Prof. Shivji, Lipumba Mtikila:Serikali Muuaji wa Prof Juan

Hapa Mtikila ana kesi nyingine nzito. Lakini kwa sababu ni Mtikila itakuja na itapita na ataendelea kupeta
 
Mbona alipokufa shemeji yake Mengi Rais alihudhuria mazishi? jamani hebu tuwe wakweli, kwa mchango aliotoa marehemu kwenye tasnia ya sheria tangu aanze kupractice law hadi anatunikiwa uprofesa haikuwa sawa kwa serikali kutotuma mwakilishi rasmi kwenye mazishi.
Anyway, hata kama serikali haikumthamini kiasi hicho lakini atapata thawabu mbinguni kwa kutimiza wajibu wake hapa duniani, hao serikali nao wataonja tu mauti. Pumzika kwa amani Prof.Jwan Mwaikusa.
 
Watanzania Bwana kila kitu lazima afike Rais.

Kwani hata kama rais angefika angefanya nini cha ziada? au kutaka ujiko tu
 
Mmmmmh waswahili na misiba....kijijini kwetu akifa mtoto wa jirani ka bahati mbaya usihudhurie kwa udhuru basiiiiiii wewe ndiye umeloga! Mwanafalsafa MBITI anasema africa hakuna kifo cha kawaida kila kifo kina sababu..lazima watafutwe wachawi ili kukonga roho za watu na familia za marehemu.!!!!!
serikali iliwakilishwa na Mwandosya au kwa sababu ni mnyakyusa mwenzake ikaonekana amekuja kama rafiki/ndugu/jamaa? baada ya kifo cha mwaikusa kama mkuu wa kaya aliwasoma watu HAPA ndio maana HAKWENDA....MAANA WATU WALIDAI EEH ATAENDA TU KWANI ANAPENDA SHUGHULI HIZO NA ATATOA SALAAM ZA KINAFIKI! hata kama mimi nisingeenda kwenye msiba uliojaaa speculations za aina hii! amekuwa clever kamtuma waziri mnyakyusa !!!! ya nini kufika mahali watu wanakunyooshea kidole bana!
Nadhani kwa mengi alikwenda akijua waombolezaji wana mchukulia kama muombolezaji na sio mtu anae wasanifu...kwa AC pia ilikuwa ngumu watu hawakukielewa kifo chae pia...serikali ilihusishwa! nadhani akifanya busara sana hakuna haja ya kuwatibua zaidi waombolezaji lets them consentreiti na msiba na speculations
mix with yours
 
Mmmh mengine ni aibu kwa kweli! Ndio kusema serikali haijui kula na vipofu au they don't care anymore kitakachofikiriwa na wananchi?!

Ni nadra sana mchawi kuonekana kwenye heshima ya mwisho kwa marehemu ambaye mchawi huyo kashiriki. It goes without swindling a word as speculated by Mtikila.

Mwandosya alijiwakilisha yeye mwenyewe kama close friend wa Jwani, kama Mhadhiri mwenzake wa pale chuoni, kama homeboy wake, kama mfiwa wa mmoja wa watu wa mkoani kwake aliyetukuka (watu wa mbeya wanatambuana sana na wanashirikiana sana kufanya mambo ya nyumbani kwao wakihamasishana kwa maendeleo ya kwao) hata kama hawajuani, wakiwa mbali na kwao ni vigumu kutambua kwamba hawatoki kijiji kimoja. Kumbuka kuondoka kwa Mwaikusa ni kupungua kwa Maprofessa wenye asili ya Mbeya ambao wangetoa mchango tosha wa kitaalam kwa mkoa huo.

