Prof. Shivji, Lipumba Mtikila:Serikali Muuaji wa Prof Juan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Shivji, Lipumba Mtikila:Serikali Muuaji wa Prof Juan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kachanchabuseta, Jul 18, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Awali iliripotiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete alitarajiwa kushiriki kwenye mazishi ya Mwaikusa, ambaye amefanya kazi ya uhadhiri mwandamizi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa muda mrefu.

  Kutoonekana kwa viongozi wa serikali kwenye mazishi yake kumeshtua wengi, hasa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani waliofika nyumbani kwa Profesa Mwaikusa kuhudhuria mazishi yake


  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema ameshangazwa kwa hatua ya serikali kushindwa kuhudhuria mazishi ya Profesa Mwaikusa, kwani ameuawa akiwa bado mtumishi wa serikali.

  “Kwanza ukiangalia tukio zima, si rahisi kukwepa kuhudhuria mazishi ya Profesa Mwaikusa, pia alikuwa mfanyakazi wa serikali hadi mauti yalipomfika, iweje sasa hawa wenzetu wa serikali washindwe kuhudhuria shughuli hii muhimu?” alihoji Profesa Lipumba.

  Alisema umakini wa Profesa Mwaikusa katika utendaji kazi enzi za uhai wake, kumesaidia nchi kupiga hatua kwenye mambo mbalimbali, hivyo serikali kushidwa kuhudhuria mazishi yake ni jambo la kushangaza.

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, alisema hakutarajia kutowaona viongozi wa serikali katika mazishi ya msomi huyo, kwani kwa namna moja au nyingine wanahusika na mauaji yake.

  “Hawawezi kuja hapa, yeye ndiye alishiriki katika kesi ya mgombea binafsi, na hawa ndio waliohusika na mauaji yake,” alisema Mchungaji Mtikila bila kufafanua.
  Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji, alisema haijawahi kutokea kwa serikali kushindwa kuleta hata mwakilishi wake kwa msiba wa aina hiyo, hasa ukizingatia kuwa Profesa Mwaikusa alikuwa mfanyakazi wa serikali.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mmmh mengine ni aibu kwa kweli! Ndio kusema serikali haijui kula na vipofu au they don't care anymore kitakachofikiriwa na wananchi?!
   
 3. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Prof. Mwandosya Mark, aliwakilisha sirikali
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  "Baadhi ya viongozi waliokuwapo kwenye mazishi yake ambao imeelezwa walihudhuria kutokana na mahusiano binafsi ni pamoja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na Nimrod Mkono (Musoma Vijijini)."
   
 5. n

  nndondo JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  I still ask the question Robert Marley asked, for how long shall they kill our prophets/people while we stand aside and look? Unless we boot them out of their comfort zone we are dead 'saa ya ukombozi ni sasa' look at what Kagame is doing to his people, see what Mugabe is busy chopping of his peoples hands, Sierra leon people are defined by how long or short the remaining of their arms pits are, wanatupeleka huko na sisi tunachekelewa, wako wapi civil society organizations wakaandaa maandamano, what is JF doing to get the so called great thinkers into action? Thinking alone is not enough with these people they do no care at all!
   
 6. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu?? Na hao waliosema wamekamatwa? ama ni janja ya kubadili upepo wa fikra zetu? Inatisha na kusikitisha sana
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Na mimi nilikua najua kuwa huyu aliwakilisha serikali!..Lakini je alisoma au kusema waraka wowote toka serikalini unaoonyesha kuwa alitumwa kuwakilisha?...Kama hakutamka hivyo, basi alifika mahali hapo kibinafsi....Kama serikali haikuwakilishwa, basi ni jambo la kutia mashaka na la kutisha sana, hasa ukichanganya na kauli za mkuu wa kaya za hapo majuzi!
   
 8. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hahaha! we dada mchokozi.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jamani si wamesema serikali iliwakilishwa na Prof mwandosya. Hivi walimu wote wa chuo kikuu wakifariki hata kama ni kwakuuwawa Rais inabidi ahudhurie? This is too much now. Sijui watu wamefanya intellinge analysisi gani kuona kuwa Marehemu kuwa alikuwa Tishio la Uhai wa serikali?

