Prof. Tibaijuka: Watu waliochota fedha za escrow kutoka Stanbic hawatajwi, sisi tulionewa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,495
Jinamizi la kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bado linamsumbua mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka baada ya kuliibua kwenye semina ya mapambano dhidi ya ufisadi, akichongea wabunge ambao hawajaguswa.

Profesa Tibaijuka alipoteza uwaziri wa nyumba, ardhi na makazi kwenye sakata hilo baada ya kubainika kuwa aliingiziwa fedha zinazoonekana zilitoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja na TANESCO na kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Profesa Tibaijuka alikuwa mmoja kati ya viongozi wa ngazi ya waziri, mbunge, jaji na viongozi wa dini walioingiziwa fedha ambazo zinatokana na Sh306 bilioni zilizochotwa kwenye akaunti hiyo.

Akichangia katika semina hiyo inayolenga kuwajengea wabunge uwezo wa kupambana na ufisadi na ambayo iliandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi (ACFE), Profesa Tibaijuka alisema wakazi wa jimbo lake walimchagua kwa mara nyingine licha ya tuhuma za Escrow kwa sababu hawakuziamini.

Alisema fedha hizo za Escrow zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwenda benki ya Stanbic na Mkombozi, lakini cha ajabu majina ya watu waliopewa fedha kupitia benki moja yalitolewa na yale ya benki nyingine yalifichwa.
Alisema inakuwaje yeye anakuwa katika tuhuma, wakati aliyempa fedha hizo hatuhumiwi.

Watu waliotajwa kwenye sakata hilo ni wale waliopewa fedha zilizopitia benki ya Mkombozi, lakini hadi sasa wale waliopewa fedha zinazodaiwa kuwa ni taslimu kutoka Stanbic hawajatajwa.
Alisema sheria pekee yake haiwezi kufanya lolote katika mapambano dhidi ya ufisadi na hakubaliani na wabunge wanaosema kuwa hata kama mahakama imeshindwa kuthibitisha ufisadi, watuhumiwa wataifishwe mali zao.

“Sisi wabunge hatukuja kufanya kazi hiyo, tumekuja kutunga sheria ili zisaidie katika kutuongoza,” alisema.

“Ni vyema kuzungumzia unyofu wa watu kwa kuanzia katika shule, makanisa, misikiti na wabunge.”

Aliituhumu Takukuru kuwa inakubali kutumiwa kwa kuchagua kesi za kuchunguza.“Tume ya Maadili ndio usiseme,” alisema.

“Mie nimeshawahi kushtakiwa Tume ya Maadili, najua kuwa kuna mbunge mwenzetu hapa alipata fedha za Escrow, lakini kwa sababu hakuwa mzungumzaji ameondoka bungeni wala hakuna mtu anajua kama alipata. Unaona jinsi ambavyo hawa watu hawako makini,”alisema.

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu alilia na watu aliowaita wazushi kwamba wanawazushia wenzao kuchukua rushwa wakati hakuna ukweli.
 
Huyu Mama hili suala bado linamtesa. Kifupi hajakubali kushindwa. Anachoshindwa kuelewa ni kuwa pesa ile iliingizwa ktk akaunti yake binafsi wakati shule inazo akaunti za benki. Pili ile milioni kumi aliyoulizwa akadai ni pesa ya mboga tu. Haoni kwamba alijichongea? Hela za shule unazitoa kabla haziaingia kwenye akaunti husika?!!

Halafu kuhusu kuchaguliwa tena haimanishi ndo kukubalika na wananchi. Sote ni mashuhuda kuna watu walishinda lakini hawapo bungeni. So hiyo si point ya msingi.
 
Mkuu hajakataa kwamba amepewa anakubali kila kitu lakini anachosema mbona waliotajwa ni wale wa Mkombozi Bank tu vipi wale waliochukua Stanbic mbona hawatajwi?Akina nani?Kama tuna nia kweli kwanini tusiwataje wote na tukawa na fare system?
 
Jinamizi la kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bado linamsumbua mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka baada ya kuliibua kwenye semina ya mapambano dhidi ya ufisadi, akichongea wabunge ambao hawajaguswa.

Profesa Tibaijuka alipoteza uwaziri wa nyumba, ardhi na makazi kwenye sakata hilo baada ya kubainika kuwa aliingiziwa fedha zinazoonekana zilitoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja na Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Profesa Tibaijuka alikuwa mmoja kati ya viongozi wa ngazi ya waziri, mbunge, jaji na viongozi wa dini walioingiziwa fedha ambazo zinatokana na Sh306 bilioni zilizochotwa kwenye akaunti hiyo.

Akichangia katika semina hiyo inayolenga kuwajengea wabunge uwezo wa kupambana na ufisadi na ambayo iliandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi (ACFE), Profesa Tibaijuka alisema wakazi wa jimbo lake walimchagua kwa mara nyingine licha ya tuhuma za Escrow kwa sababu hawakuziamini.

Alisema fedha hizo za Escrow zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwenda benki ya Stanbic na Mkombozi, lakini cha ajabu majina ya watu waliopewa fedha kupitia benki moja yalitolewa na yale ya benki nyingine yalifichwa.

Alisema inakuwaje yeye anakuwa katika tuhuma, wakati aliyempa fedha hizo hatuhumiwi.

Watu waliotajwa kwenye sakata hilo ni wale waliopewa fedha zilizopitia benki ya Mkombozi, lakini hadi sasa wale waliopewa fedha zinazodaiwa kuwa ni taslimu kutoka Stanbic hawajatajwa.

Alisema sheria pekee yake haiwezi kufanya lolote katika mapambano dhidi ya ufisadi na hakubaliani na wabunge wanaosema kuwa hata kama mahakama imeshindwa kuthibitisha ufisadi, watuhumiwa wataifishwe mali zao.

“Sisi wabunge hatukuja kufanya kazi hiyo, tumekuja kutunga sheria ili zisaidie katika kutuongoza,” alisema.

“Ni vyema kuzungumzia unyofu wa watu kwa kuanzia katika shule, makanisa, misikiti na wabunge.”

Aliituhumu Takukuru kuwa inakubali kutumiwa kwa kuchagua kesi za kuchunguza.“Tume ya Maadili ndio usiseme,” alisema.

“Mie nimeshawahi kushtakiwa Tume ya Maadili, najua kuwa kuna mbunge mwenzetu hapa alipata fedha za Escrow, lakini kwa sababu hakuwa mzungumzaji ameondoka bungeni wala hakuna mtu anajua kama alipata. Unaona jinsi ambavyo hawa watu hawako makini,”alisema.

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu alilia na watu aliowaita wazushi kwamba wanawazushia wenzao kuchukua rushwa wakati hakuna ukweli.
Yeye anawajua majina hayo wengine waliochukulia Stanbic si awataje tu kuliko kulalamika tu.
 
Huyu Mama hili suala bado linamtesa. Kifupi hajakubali kushindwa. Anachoshindwa kuelewa ni kuwa pesa ile iliingizwa ktk akaunti yake binafsi wakati shule inazo akaunti za benki. Pili ile milioni kumi aliyoulizwa akadai ni pesa ya mboga tu. Haoni kwamba alijichongea? Hela za shule unazitoa kabla haziaingia kwenye akaunti husika?!!

Halafu kuhusu kuchaguliwa tena haimanishi ndo kukubalika na wananchi. Sote ni mashuhuda kuna watu walishinda lakini hawapo bungeni. So hiyo si point ya msingi.

hujamwelewa prof wewe,,, rudia kusoma afu ndo uje uchangie upya
 
Sheria ya Tanzania imewafanya baada ya watu kuwa juu yake na wengine chini. Mara nyingi viongozi wanaposema hakuna mtu aliyejuu ya sheria ni kiini macho tu. Wengi hatuongozwi au kuongozwa na sheria bali woga. Bali kama Mungu tungemtanguliza mbele katika maisha yetu haya yasingetokea.
 
Mkuu hajakataa kwamba amepewa anakubali kila kitu lakini anachosema mbona waliotajwa ni wale wa Mkombozi Bank tu vipi wale waliochukua Stanbic mbona hawatajwi?Akina nani?Kama tuna nia kweli kwanini tusiwataje wote na tukawa na fare system?
Yeye atusaidie kuwataja kama anawajua, sasa hivi si hayuko kwenye baraza.
 
Back
Top Bottom