Prof. Wajiri Sanganyi(US): Ujumbe wangu kwa Vyama Pinzani nchini Tanzania

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Anaandika Prof.Wajiri Sanganyi(US).

Nina wasalimia kutoka huku kwa bwana Trump ambapo tupo huku kimajukumu,Ila tukiendelea kufuatilia yote ambayo yanaendelea nyumbani huko Tanzania.

Nimeshiriki siasa za upinzani huko Tanzania miaka ya 1991 nikiwa na akina Juliasy Miselye ,Prosper Rwegoshora,Peter Golugwe,akina Thao,Mgeta, Leo Lwekamwa. Leo Lwekamwa sasa hivi yeye yupo huku US, wakati huo tukiwa TLP.

Leo ninataka nitoe ujumbe huu kwa viongozi na wanachama wa vyama pinzani.Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa siasa zinazoendelea sasa hivi nchini kwetu Tanzania.Hasa upande wa CCM , vyama pinzani, chadema na ACT-mzalendo.Mnapitia changamoto kadhaa poleni.Ni changamoto ambazo hata sisi tulipitia huko nyuma wakati wa Nyerere,Mwinyi na Mkapa.


Naomba leo nizungumzie kuhusu upinzani tuu.Kwa namna ninavyoamini vyama vikubwa vya upinzani Tanzania kwa sasa ni vyama viwili tuu, Chadema na ACT mzalendo mnikosoe nikikosea.

Ninataka kuwaambia viongozi wa vyama pinzani nchini Tanzania hasa Chadema chini ya mtoto wangu Mbowe na ACT mzalendo chini ya mtoto wangu Zitto.

Lazima mfahamu kwanza vyama huwa havidumu milele bali vinazakiwa,vinakuwa na hufikia muda vinakufa au vinakosa nguvu kabisa.Hii sio hiari ni kanuni (Party is formed,grow and witheraway).

Siasa za vyama hivi viwili kati ya Chadema na ACT mzalendo ni siasa za kugombea kuishi (Survival for the fittest).Chadema wapo katika kilele cha ukuaji(Grey step/Peak step),Act mzalendo ndio wanaanza ukuaji hasa baada ya kumpokea Maalimu Seif hivyo wanapambana kukuwa.

Nina rafiki zangu wapo Chadema mara zote huwa wakiniambia kwamba Chadema haiwezi kuunganisha nguvu na ACT mzalendo kwani ACT mzalendo ni chama kidogo sana.Mimi huwa nina washauri Chadema kama wanahitaji waendelee kuwepo katika midani ya siasa ni lazima waunde umoja na ACT mzalendo pia na vyama vingine pinzani katika chaguzi.

Huwa nina ambia rafiki zangu huko Chadema kwamba wasitiwe upofu na wingi wa wabunge walio nao ,hao walipatikana mwaka 2015 tuu sio guarantee ya kuendelea kuwapata katika chaguzi zijazo bila nguvu ya umoja.Hivyo kudharau vyama vingine wanavyoita vidogo sio vyema hata kidogo .Sisi tulio watangulia tunajua hayo.Nina wapa mifano kuanzia uchaguzi wa 1995 , 2000,2005,2010,2015

Mwaka 1995,NCCR ilikuwa chama pinzani kikuu chenye nguvu kipindi hicho chini ya Mbatia , Anthony Komu,Masumbuko Lamwai,Ringo Tenga,Mvungi na Mrema.

Uchaguzi wa 1995 ,Mkapa wa CCM alipata kura 4026422 sawa na asilimia 61.82 akifuatiwa na Mrema akiwa Chama kikuu cha upinzani NCCR alipata kura 1,808,616 sawa na asilimia 27.77,vikifuatiwa vyama vingine vya upinzani .Nakumbuka Mkoa wa Dar es salaam wakati ule Mrema alipata kura nyingi sana hatimaye uchaguzi ule mkoa wa Dar ulifutwa .