  Hata kama ni hisia tujaribu kuzihoji hisia zetu ili tuwe na ubiased speculation
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Wako bize kujisafisha na ksherekea vijisenti walivyokwisha chuma!
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Lakini mimi sioni strong point kwenye hoja zao, la kwamba eti kwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa serikali basi ilitakiwa viongozi wa serikali wahudhurie, hilo halileti maana. Wafanyakazi wangapi wa serikali wanaofariki hata mkuu wa wilaya tu hahudhurii? Sioni pointi ya msingi ya kuhudhuria kwa serikali katika mazishi hayo. Lakini kutokana na mazingira ya kifo chake, nilitegemea pengine serikali ingetuma japo salamu za rambi rambi. Lakini so far hilo halijafanyika.
  Mimi ninachokifurahia ni kwamba hili soko la pamoja limeanza. Bila shaka litawafundisha watanzania kuwa aggressive na kujifunza kudai na kutetea haki zao kwa nguvu. Kama hivi tunauawa na hakuna hata mmoja anayetoa tamko juu ya hilo, na Rais anaendelea kuhutubia kwamba nchi ina amani ya kutosha na kwamba ujambazi umepungua kwa kiasi kikubwa, na wabunge wanampigia makofi. Natamani siku moja atokee kichaa awagonge malungu hawa wabunge ili wajifunze kuwa aggressive kutetea haki za watanzania. Kwa sababu hawa wabunge ndiyo watunga sheria na ndiyo wenye nafasi nzuri ya kuipush serikali kutekeleza majukumu yake. Hii ua ua inavyoendelea tulitegemea wabunge waseme chochote au waonekane kukerwa na hiyo hali na kubuni mkakati lakini hakuna kitu. Wakifika bungeni ni kusinzia, akishituka ni kupiga makofi hata kama hajui ni nini kilikuwa kinajadiliwa. Natamani kusiwepo na uchaguzi, maana watu tunapigwa na jua kwa kupanga foleni ya kwenda kumchagua mbunge, halafu akiingia bungeni hana lolote. Inaboa, inakera!!
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  jamani serikali itashiriki mamabo mamngapi?..... kama kila msiba mkuu wa kaya atahudhuria ama kutuma mwakilishi, je hatutalalamika mbele ya safari kuwa anatumia muda na kodi zetu kwa shughuli za kawaida??.... na hao waliohudhuria hawatoshi kumpa heshima aliyostahili hadi serikali? hebu tubadilike!!..
   
 13. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Lakini hata hivyo tukiangalia mchango wake katika fani ya sheria na pia mchango wake katika kitivo cha sheria pale UDSM na pia tukio la kifo chake serikali ilipaswa,haswa wizara ya sheria na katiba angalau kutuma ujumbe ili kumuenzi gwiji huyu.
  Labda kutokana na ubize wa maandalizi ya uchaguzi basi wanasahau mambo kama haya
   
 14. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Serikali yetu haijali!!!!!!!!!!! Angekuwa fisadi mwenzao ungeona wanavyomiminika!! Watanzania amkeni, mnalala hata mchana!!!!!!!!!!!!
   
 15. M

  Mutu JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  The guy was no ordinary staff, kweli unasema alikuwa tu kama wafanyakazi wengine wa serikali.
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe katika hilo.
  Na pia haitoshi kuchukulia kigezo hicho cha kutokuhudhulia kwa mwakilishi wa serikali kwenye mazishi basi ndo kifo chake kiwe kimepangwa na serikali. No no no.
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani utaratibu wa mazishi ni jukumu la familia. Tena huyu hakuwa kiongozi wa serikali. Kutopewa nafasi kwa mkuu wa chuo kuongea au , diwani wake kuongea au haiwezi kutia mshaka kiasi hicho. Msiba huo haukuwa mali ya serikali. Wafanyakazi wa UDSM sio wafanyakazi wa serikali pa see maana hata mishahara yao ni tofauti. What if wahusika/familia hawakuona umuhimu wa mwakilishi wa serikali kupewa nafasi ya kuongea? Je diwani/ au balozi wake alipewa nafasi ya kuongea? Siamini kuwa serikali ya Tanzani unahusika. naamini Serikali ina nyenzo na rasimali za kuwashughulia mtu kama marehemu katika njia amabazo sio lazima kuondoa uhai wao. Mnao sema serikali ya tanzania imehusika mnataka tuamini kuwa walishindwa kumtuliza na kumpoteza kama walivyofanya kwa Masumbuko Lamwai . kwangu mimi kuhusika kwa serikali ya Tanzania moja kwa moja na kifo hiki ni 0.0001. hiyo ni kwa sababu serikali ina kila wajibu wa kulinda uhai wa professor , mkulima, mwanafunzi ,mfanyabiashara , etc . Naweza kuweka probability ya mambo ya rwanda kuwa 0.3.
   
 18. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu kama Prof Juan alikuwa na mchango mkubwa katika serikali hasahasa wizara ya katiba na sheria kwanini hawkutuma uwakilishi wao??
   
 19. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii issue ya kusema serikali imehusika na kifo chake, kuna uthibitisho? Kama upo tujuzwe.
   
 20. k

  kirongaya Member

  #20
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli serikali haikutenda haki imeshindwa kutuma mwakilishi hata wa kusoma hutuba ya yaliyojiri mmh
  inaumiza sana kama ni kweli ila sishangai ni matokeo ya tabaka lililopo hapa nchini, nakupa mfano mdogo
  afe mtoto au mke wa mtu maaruf yawezakuwa ni mfanyabiashara mchangiaji mzuri wa chama tawala au
  mwanasiasa atakayebaki ofisini ajipenda mpaka mkuu wa nchi, kwa mtu kama prof marehemu licha ya elimu
  yake na umashuhuri je tukio lenyewe la mauaji tosha kuwa ni ujumbe kwa serikali kukemea na kuwapa
  faraja wafiwa, kumbe tunajifunza hata wewe na mimi kesho likitokea si jambo la kushtua ni utamaduni tu
  kama kama vile nchi haina uongozi tuamke
   
Loading...