Bright Smart
JF-Expert Member
- May 4, 2011
- 644
- 311
Awataje yeye maana wote wanafahamiana atakua karahisisha mambo
Mama anataka wale waliomtaja ndio wawataje na waleeeeYeye atusaidie kuwataja kama anawajua, sasa hivi si hayuko kwenye baraza.
Jinamizi la kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bado linamsumbua mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka baada ya kuliibua kwenye semina ya mapambano dhidi ya ufisadi, akichongea wabunge ambao hawajaguswa.
Profesa Tibaijuka alipoteza uwaziri wa nyumba, ardhi na makazi kwenye sakata hilo baada ya kubainika kuwa aliingiziwa fedha zinazoonekana zilitoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja na Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Profesa Tibaijuka alikuwa mmoja kati ya viongozi wa ngazi ya waziri, mbunge, jaji na viongozi wa dini walioingiziwa fedha ambazo zinatokana na Sh306 bilioni zilizochotwa kwenye akaunti hiyo.
Akichangia katika semina hiyo inayolenga kuwajengea wabunge uwezo wa kupambana na ufisadi na ambayo iliandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi (ACFE), Profesa Tibaijuka alisema wakazi wa jimbo lake walimchagua kwa mara nyingine licha ya tuhuma za Escrow kwa sababu hawakuziamini.
Alisema fedha hizo za Escrow zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwenda benki ya Stanbic na Mkombozi, lakini cha ajabu majina ya watu waliopewa fedha kupitia benki moja yalitolewa na yale ya benki nyingine yalifichwa.
Alisema inakuwaje yeye anakuwa katika tuhuma, wakati aliyempa fedha hizo hatuhumiwi.
Watu waliotajwa kwenye sakata hilo ni wale waliopewa fedha zilizopitia benki ya Mkombozi, lakini hadi sasa wale waliopewa fedha zinazodaiwa kuwa ni taslimu kutoka Stanbic hawajatajwa.
Alisema sheria pekee yake haiwezi kufanya lolote katika mapambano dhidi ya ufisadi na hakubaliani na wabunge wanaosema kuwa hata kama mahakama imeshindwa kuthibitisha ufisadi, watuhumiwa wataifishwe mali zao.
“Sisi wabunge hatukuja kufanya kazi hiyo, tumekuja kutunga sheria ili zisaidie katika kutuongoza,” alisema.
“Ni vyema kuzungumzia unyofu wa watu kwa kuanzia katika shule, makanisa, misikiti na wabunge.”
Aliituhumu Takukuru kuwa inakubali kutumiwa kwa kuchagua kesi za kuchunguza.“Tume ya Maadili ndio usiseme,” alisema.
“Mie nimeshawahi kushtakiwa Tume ya Maadili, najua kuwa kuna mbunge mwenzetu hapa alipata fedha za Escrow, lakini kwa sababu hakuwa mzungumzaji ameondoka bungeni wala hakuna mtu anajua kama alipata. Unaona jinsi ambavyo hawa watu hawako makini,”alisema.
Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu alilia na watu aliowaita wazushi kwamba wanawazushia wenzao kuchukua rushwa wakati hakuna ukweli.
Niliona juzi Temeke dereva aliyekamatwa akisafirisha wahamiaji haramu akikiri kosa mbele ya media, lakini akauliza swali la msingi kuwa aliyemkabidhi hao watu (mmiliki wa mzigo) alipandishwa kwenye gari la polisi lakini walivyofikishwa kituoni hakuonekana. Na ikagundulika kwa polisi wamemwachia kabla hajafika hapo.Huyu mama asizungushe watu kwanza alitakiwa aombe radhi kwa Umma kupokea zile fedha kwa njia za kifisadi lakini pia azirejeshe mana hoja hapa ni kwanini yeye alichukua zile fedha??
kwa sababu hata hao aliowataja kwamba hawajachukuliwa hatua hakubadilishi yeye kutokuwa fisadi. Nafkiri Tibaijuka amesahau kwamba yeye alikuwa waziri na waziri ni kiongozi wa juu serikalini na umma.