Miaka mitano kupita ulikuwa uchaguzi wa 2000 ,awamu ya pili ya Mkapa.Matokeo Mkapa kura 5,863,201 asilimia 71.74 ,Sasa hivi karata ilibadilika sio NCCR tena ilikuwa CUF chini ya lipumba akipata kura 1,329,077 asilimia 16, akifuatiwa na TLP baada ya Mrema kuhamia TLP kutoka NCCR ,NCCR ikawa ya Mwisho hata wabunge ikashindwa na TLP.Nakumbuka TLP waliopata wabunge 16 pia kuongoza Halmashauri ya Moshi, nakumbuka kipindi hicho msajili George Liundi alitaka kukifuta chama cha TLP kabla ya uchaguzi wa 2000 ,baada ya uchaguzi wa 2000 TLP chini ya Leo Lwekamwa na akina Thao ,Mselya,Mgeta ikawa ponapona yao.

Chama cha NCCR kilipotelea mbali naambiwa sasa hivi kina Mbunge mmoja James Mbatia.

Uchaguzi wa 2005 , Kikwete wa CCM alipata kura 9,123,952 sawa na asilimia 80.28 , akifuatiwa na CUF ya Lipumba wakati huo kura 1327125 , akifuatiwa Mbowe wa Chadema kura 668,756 asilimia 5.88

Hapo ndipo ilikuwa mwisho wa Chama cha NCCR,TLP na CUF kama vyama vikuu vya upinzani nchini Tanzania.

Uchaguzi 2010 Kikwete wa CCM alipata asilimia 62.83 na chama pinzani kilichoongoza ni Chadema mgombea wake Dr.Slaa asilimia 27.05 akifuatiwa na Lipumba CUF asilimia 8.28

Na 2015 aliongoza Magufuli wa CCM na upinzani ni ukawa Lowasa.

Hii ni mifano dhahiri ili Chadema wajue kwamba ponapona yao kama chama kikuu cha upinzani ni Umoja miongoni mwa vyama pinzani.Ndio nafasi yao ya kuendelea kuishi bila njia hiyo ni rahisi chama hicho kufa mapema kama vyama vingine namna vilivyokufa.

Wafuasi mara zote hubadilika baada ya kuona chama kimepoteza mvuto au kuzeeeka,wafuasi waliacha NCCR 2000 waka Support CUF na TLP ,waliacha TLP 2005 waka Support CUF na Chadema,2010 wafuasi waliacha CUF waka Support Chadema ,2015 ilikuwa ukawa ndio Chadema ikapata wabunge wengi wanaoringia sasa bila umoja tena wa vyama pinzani chadema mtaongea habari nyingine mara nyingi huwa nina waambia .

Hivyo kwa aina ya Siasa za sasa Chadema haipaswi kudharau kabisa chama cha ACT mzalendo kwa kutamka hawawezi kuungana.ACT mzalendo naambiwa kimeenea Zanzibar kote , bila kusahau lazima tufahamu kwamba siasa za Zanzibar ni za tofauti na bara.Zanzibari hata wasipoungana ikisimama ACT tuu uwezo wa kupambana na CCM upo mkubwa na kupata viti hata kura nyingi.

Ila huko bara Chadema na ACT mkusimama pekeenu,mtafanywa kama kwenye chaguzi za marudio (Wabunge na Madiwani) , pia serikali za mitaa.

Kwa mfano Chadema na ACT mzalendo huko bara mkikosa jimbo hata moja bila kuungana , Zanzibar ACT mzalendo itapata viti hivyo na ACT kuwa chama kikuu cha upinzani kupitia Zanzibar sababu siasa zao ni tofauti na huko bara.

Mimi nina jua kuwa Chadema kinachukia sana kukuwa kwa ACT mzalendo hasa baada ya Maalim Seif kuhamia ACT mzalendo,chuki za namna hiyo zipo sana katika siasa za upinzani .Kuhama kwa Maalim Seif kwenda ACT mzalendo ilikuwa ni sawa na kuhama kwa Mrema kutoka CCM kwenda NCCR.

