Mtamuua mama wa watu, si akapumzike amalizie hela ya mboga!!!
mboga kama hizi hapa akimaliza ndio aje kugombea tena
Kosa la kwanza kabisa alilolifanya huyu mama yetu mpendwa ilikuwa ni kukubali kugombea ubunge na then uwaziri kupitia ccm, japo anaweza akawa amegain material benefits lakini naamini hazitakaa daima zilingane na heshima yake aliyokuwa kaitengeneza.
Kosa la pili ni pale aliposhauriwa vibaya (japo naamini kwa uelewa wake haitaji hata washauri mbuzi) baada ya kutuhumiwa kupokea pesa kinyume na maadili ya kazi akang'ang'ania uwaziri badala ya kujiuzuru. Cha kusikitisha hapa aliyemshauri ndiye aliyemuabisha!
Ingelikuwa busara baada ya kufukuzwa uwaziri bila hata heshima anayostahili angeamua ku quit siasa lakini hakuonekana kufanya hivyo.
Kosa la tatu analofanya sasa ni kwenda kugombea tena ubunge tena kwenye chama kile kile, bora hata angelikuja kama James Lembeli!
Kama wanavyosema kuwa kosa ni kurudia kosa sasa yeye sidhani kama atarudia kosa mara ya tatu alafu asamehewe!
liyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna
Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana
alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi wake
katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka
alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni
kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika
kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika
kuondoka.
Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara
ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika
kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu
ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza
ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
mboga kama hizi hapa akimaliza ndio aje kugombea tena
* Alisema yeye ni ngangari, alidai wana Muleba wanampenda hata baada ya kutoswa uwaziri...ngoja akomae wanaMuleba wazidi kumuabisha....si apumzike ale pension? au anataka kufia jukwaani?
Mbona mimi naisikia vyema? Angalia sehemu ya sauti ya device unayotumia.Kilichomponza mama Tiba ni maneno yake ya kejeli.