Serikali na bunge imewogopa yeye atawaweza wapi. Hajitaki?Yeye anawajua majina hayo wengine waliochukulia Stanbic si awataje tu kuliko kulalamika tu.
Mkuu hajakataa kwamba amepewa anakubali kila kitu lakini anachosema mbona waliotajwa ni wale wa Mkombozi Bank tu vipi wale waliochukua Stanbic mbona hawatajwi?Akina nani?Kama tuna nia kweli kwanini tusiwataje wote na tukawa na fare system?
Yeye hana mamlaka kuwataja ila mpaka hapo ametuonesha kuwavyombo vyetu hakuna lolote vina fanya kazi kwa kutumiwa tu hawafati sheria na utaratibu unavyo wataka kusema,haiwezekani watu wachote pesa huko BOT alafu waje kuwababmbikizia watu huku downstream,kibaya zaidi zilizo gawiwa mkombozi tena kwa kufata utaratibu wote ndio wanao sumbuliwa lakin huyu singa singa ambae hata hakulipa kodi na aligawa pesa nyingi sana huko stanbic hasumbuliwi,watanzania kuna maswali mengi sana ya kujiuliza hapa na kuhoji,kwanini kuna kigugumizi ktk orodha ya stanbic???huyu mama ana hoja ya msingi tusibezeAwataje yeye maana wote wanafahamiana atakua karahisisha mambo
Yeye si anawajua?
Atutajie
Sasa ufisadi wake unaingiaje wakati kesha sema toka mwanzo na ukumbuke alikua mtu wa kwanza KUKUBALI hadharani kuwa kweli alipokea mchango na alipewa mchango kwa ajili ya shule,maelezo gani uliyataka??hao wengine hawana maelezo ndio mana mpaka leo wako kimya kwasababu hawakua na sababu ya kupokea izo pesa,maelezo ya kutoa hakunaHuyu mama asizungushe watu kwanza alitakiwa aombe radhi kwa Umma kupokea zile fedha kwa njia za kifisadi lakini pia azirejeshe mana hoja hapa ni kwanini yeye alichukua zile fedha??
kwa sababu hata hao aliowataja kwamba hawajachukuliwa hatua hakubadilishi yeye kutokuwa fisadi. Nafkiri Tibaijuka amesahau kwamba yeye alikuwa waziri na waziri ni kiongozi wa juu serikalini na umma.
Basi na yeye angeenda kuchukulia stanbicYeye hana mamlaka kuwataja ila mpaka hapo ametuonesha kuwavyombo vyetu hakuna lolote vina fanya kazi kwa kutumiwa tu hawafati sheria na utaratibu unavyo wataka kusema,haiwezekani watu wachote pesa huko BOT alafu waje kuwababmbikizia watu huku downstream,kibaya zaidi zilizo gawiwa mkombozi tena kwa kufata utaratibu wote ndio wanao sumbuliwa lakin huyu singa singa ambae hata hakulipa kodi na aligawa pesa nyingi sana huko stanbic hasumbuliwi,watanzania kuna maswali mengi sana ya kujiuliza hapa na kuhoji,kwanini kuna kigugumizi ktk orodha ya stanbic???huyu mama ana hoja ya msingi tusibeze
pesa zilizopitia mkombozi bank zilikuwa mgao wa yule mzee wa kihaya,aliyetoa plot yake kusimika mitambo ya umeme,lilikuwa gawio la mbia katika mradi huo,na huyo mzee sijui alitembelewa na roho mtakatifu ama alikuwa hajawahi kushika pesa nyingi kwa ghafla,akaanza kuzigawa kwa ndugu,jamaa,marafiki na maaskofu,Labda za stanbic hazikuwa za escrow ndiyo maana hawakutangazwa
Kabisa kama anaweza akawakilishe hoja Bungeni na kuomba ufafanuziBasi she should shut up and and keep quiet