Mrema akiwa CCM alikuwa na cheo cha Naibu waziri Mkuu na waziri wa wizara nchini.Wakati huo Mrema alikuwa Mrema ,Mrema kweli .Alipo hama kutoka CCM alitakiwa kwenda TLP kwa akina Leo Lwekamwa na ikatakiwa awe mwenyekiti wa TLP ,akina Leo Lwekamwa akakubali kujiuzulu na wakaenda badili jina la mwenyekiti kwa msajili wakati huo ni George Liundi hivyo kujiandaa kumpokea Mrema ili aingie TLP,wakafunga Safari hadi Moshi kumchukua Mrema.Walipofika wakapata taarifa kwamba Mrema ameshawishiwa na NCCR hivyo amejiunga na NCCR.

Akina Leo Lwekamwa waliishiwa nguvu hivyo kuanzia 1995 hadi 2000 TLP walikuwa na chuki kubwa dhidi ya NCCR ,hii ndivyo ilivyo sasa kwa Chadema dhidi ya ACT mzalendo hasa baada ya Maalim Seif kuhamia chama hicho ikiwa cha ACT mzalendo wakati Chadema wakati huo waliniambia walikuwa tayari wamerekebisha ofisi yao kubwa Makao makuu Chadema Zanzibar ipo Kikwajuni.Chadema walikasirishwa kwa kwa hoja ya kwamba Maalim kwenda katika chama kidogo ACT mzalendo ni kuvunja nguvu ya upinzani alipaswa kuja katika chama kikuu cha upinzani bara ili kiwe tena nguvu Zanzibar ,hii ni chuki kubwa dhidi ya ACT mzalendo .

Ndio maana , uchaguzi serikali za mitaa hawakuungana na kwa taarifa nilizopewa uchaguzi mnafanya mwaka huu CHADEMA hawataki kuungana.

Ukweli ni kwamba mtu mwenye umri wa miaka 60 huwezi kumpa umri wa kuishi (Life expectancy) ya miaka 50 ijayo huwa ni vigumu atakuwa aidha mzee sana hajiwezi au kufa huo ndio mfano wa Chadema kwa sasa, Chadema hakina miaka 10 mbele nipo mtaniambia.Ila ni rahisi kwa mtoto wa miaka 15 kumtabiria kuishi (life expectancy) miaka 50 ijayo,mfano huu ni sawa na ACT wazalendo .

Lazima tuelewe kwamba Chadema umri wake sasa upo kileleni ,hakuna Chadema zaidi ya ile ya 2005,2006,2008,2009,2010,2011,2012,2013,2014,2015 no more Chadema badala yake kuna rise up ya chama kingine cha upinzani hii ndio principle hata ACT wazalendo itakufa tuu.

Hivyo Raia yangu ili huko Tanzania kuendelee kuwa na mfumo wa vyama vingi imara kuunganisha nguvu ni jambo lisilo kwepeka , watoto zangu Mbowe na Zitto Kabwe zingatieni hayo.

Good Day ,Tanzanians.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Surreal !! Republican Vs Democrats wameishi over 200yrs, still strong, as well as Labour Vs Concervatives, ANC Vs DA, logic ya professor huyu haipandi

labda aseme vyama vitayarishe warithi vijana....

Hata mimi nimejaribu kumuelewa kwenye ishu ya vyama kuzaliwa, kukua na kisha kufa, nikashindwa kuipata mantiki...

Yaani yeye, kwa kuwa TLP, NCCR na CUF viliishi miaka isiyozidi 10 na kutoweka amechukulia ndiyo kawaida na itakuwa hivyo kwa vyama vingine...

Umemtolea mifano ya Democrat na Republican (USA) na Conservative na Labour (UK) kwamba vimeishi miaka zaidi ya 200 sasa, nadhani atakuelewa....

Aidha hata hapa TZ, CCM iko kwa miaka zaidi ya 50 sasa. Kwa nini vya kufa viwe hivyo vingine tu?

Prof. kwa uzoefu wake ktk siasa kama anavyojinasibu, angejikita zaidi ktk kushauri na kuelekeza mbinu na njia sahihi na bora kukifanya chama cha siasa kuishi maisha marefu.....

Halafu anazungumzia ishu ya vyama kuungana kana kwamba hajui mazingira ya kikatiba na kisheria ya TZ kuwa hayaruhusu vyama kuungana unless mmeviua kwanza na kuanzisha chama kipya...

Labda kama ni ishu ya MASHIRIKIANO hiyo inaeleweka. Na ndivyo ilivyokuwa katika GE ya 2015 na naamini ndivyo itakavyokuwa mwaka huu 2020....

Tunachoweza kuwashauri vyama pinzani dhidi ya chama kinachoongoza serikali, ni kurekebisha kasoro zilizojitokeza mwaka 2015 hata maeneo mengine kukawa hakuna kuelewana katika mashirikiano yao na kujikuta kwenye migongano iliyoathiri kura zao na kujikuta wagombea wa CCM wakipata faida ya kutoelewana kwao na kujikuta wanashinda kata (udiwani) na jimbo (ubunge)...

Asante
 
Maneno haya ni mabebo ya busara na halisia.

Kama kuna jambo ambalo limekuwa likituvunja moyo wananchi wengi, ni kushindwa kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuwa na muungano wenye nguvu.

Kama ninyi viongozi tu mnashindwa kuwa na mwungano wenye nguvu, mkipata madaraka, mtawezaje kuwaunganisha mamilioni ya Watanzania.

Kuwa na muungano wenye nguvu kwa vyama vya upinzani, uwe mtihani wao wa kwanza ili kujua kama wana uwezo wa kuongoza au hawana. Hapa nazungumzia muungano wa vyama vya upinzani halisi. Siyo vyama mamluki. Na tunaposema vyama mamluki, kuwe na uthibitisho hasa kuwa chama hiki ni chama mamluki, na siyo hisia.

MBOWE, ZITO, MAALIMU, RUNGWE - Mtuambie kama mna uwezo wa kuongoza au hapana?

Uwezo wenu wa kuongoza tutaupima katika kujenga mshikamano wa vyama vya upinzani wenye nguvu au uundwaji wa chama kimoja chenye nguvu. Kuna sababu huwa mnazitoa lakini ni sababu ambazo hazina maana wala msingi.

Sitahangaika na uchaguzi kama vyama hivi, kila kimoja kitaenda kama kilivyo. Kwa sasa naamini Zito/ACT wapo tayari, tatizo lipo kwa CHADEMA.
 
Sijalielewa lengo hasa la huyu Professor ni lipi? Maana naona amejikita katika kuitisha zaidi CHADEMA huku akilazimisha kwamba ACT ndiyo mbadala.

Anakiri mwenyewe kwamba CHADEMA kwa hivi sasa ni chama kikubwa, ila kwa kuwa haupendi ukubwa huo wa CHADEMA, na anaupuuza kwa kudai upo kwenye peak na hivyo hauna muda mrefu. Anakiri kwamba ACT ni Chama kidogo ila life expectancy yake ni kubwa hivyo ina matumaini na attention yake ipo kule anachosahau ni kwamba udogo au upya wa Chama haukipi gurantee ya kukua, kwani akina Dovutwa na wenzao nao waliibuka na vyama vyao, yaani vilikuwa vidogo lakini vimeishia kudumaa.

Simshangai Professor huyu kwa kuamini kwamba maisha ya vyama vya siasa ni ya muda mfupi sana. Kama anaamini mafanikio ya vyama vya siasa ni lazima kuwa na mtu fulani, then yupo sahIhi. Hajaelezea kimuundo na kimfumo ni namna gani amejiridhisha kwamba ACT ndiyo kitakuja kuwa Chama kikuu cha upinzani, bali matumaini yake ni sababu ya Maalim Seif kujiunga na ACT na hivyo kuwa na uhakika na viti vingi kutoka Zanzibar. Haipi nafasi yoyote ile ACT upande wa kule bara na kwa makusudi anakwepa kuongelea nafasi ya ACT kule bara ila anaitisha CHADEMA kwa matarajio ya nafasi ya ACT kule Zanzibar.

Profesor anaishawishi CHADEMA yenye muundo na mtandao unaoeleweka na wenye nguvu ijiunge na ACT inayotaka kusimama kwa kujishikilia kwenye kanzu ya Maalim Seif (What a Joke)?
 
Surreal !! Republican Vs Democrats wameishi over 200yrs, still strong, as well as Labour Vs Concervatives, ANC Vs DA, logic ya professor huyu haipandi

labda aseme vyama vitayarishe warithi vijana....
Umeona? Kila Nchi unataja vyama vikuu viwili, wapi umeona vitatu au zaidi??? Hapa Tanzania kimoja ni CCM, cha pili ni kipi??

Sasa hicho Cha pili ndicho kinatakiwa kiundwe na ili kiwe na nguvu Kama CCM kinahitaji muunganiko. Rahisi tu
 
Surreal !! Republican Vs Democrats wameishi over 200yrs, still strong, as well as Labour Vs Concervatives, ANC Vs DA, logic ya professor huyu haipandi

labda aseme vyama vitayarishe warithi vijana....
Mzee unalinganisha apples na Oranges?
Siasa za Marekani au Ulaya ni tofauti sana na za hapa Tanzania.

Kiwango cha uelewa cha wanachama na wafuasi wake ndio shida kubwa kwa siasa za Afrika.
 
Anaandika Prof.Wajiri Sanganyi(US).

Naomba leo nizungumzie kuhusu upinzani tuu.Kwa namna ninavyoamini vyama vikubwa vya upinzani Tanzania kwa sasa ni vyama viwili tuu, Chadema na ACT mzalendo mnikosoe nikikosea.

Siasa za vyama hivi viwili kati ya Chadema na ACT mzalendo ni siasa za kugombea kuishi (Survival for the fittest).Chadema wapo katika kilele cha ukuaji(Grey step/Peak step),Act mzalendo ndio wanaanza ukuaji hasa baada ya kumpokea Maalimu Seif hivyo wanapambana kukuwa.

Hivyo Raia yangu ili huko Tanzania kuendelee kuwa na mfumo wa vyama vingi imara kuunganisha nguvu ni jambo lisilo kwepeka , watoto zangu Mbowe na Zitto Kabwe zingatieni hayo.

Good Day ,Tanzanians.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Abdul Nondo, naunga mkono hoja.
Hili la Chadema kuungana na ACT hata mimi niliwahi kushauri


P
 
Kaka Mayalla huyu Prof ,nimemuelewa Mimi binafsi hasa katika suala la Chadema na Act kuwa pamoja
Mkuu Abdul Nondo, naunga mkono hoja.
Hili la Chadema kuungana na ACT hata mimi niliwahi kushauri


P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Surreal !! Republican Vs Democrats wameishi over 200yrs, still strong, as well as Labour Vs Concervatives, ANC Vs DA, logic ya professor huyu haipandi

labda aseme vyama vitayarishe warithi vijana....
Utaikataa lkn ndio ukweli, vyama ulivyotaja ni kweli vinaishi lkn elewa kuwa hakuna utitiri wa vyama labda ingekuwa CDM na CCM au CCM na ACT sasa hivi ni vingi mno
Lingine hakuna muungano wao dhidi y chama tawala.
Ccm ina miaka 43 ina nguvu za kinidhamu, kimuundo na kifedha.
Kushinda labda iwe miujiza kwa upinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno haya ni mabebo ya busara na halisia.

Kama kuna jambo ambalo limekuwa likituvunja moyo wananchi wengi, ni kushindwa kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuwa na muungano wenye nguvu.

Kama ninyi viongozi tu mnashindwa kuwa na mwungano wenye nguvu, mkipata madaraka, mtawezaje kuwaunganisha mamilioni ya Watanzania.

Kuwa na muungano wenye nguvu kwa vyama vya upinzani, uwe mtihani wao wa kwanza ili kujua kama wana uwezo wa kuongoza au hawana. Hapa nazungumzia muungano wa vyama vya upinzani halisi. Siyo vyama mamluki. Na tunaposema vyama mamluki, kuwe na uthibitisho hasa kuwa chama hiki ni chama mamluki, na siyo hisia.

MBOWE, ZITO, MAALIMU, RUNGWE - Mtuambie kama mna uwezo wa kuongoza au hapana?

Uwezo wenu wa kuongoza tutaupima katika kujenga mshikamano wa vyama vya upinzani wenye nguvu au uundwaji wa chama kimoja chenye nguvu. Kuna sababu huwa mnazitoa lakini ni sababu ambazo hazina maana wala msingi.

