Prof. Tibaijuka ahamishia kibao kwenye 'beacons' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Tibaijuka ahamishia kibao kwenye 'beacons'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 18, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,695
  Trophy Points: 280
  Prof. Tibaijuka ahamishia kibao kwenye 'beacons'

  Monday, 17 January 2011 19:30 newsroom  NA NJUMAI NGOTA

  BAADA ya moto kuwashwa kwa wavamizi wa viwanja vya umma (wazi) na waliojitwalia maeneo ya hifadhi ya mikoko, kibao sasa kimehamia kwa watu waliojenga juu ya mawe ya alama za mipaka ya viwanja (beacons).
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameagiza waliojenga juu ya mawe hayo kubomoa kilichojengwa, kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
  Alitoa agizo hilo jana, akieleza kukerwa na baadhi ya watu waliojenga kuta juu ya mawe ya alama na wengine kuziweka ndani ya uzio wa nyumba zao.
  Profesa Anna akizungumza kwa njia ya simu, alisema hivi karibuni alitembelea maeneo ya Mbezi, Dar es Salaam, ambako alikuta sheria za ujenzi zimekiukwa.
  ÒNilipita maeneo ya Mbezi, niliona watu wamejenga uzio na mawe ya alama yakiwa ndani. Maeneo hayo yamepimwa kama ilivyo Sinza, mawe yanatakiwa yawe nje ya ukuta,Ó alisema.
  Alisema atatuma watendaji kufanya ukaguzi katika maeneo hayo, akionya kuwa, wasiofuata taratibu za ujenzi watavunjiwa.
  Profesa Anna alisema sheria inatoa adhabu kwa kosa la aina hiyo, ambayo ni kifungo cha miaka sita jela. Alisema kila mtu akitaka eneo lake liwe kubwa, wataziba hata njia za watu kupita.
  Kwa mujibu wa Profesa Anna, anachofanya hivi sasa ni kutoa elimu kwa wananchi ili watambue umuhimu wa makazi na kufahamu sheria na kwamba, serikali haimkomoi mtu.
  Desemba 14, mwaka jana, Profesa Anna aliamuru kuvunjwa kuta na jengo lililokuwa jirani na hoteli ya Palm Beach na lingine lililokuwa eneo la Ocean Road, kutokana na kujengwa kinyume cha sheria.
  Kuta hizo na majengo yaliyokuwa ndani yalivunjwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
  Profesa Anna Desemba 30, mwaka jana, aliagiza wananchi waliojitwalia na kujimilikisha maeneo ya hifadhi ya mikoko, kubomoa nyumba zao la sivyo bomoabomoa itawakumba.
  Wizara hiyo hivi karibuni ilifuta viwanja batili 44 viliyopo kwenye hifadhi ya mikoko, eneo la Jangwani Beach na kuwaagiza waliojimilikisha kubomoa majengo yao.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,695
  Trophy Points: 280
  Kaza uzi dada'angu..........................tuondolee udhalimu kwenye jamii yetu.............................
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  wapi wewe huyo mama hamna kitu anarukaruka tu la viwanja vya wazi hajamaliza karukia kitu kingine mikoani tatizo la viwanja vya wazi liko palepale mbali na beacon kuna matatizo ya msingi kama hili la Arusha vijijini wananchi wamelipia hela za kuomba viwanja na badala yake wametumia hyo hela kuwapimia vigogo viwanja yeye katoa kipaumbele kwa beacon priorities ni zipi? Jaman mi namuona yeye ni ka wale tu 'NDEGE WA RANGI MOJA HURUKA PAMOJA' so mi simfagilii wala nini hamna tija katika hilo
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  chapa ilale mama
   
 5. Ngoreme

  Ngoreme Senior Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  mbona open space bado nyingi zimeingiliwa hasa ile ya pale ddc keko karibu na backery jamaa amejenga petrol station (filling station) sasa na nilisha tuma ripoti anza kazi mama
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Ndo aina ya watendaji tunaowahitaji...kaza uzi mama...tunathamini contribution yako tokea UN-HABITAT
   
 7. U

  Uswe JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  i wish we ndo ungekua rais
   
 8. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  mh!sasa huu ni unoko usio kuwa na faida kwa jamii,kwanza akamilishe zoezi la open spaces,kwani nyingi zimevamiwa,then asimamie kuendelezwa kwa open spaces,kwani hizi spaces ni useless spaces kwa sasa hazina maua,wala mabench ya kupumzikia,miti ya kivuli etc
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nadhani asiishie kwenye maneno matendo zaidi. Yale ya ukuta alotaka kuubomoa yamefika wapi?
   
 10. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni huyu mama na Magufuli tu wengine wooote mazoba.
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Rais wako anapenda?
   
 12. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wewe unaonekana ni muhindi unachuki, nenda kwenu india nyie ndo mnaotuharibia nchi na kuongeza rushwa, kwenda
   
 13. father

  father Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kujenga juu ya beacon au kufungia beacon ndani ya fensi yako ni tatizo linalohusiana na open space. Ila hii ni open space ndogo kwa ajili ya watu kupita
   
Loading...