Prof. Ndalichako: Wanafunzi UDOM wamerudishwa nyumbani kwa sababu ya mgomo

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Amesema wanafunzi 7802 wamerudishwa nyumbani kwa sababu ya mgomo uliodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja na serikali ilitafuta uvumbuzi wa mgomo huo bia mafanikio.

Walimu ndio waliogoma na sababu kuu ilikuwa ni madai ya fedha na serikali imeona wanafunzi waende nyumbani huku jitihada za kutatua mgomo zikiendelea

 
Nasikitishwa sana na tabia ya watanzania na wanataaluma wa habari kuripoti mambo bila kufika eneo husika au kuonana na wahusika kupata uhakika wa habari wanayotaka kuwajulisha watanzania.Kuna baadhi ya vyombo vinadiriki kuchambua habari na kuijadili katika mlengo potofu na kuwatia shaka na wasiwasi wanafunzi.

Unachotakiwa kutambua nikuwa mpaka sasa wanafunzi hawajaambiwa sababu hasa ya msingi ya kufukuzwa chuoni.Ila yapo mazingira yanayoweza kuwa ndio kiina cha haya yote.

1.Walimu wamekuwa na mgomo tangu semister hii imeanza wakidai malipo yao na stahiki mbalimbali.Kwa maana hiyo wanafunzi hawa wa diploma maalumu hawajasoma zaidi ya lecture 3 na kuna kozi hawakusoma kabisa mpaka wakati huu wiki ya 9 ambayo walitakiwa wawe katika mitihani.Kwahiyo chuo na serekali wameshindwa kuhafikiana namna ya kutatua matatizo ya walimu

2.Lakini mbali na malipo walimu wanadai vitendea kazi ili waweze kutoa elimu bora .mfano vifaa vya maabara,projector,maker pen n.k.Huwezi amini course iliyopangiwa practicle 10 inafanyika moja tu kwa kisingizio kemikali hakuna.Kwa hiyo kuna kukadiriwa alama za practicle kitu ambacho sio sawa.

3.Baada ya kukaa wiki zote hizo ndipo wanafunzi wa diploma waliokuwa wakiishi collage ya social science walipoanza kushawishi maandamano ya kudai kuanza kufundishwa kama haki yao.Kwa uchache kati ya Alhamisi au Ijumaa walianza maandamano kuelekea utawala mkuu bahati mbaya polisi walifanikiwa kuya zuia.

Kinachoonekana hapa mpaka wanafunzi kufukuzwa ni kutaka kuficha yanayowahusu na kuwaachia watanzania waropoke yao ukweli uendelee kupotoshwa.HAKUNA KIONGOZI YOYOTE WASEREKALI WALA CHUO ALIYETAMKA KUWA HAWA WANARUDISHWA KWAKUKOSA SIFA.Isipokuwa chanzo cha yote haya ni mgomo wa walimu wa walimu waliofukuzwa.Kwa muda waliokaa bila kusoma ni mrefu kwahiyo nikama semister imeisha hakuna jipya linaloweza kufanyika.
Kuwafukuza haraka nikuogopa reaction ya wanafunzi baada yakuona inaweza kutokea fujo na sio sifa kama watu wengine wanavyotaka kuudanganya umma.
 
Sasa wabunge kama wanajua ni mgomo wa waalimu kisa pesa kama ni wazalendo wakusanye posho zao za siku moja wakalipwe waalimu watoto waendelee na shule.

Mgomo kushugulikia hatua ya ziada ni kusitisha mafunzo wakati suluhisho linatafutwa.


Watoto wenyewe kumbe hawajafukuzwa kama radio mbao inavyodai.
 
Aisee poleni sana, kwa kuwa suala lenu limefika bungeni nina imani kuwa sasa mtapata suluhisho
 
Sasa wabunge kama wanajua ni mgomo wa waalimu kisa pesa kama ni wazalendo wakusanye posho zao za siku moja wakalipwe waalimu watoto waendelee na shule.

Mgomo kushugulikia hatua ya ziada ni kusitisha mafunzo.


Kumbe hawajafukuzwa kama radio mbao inavyodai
wanafunzi wamefukuzwa tena walipewa masaa machache wawe wameondoka chuoni chini ya uloinzi mkali.
 
Sasa wabunge kama wanajua ni mgomo wa waalimu kisa pesa kama ni wazalendo wakusanye posho zao za siku moja wakalipwe waalimu watoto waendelee na shule.

Mgomo kushugulikia hatua ya ziada ni kusitisha mafunzo.


Kumbe hawajafukuzwa kama radio mbao inavyodai
Ni kazi ya serikali kulipa waalimu,kodi zinaenda wapi?
 
Kushindwa kwa Ndalichako ni aibu kwa Jf tulimpigania sana humu ila kitendo cha mitihani kuvuja na hili linapunguzia sifa huyu mama.
chuki chuki chuki tena binafsi au za kupikwa

na kati ya waliompigania we haumo
 
Back
Top Bottom