Sitahangaika na uchaguzi kama vyama hivi, kila kimoja kitaenda kama kilivyo. Kwa sasa naamini Zito/ACT wapo tayari, tatizo lipo kwa CHADEMA.
Huu ndio ukweli wapinzani wasiotaka kusikia ndio hapo huwa najua Tz hatuna upinzani ktk ngazi za viongozi wa juu, upinzani ni raia wa kawaida mtaani.
Jiulize assume watu mil 5 wajiandikishe na watokee kupiga kura .
Halafu vyama Ccm, Cdm, Act na wengine nao kila mmoja amesimamisha mgombea haiitaji nabii wala dawa kujua ccm inashinda hata isipotumia kile wanadai dola, maana raia wapinzani lazima waganyike tu.
Uchaguzi ule ACt ilikataa kuungana
Mwaka huu CDM imekataa kuungana, je kuna haja ya kutoamini Ccm inachukua?
Nadhani wanakataa kwa kile wao wanakijua ambacho ni maslahi ya ccm. Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema musiungane na act wazalendo Kuna mammluki za ccm zimo humo mtapotea shauri zetu hivi mbona haha sema sababu ya ccm kusurvise pamoja nakwamba haina sifa ya kuwa madarakani
 
ccm nayo itakufa lini ? , maana naona falsafa ya ukuaji ime base kwa wapinzani au yenyewe haikui ?. maana naona kifo chao kitaletwa na Mungu , untouchable
 
Kwanza tuelewane jambo moja, kwa Tanzania yetu hii muungano wa vyama unaruhusiwa? je, unatambulika kisheria? na kama wakiungana msajili wa CCM atawaruhusu? au ndio mnataka avifute vyama vyote viwili kwa mamlaka aliyopewa hivi karibuni?! kinyume na hapo tusidanganyane, haitakaa itokee waungane.

Pili, kwa vyama vilivyotangulia na kufa, mfano wa NCCR Mageuzi ya Mrema, kilikuwa strong kwa kiasi gani kuweza kuhimili hila na mbinu chafu dhidi yake (NCCR)? sitaki kuamini kilijifia tu bila sababu, tena nyingi toka nje ( chama tawala).

Hili linathibitishwa na tabia ya CCM kununua wapinzani, kuwatishia maisha, na ikibidi kuwaua kabisa kama hawatataka kujiunga na chama chao ( kwa hili mifano ipo tele).

Mwisho niseme tu, uwepo wa chama chochote cha upinzani Tanzania unategemea kwanza na uongozi imara wa chama husika( usioyumbishwa na kesi za kutunga, kuwekwa mahabusu, kuharibiwa mali, na mengine).

Pili, kuzijua mbinu chafu za chama tawala na kufahamu namna ya kuzishinda ili kisife, ( CDM wamethibitisha hili na wanaendelea kulithibitisha).

Tatu, uwepo mtindo wa kuwaandaa viongozi wenye mvuto kwa jamii ili waweze kuongoza chama mbele ya safari, mf. kwa CDM, uwepo wa watu kama Lissu, Mnyika, Bulaya, Mdee na wengine, hii kwangu ni hazina kwa chama husika, hivyo sababu alizozitoa huyo Prof wa US ni za zamani, hayajui mazingira ya sasa ya siasa za upinzani Tanzania.

Lastly kabisa, naona siku hizi imeshazoeleka kwa baadhi ya watu CCM lazima kishinde kila uchaguzi unaofanyika Tanzania, wengi wameshachoka kukumbuka kama CCM huwa kinashinda kihalali au lah, wameshachoka akili, hawaoni mbele tena, wamezoea rafu za CCM, hawakumbuki madhila wanayofanyiwa wapinzani wakati wa chaguzi mbalimbali, wao wameamua tu kuacha kufikiri na kusema CCM lazima ishinde, ajabu sana!

Sasa niwaulize mnaoamini CCM lazima ishinde kama hao wawili hawataungana, je, wakiungana halafu yakabaki mazingira tuliyonayo sasa ( tume ya uchaguzi ya CCM,polisi wa maji ya kuwasha wa CCM) huo muungano wao utasaidia nini?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom