye hili.
 
Msome mleta mada alichouliza hopefully utamuelewa

😆😆😆profesa wa jalalani njoo huku mkulima anataka kushika chuo Cha maprofesa
 
Kwanza nikurekebishe ya kwamba u Professor ni cheo na sio elimu. Elimu inaishia ngazi ya PhD. Kwa huku kwetu ukiwa na PhD cheo chako kitakuwa Senior Lecturer then ukipublish unakuwa Associate Professor na baadae Professor.

Je PhD inathibitishwaje? Kamati katika chuo husika inaundwa inategemea na chuo, lakini sehemu nyingi kunakuwa na external examiner mmoja na Internal either wawili au zaidi. Watapitia thesis yako then watashauri kulingana na utaratibu wa chuo. Baadae mwanafunzi unaitwa kupresent either kwa kamati tu au publicly kuhakiki kama kweli kazi hiyo ni yako. Baadae unapewa muda wa kufanya marekebisho kama yapo then baadae unatunukiwa PhD kutokana na ile report ya examiners.

Kama ulivyozungumza mleta mada kuwa kuna board mbalimbali za kitaalum, kwa maana hiyo Professor pia atawajibika kwenye board yake ya kitaaluma. Kama ni daktari, basi atawajibika kwa TMC and alike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeandika na kueleza vizuri lakini masahihisho kidogo tu ni kuwa kuwa na PhD sio tiketi ya moja kwa moja kuwa Senior Lecturer, Senior Lecturer ni cheo cha kazi kama ilivyo Professor na inahitaji upublish ili kufika ngazi hiyo, na kuna point zinazohitajika kutokana na machapisho na muda wa kufundisha
 
Shukrani mkuu kwa marekebisho. Kwa wenzetu nchi nyingine ukimaliza PhD ajira yako inakuwa ni assistant professor then associate professor to full professor. Kama ulivyosema, publication zitakufanya upande haraka.
Umeandika na kueleza vizuri lakini masahihisho kidogo tu ni kuwa kuwa na PhD sio tiketi ya moja kwa moja kuwa Senior Lecturer, Senior Lecturer ni cheo cha kazi kama ilivyo Professor na inahitaji upublish ili kufika ngazi hiyo, na kuna point zinazohitajika kutokana na machapisho na muda wa kufundisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nikurekebishe ya kwamba u Professor ni cheo na sio elimu. Elimu inaishia ngazi ya PhD. Kwa huku kwetu ukiwa na PhD cheo chako kitakuwa Senior Lecturer then ukipublish unakuwa Associate Professor na baadae Professor.

Je PhD inathibitishwaje? Kamati katika chuo husika inaundwa inategemea na chuo, lakini sehemu nyingi kunakuwa na external examiner mmoja na Internal either wawili au zaidi. Watapitia thesis yako then watashauri kulingana na utaratibu wa chuo. Baadae mwanafunzi unaitwa kupresent either kwa kamati tu au publicly kuhakiki kama kweli kazi hiyo ni yako. Baadae unapewa muda wa kufanya marekebisho kama yapo then baadae unatunukiwa PhD kutokana na ile report ya examiners.

Kama ulivyozungumza mleta mada kuwa kuna board mbalimbali za kitaalum, kwa maana hiyo Professor pia atawajibika kwenye board yake ya kitaaluma. Kama ni daktari, basi atawajibika kwa TMC and alike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye ku " publish" unatuacha asante kwa maelezo. Tafadhali una publish nini na kwa nani. Nitashukuru kama wajuzi mtatunyoshea hapo. Tumieni kiswahili tu fasaha ukiswanglish utatuacha. Asante.

Ku publish maana yake ni kutoa machapisho ya kitaaluma, machapisho hayo ni kutangaza matokeo ya tafiti mbalimbali ulizofanya au ulizoshiriki kufanya, lengo la kwanza ni kama nilivyosema hapo juu kusambaza habari za tafiti lakini pia kutoa masuluhisho ya changamoto mbalimbali lakini pia ni kuelimisha jamii! Lengo la pili ni la kitaaluma unachapisha ili upande ngazi au upandishwe cheo kuna msemo huko vyuo vikuu unasema "Publish or Perish". Kwa hiyo ili upande ngazi na kupata maslahi mazuri kwa wanataaluma kuanzia ngazi ya Assistant lecturer to Associate Professor ni lazima utoe machapisho! ili kufikia kiwango fulani cha points! ila ukifika ngazi ya Full Professor machapisho ni kwa ajili ya kutoa tu mchango kwenye jamii maana hakuna promotion zaidi ya hapo (kwa ufahamu wangu)! Natumai nimejibu swali lako!
 
Asante sana Mkuu nimeelewa vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[QUOTE="Kilembwe, post: 33817642, member: 18291"Natumai nimejibu swali lako![/QUOTE]@@

NJE YA MADA

Naona hili nalo unaweza kunisaidia:

Niliwahi kumpatia takwimu fulani mwanafunzi wa UDSM aliyekuwa ana somea nadhani mambo ya Maji.
Kila mara alinifuata kujadili kuhusu zile takwimu na baadae akaniambia
Rafiki yangu degree nime dedicate kwako pia.

Nilielewa ana maana nimetoa mchango fulani ktk masomo yake.

Ila baada ya hapo sikumwona tena mpaka leo. Sasa ile dedication nashindwa kuelewa mimi nitampata wapi na je inahusika vipi ulazima wa yeye ku dedicate hii inamsaidiaje yeye au mimi kitaaluma.

Ingawa nakiri kuwa baada ya hapo niliona Boss ananiamini sana huenda alimwaga sifa kwa Boss kabla ya kuniambia mimi kuhusu hiyo dedication.

Nitashukuru kama utaninyoshea hapo pia naona wewe umepita huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom