Prof. Tibaijuka adhalilishwa mkutano wa kampeni za maoni CCM, Mkutano wavunjika

Magufuli alishawahi kuwaambia wakazi wa Kigamboni kuwa kama hawawezi kulipa nauli mpya ya Pantoni wapige mbizi. Hakika hawa watawala huwa wanatoa kauli za hovyo, zenye kuleta maudhi na machukizo mbele ya jamii lakini wananchi huwa hawachukulii serious hata kidogo;

Rejea kauli kama:
Sh. Bilioni Moja ni VIJISENTI; (Andrew Chenge)
Ni bora wananchi wale nyasi ili ndege ya rais inunuliwe; (Basil Mramba)
CCM itashinda hata kwa goli la mkono; (Nape Nnauye),

Ccm wamelaaniwa
 
Nasubiri kusikia ya chenge, hivi job ñdugai kachukua fomu ama hajachukua?? maana nasikia jimboni kwake kafanya 0
 
Uongo!
Kama huna la kuandika si unabana tu. Unanikumbusha hadithi ya mwizi sugu. Baada ya kukaa muda bila shughuli anajiibia shati lake mwenyewe.

mwaka huu mtanyooka manyang'au mana ukweli unawauma kweli.
 
Uongo ni upi sasa. Kwanza huyu mama alishasema yeye hatafuti kazina wala hana njaa, kama ni hela ya kula anayo. Yeye hagangi njaa na kama watu wa Nshamba wanataka kuwa na kiongozi mganga njaa wamuweke waone atawasaidia vipi. Iweje tena yuko jukwaani anajinadi?


Uongo!
Kama huna la kuandika si unabana tu. Unanikumbusha hadithi ya mwizi sugu. Baada ya kukaa muda bila shughuli anajiibia shati lake mwenyewe.
 
Yaani mama anaomba msaada wa polisi? Huyo nafikiri ajitoe tu kwenye hicho kinyang'anyiro cha Ubunge.

Tiba
 
Mbona kwenye hiyo video sioni alipodhalilika Prof Tibaijuka! Wahuni wachache wamepewa pombe wakashout mbona umati ulikuwa nyombi na umetulia? Hizi kampeni chafu zitaitumbukiza nchi kwenye machafuko

Sio wote wenye macho huona.
 
Ningekuwepo eneo la tukio tungekuwa tunaongelea habari nyingine kwa sasa huyu Tibaijuka ana madharau sana zile milioni 10 alienda kununua mboga hazamjatosha anataka ubunge tena?
 
Back
Top Bottom