Profesa Abdulaziz Lodhi bingwa wa taaluma za Lugha

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,400
24,323
SIMULIZI NDEFU ZA KUVUTIA ZA PROF. ABDULAZIZ LODHI, KTK MAHOJIANO MAREFU NA MTAYARISHAJI WA KIPINDI CHA GUMZO LA GHASSANI



Mzalendo mzanzibari Profesa Abdulaziz Lodhi, bingwa wa taaluma za Lugha anasimulia Zanzibar kabla ya uhuru na baada ya Mapinduzi pia mchango wake ktk elimu Zanzibar na Tanzania bara baada ya Muungano. Asimulia jinsi alivyoshiriki kuzika miili ya watu kufuatia mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyotokea Zanzibar na jinsi alivyoshirikiana na makomredi wa Umma Party kurudisha hali ya usalama Zanzibar ...siku chache baada ya Mapinduzi.

Ualimu wake sekondari ya St. Xavier (Kibasila) na Agha Khan zote za Dar es Salaam kabla ya kuondoka Tanzania kwenda nje kusoma zaidi mwaka 1968 na mchango wa Profesa A.Y Lodhi katika kuanzishwa chuo kikuu na vyuo vya elimu ya juu Zanzibar SUZA.


Harakati zake akiwa mmoja wa viongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania na All Zanzibar Students' Union (AZSU) kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishirikiana na vyama vyote vya kisiasa bila kujali itikadi za Umma Party, Afro Shirazi Party, Hizbu n.k.

Zanzibar mwaka 1960 ilikuwa na zaidi ya wanafunzi 300 katika vyuo vikuu seems mbalimbali ulimwenguni.

Source : Gumzo la Ghassani

Dr. Abdulaziz Y. Lodhi (b. 1945, Zanzibar) is Professor Emeritus at the Dept. of Linguistics and Philology, Uppsala University, Sweden. He has published extensively on Swahilistics, East African Social Studies and Zanzibar Affairs. Currently he is also a Member of the International Scientific Committee (ISC) of the Slave Route Project: History and Memories for Dialogue, Unesco, Paris. Zanzibar Revolution revisited: A short review essay | Pambazuka News

Wasomi vijana wengi waliondolewa katika utumishi serikalini Zanzibar baada ya mapinduzi na kupelekwa Tanzania bara walipopewa kazi katika shule za sekondari na vyuo mfano Haroub Othman, Maalim Ali Ahmed Jahadhmi na Maalim Sultan Mugheiri ambao sasa ni wanataaluma wahadhiri wakubwa nchini Marekani na Maalim Salim Kifua huko Japan.

Wengine kina Maalim Shaaban Saleh Farsy and Maalim Said Iliyas waliingizwa kutafsiri Military Code na sheria za Tanzania toka kiingereza kwenda Kiswahili na Maalim Jaafar Tejani alipelekwa UDSM taasisi ya utafiti wa Kiswahili Kiswahili Research at the University of Dar es Salaam pia kuongoza kuanzishwa kwa kamusi ya kiswahili mradi uliokuwa chini ya Ofisi ya Rais Dar es Salaam .

Profesa Abdulaziz Lodhi mtaalamu wa lugha na historia za lugha za waBantu pia ni mwandishi wa vitabu kadhaa tajwa kikiwemo cha Institution of Slavery Zanzibar n.k

Profesa A.Y Lodhi anasisitiza umuhimu wa kusoma pia kufahamu Fasihi na historia katika lugha za kiSwahili na Kiingereza.
 
Back
Top Bottom