Kama angetumwa na serikali, Mwandosya asingelificha hilo. Kusema kwamba sio lazima serikali ihudhurie, hivi wanaosema hivyo hawajui kwamba serikali inawategemea sana wasomi wake waliopo nchini kwa uzalendo wao kupata nguvu ya maamuzi magumu badala ya ushauri kutoka nje ya nchi? Sasa kama walimtumia Jwani, wanataka kusema serikali haijapungukiwa na mtoa maoni kama Horub Othman alivyosemwa sana na serikali kwamba wamepata pengo? Wanataka tuamini kwamba kuna mapengo yasiyo na faida? Au kwa kitendo cha Jwani kusema suala la mgombea binafsi ni haki ya Mtanzania yeyote ndio kitanzi cha Jwani? Hivi kwa kumwondoa Jwani ndio wamefanikiwa kuiondoa hoja hiyo mioyoni mwa watu makini? Kwani Jwani alitaka kuwa mgombea binafsi? Naamini alikuwa anatetea kile alichokiona ndicho kitu sahihi kwa nchi. You can never kill anyone who looks dissimilar to you in the opinions. After all, everyone will die, the tears that goes with Jwani wuill sweep everyone connected to his death, whether openly or otherwise. Waliohusika hawatakaa wakapata amani milele na mauaji holela ya kiasi hicho.

OK tuseme ni majambazi wa kawaida tu, sasa serikali haionyeshi masikitiko ya mauaji ya majambazi kwa raia wake? Kwa nini watu wasiamini kuwa serikali inasimamia aina fulani ya ujambazi na kuwa kinyume na ujambazi ambao unawalenga wao na mali zao? Kama angekuwa jamaa ya viongozi wa serikali lakini sio wafanyakazio wa serikalini, je, serikali isingekwenda kwa wakuu wao kujipendekeza kwamba serikali inaungana na walioathiriwa na mauaji kama hayo? Tatizo la viongozi wa Tanzania ni pale wanapokuwa wabinafsi kupita kiasi hata ikibidi kuridhia roho ya mtu itoke ili maslahi ya watu wa serikalini yaendelee kusimama. Kwasema vizuri Lukuvi japo na yeye ni serikali mmojawao, kwamba wanasiasa wanapalilia uhalifu kwa kushiriki kwa namna mbalimbali katika kuhakikisha uhalifu huo unafanyika bila wanasiasa wenyewe kuonekana wazi.

Ipo siku nao wataishia vibaya. Ni vema kuheshimu uhai wa mwenzako. Madhambi mengine tunayoyafanya hata shetani anatushangaa tukoje na ukaidi wetu. OK kwamba wanataka Tanzania iwe kama Siera Leone, wao watakaa pepo ipi? Tutabanana hapahapa tuendelee kukatana mikono, ujanja kuwahi, hapo klia mtu atakapokuwa mjanja ndio watatambua ubaya wa walipotufikisha, maana na wao watakuwa wanaomboleza sawia.

Tuepuke upuuzi huo, hatujazoea sie.
 
Na mimi nilikua najua kuwa huyu aliwakilisha serikali!..Lakini je alisoma au kusema waraka wowote toka serikalini unaoonyesha kuwa alitumwa kuwakilisha?...Kama hakutamka hivyo, basi alifika mahali hapo kibinafsi....Kama serikali haikuwakilishwa, basi ni jambo la kutia mashaka na la kutisha sana, hasa ukichanganya na kauli za mkuu wa kaya za hapo majuzi!

huyu alijiwalikilisha mwenyewe binafsi kama mmoja wa wala vichwa wa UDSM
msissinnginzie serikali..hii gava nasema gavament hii italaaniwa maisha akika...
sema tuu bwana akitwaa arudishi angekuwa anarudisha tngeona mambo ya aibu
ulale salama prof
 
spchlessss.
god knws.
sa km ni ivo asi ata mtikila akuwa hatarini au mtikila yesu
 
spchlessss.
god knws.

Asante ila na wewe ungetoa mawazo yako kutokana na hili, ukisema spchless haisadii chochote Japa Prof Juan ameishatangulia tungekemea unyama huu ili usurudie tena, WASOMI WETU WAKIUWAWA MTOTO WAKO ATAKUWA NA UWEZO WA KUTUMIA COMPUTER/SIMU kama unavyofanya??
 
Sawa serikali haikuhudhiria mazishi ya prof hilo sawa inawezekana walitingwa tusiwahukumu sana! ila huyo mtikila ni nani mpaka anatoa maneno ya uchochozi kama haya?
 
Back
Top Bottom