Pole sana Anna. Sisi wengine tunajua wewe ni "iron lady". Siasa ziko rough na endelea kujifunza mbinu za kupambana.
Muleba hawamtaki tena huyo mama ana dharau kama za Masha.
Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba.
Prof Tibaijuka alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni kupitia CCM.
Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika kuondoka.Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo.
Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
siungi mkono tabia ya kuzomea wasomi wetu. najuwa Anna ameponzwa na mfumo wa kiwizi-wizi wa ccm, lakini utu wake na hadhi yake kama professor havipashwi kudharauliwa hata kidogo kwa kisingizio chochote. tuwache siasa za majitaka.
liyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna
Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana
alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi wake
katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka
alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni
kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika
kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika
kuondoka.
Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara
ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika
kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu
ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza
ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
Safi sana waanze kumrushia na mawe sasa kuzomea imetosha.
Inamaana bado anataka kugombea tena ubunge yan atakayempa kura huyu mama nitamshangaa sana
Ako kamama bora mkapige mawe adi kufa.Kajizi sana ako kabibi.
Tatizo kiburi kilimjaa sana utadhani kura alijipigia yeye mwenyewe....apigwe tu
si apumzike ale pension? au anataka kufia jukwaani?
Hvi sio huyu aliyesema haombi ajira wala hana njaa sasa huko anatafuta nini?
Kilicho muharibu nikinywa chake sijui nakabila lake limemponza?anazarau sn
Dawa ya FISADI sio kumshangilia ni kumzomea na kupiga
Asante wana bukoba kwa kutufungulia ukurasa
siungi mkono tabia ya kuzomea wasomi wetu. najuwa Anna ameponzwa na mfumo wa kiwizi-wizi wa ccm, lakini utu wake na hadhi yake kama professor havipashwi kudharauliwa hata kidogo kwa kisingizio chochote. tuwache siasa za majitaka.
Mambo yalipokuwa magumu ikabidiMama wa Mboga aombe askari wa ulinzi kumtoa kwenye mkutano.
Leo Katika hali isiyo ya kawaida,Mkutano wa Wananchi na Watia Nia wa Ubunge Jimbo la Muleba Kusini kwa Tiketi ya CCM umeshindwa kufanyika na kuahairishwa kutokana na Vurugu zilizojitokeza pale aliposimama Mama Anna Tibaijuka Mbunge wa Jimbo La Muleba Kusini maarufu kama "Mama wa Mboga"
Ilivyokuwa;
Watia nia hao wa CCM kwa pamoja wakiwa wameambatana na Prof Anna Tibaijuka,walitoka Wilayani na kwenda moja kwa moja katika Makao Makuu ya Kata ya Nshamba.Pale Nshamba Mjini Ahamuhumula,walienda kujinadi kwa Wananchi wa Nshamba.
Kama kawaida kwenye mkusanyiko wa Wananchi kunakuwa na Watu wa vyama tofauti.
Ndipo wakati watia nia wakiongea,ikafika zamu ya Mama wa Mboga,Mama Anna Tibaijuka kuongea na Wananchi wa Nshamba.
Kabla hajaanza kumwaga sera,ndipo pembeni pembeni ikaanza kusikika minongono ya watu wakihoji kuwa Mama Aseme aliwaona wapi wakinywa Viroba alivyosema siku akiwa na Kinana?
"Kwanza utwambie ulituona wapi tukinywa viroba?,huyu Mama hana heshima amelewa madaraka" "Na Ccm mkirogwa kumrudisha huyu,Jimbo tunawapa Upinzani hilo mlijue" Walisikika baadhi ya watu wakiongea kwa sauti mkutanoni hapo hali iliyomfanya Prof Anna aanze kuweweseka na kughafirika na kuanza tena kujibu mapigo kwa maneno ya kejeli!
Akatamka kwamba "Watu wa Nshamba hamuwezi kuniyeyusha kama Mshumaa mimi siyo mshumaa,kaeni na ujinga wenu".
Basi hali hiyo ikaleta mtafaruku! Zomea zomea maarufu kwa Kihaya "Okugegeeza" ikaanza kupita kiasi ndipo Mama alipotolewa kwa Ulinzi mkali wa Polisi na Green Guard ili kukwepa "amabare ga abanyansi" na Mama akatokomea,na ndipo Mkutano ulipohairishwa na Mc wa Mkutano huo huku watia nia wengine wakisema wamenyimwa haki yao ya kujinadi! Lakini hatimaye Mkutano umehairishwa mpaka baadae itakapotangazwa tena.
Kilichofurahisha zaidi ni wakati pale Watu wa Nshamba wakipaza sauti kwa mama Tibaijuka walisikika wakiongea Kiswahili safi na kilichonyooka kisicho na Lafudhi ya Kihaya hali hiyo inaonesha sasa Nshamba imekuwa,na imeanza kupiga hatua! Kiswahili safi kabisa!
Credit: Mr Edmund Revelian
Mbunge wa jimbo la Muleba kusini Prof anna Tibaijuka jana july 21,2015 alidhalilishwa na wana CCM katika kata ya Nshamba baada ya yeye na wagombea wenzake kufika eneo hilo kujinadi kabla ya kupigiwa kura hapo august 1,2015.Mwendeshaji wa mkutano alikuwa ni katibu wa CCM wa wilaya kwa kumkaribisha kila mgombea kueleza sera zake.
Chanzo: Bukobanewz