Prof. Ndalichako, kiatu kishampwaya!

Prof. Ndalichako, kiatu kishampwaya!

Kaveli

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
5,458
Reaction score
8,961
Siku anateuliwa kuongoza Wizara ya elimu (wizara ambayo ndiyo 'backbone' ya ustawi wa Taifa), nilifurahi sana. Nikajisemea moyoni kwamba sasa gari limepata 'suka' na safari itakuwa salama.

Safari ikaanza suka akiwa imara. Lakini kadri safari ilivyoendelea, nikagundua kuwa kumbe suka wetu ni 'deiwaka' tu, na sio 'profesheno' !

Akaanza ubabaishaji. Siku akalala akaota GPA ya 3.5... na kweli kesho yake tu rukwili ikapitishwa GPA ya 3.5! Nikajisemea moyoni... ohooo sasa suka kaanza kuacha reli, ngoja ni-fasten my belt kabisa mapema.

Haijaisha week, akalala akaota GPA ya 3.0... na kweli kesho yake tu rukwili GPA ya 3.0 ikapitishwa! Nikasema "toba, suka kaanza kupiga ramli kwenye safari yetu?!!"

Yote tisa.... kumi kwenye mikopo ya chuo! Hapa sasa ndiyo nimeconclude kuwa kumbe Wizara ya Elimu bado haina suka, bali deiwaka tu!

75% kukosa mkopo hii ni ajabu ya mwaka!

Mtoto wa maskini kapanda ngorika kutoka sitimbi kijijini kaja mjini kusoma chuo, eti anapewa mkopo wa Tsh. 77,000 ajikimu chuoni! Seriously kabisa Officer mzima yupo Heslb kwenye kiti cha kuzunguka ana-approve Tsh 77,000 kwa ajili ya mkopo wa mwanafunzi wa chuo??!! Hizi ni dharau kwakweli. Otherwise naanza kuamini ule utafiti kwamba nchi hii wengi wana matatizo ya akili. Heslb wanastahili wachapwe bakora nyingi sana kama mvua!

Tanzania inahitaji overhaul ya hali ya juu sana. La sivyo, dharau hizi za viongozi zitazidi kuwafanya wananchi waishi kama mashetani kweli.

Mama Ndali, absolutely sasa kiatu kinakupwaya! Ubabaishaji kwenye elimu ya nchi, Taifa mnaliweka bondi.

Mhe. Rais Magufuli anahitaji kuona Tanzania ya viwanda. Ni jambo jema sana. Ili kuifikia Tanzania ya viwanda, basi tuacheni siasa na ubabaishaji kwenye sekta ya Elimu.

-Kaveli-
 
Tatizo siyo mvaaji. Tatizo ni mnunuzi wa hicho kiatu. Wewe unavaa kiatu namba 8 sasa unalazimishwa uvae namba 12. Una mawazo mazuri sana ya kukifanya kiatu chako kipungue angalau kifikie namba tisa hivi lakini aliyekununulia hataki ukiguse kwa sababu hajaribiwi na hataki kusikia mawazo yako. Basi unajikaza tu na kushindilia matambara ili uendelee kukivaa na kumridhisha aliyekununulia. Vinginevyo ukiona matambara yana-disfigure vidole vyako na kukufanya utembee kwa shida kama mkoma kiasi cha kuchekwa na jamii basi kirudishe kiatu hicho kwa mwenyewe au kibadilishe namba kutoka 12 unayolazimishwa kuivaa mpaka 8 unayoipendelea bila ruhusa liwalo na liwe!

Wavaaji wa viatu hivi safari hii mtawaonea tu lakini kusema kweli aliyewanunulia wanamwogopa mno na wengi wamevivaa kwa woga na japo wanaumia vidole na miguu wengi wanajikaza tu hivyo hivyo. Safari ni lazima iendelee ati!
 
Mkuu, umenena kuntu. Kumbe tatizo sio suka, bali ni 'mwenye gari' !

Mtukufu anaogopwa, hashauriki, na hajaribiwi!

Basi wacha tukalime mihogo Mkuu. Hii safari ngumu!

-Kaveli-
 
Huyu Mama mnamuonea bure tu! Nitajieni Waziri mmoja tu ambaye mpaka sasa ana maamuzi ndani ya hii govt ya Tembo, hamwakumbuki kina Kigwa'la, Nchemba, nk jinsi walivyoanza kwa kasi? Umeshawasikia tena? Mwacheni mama wa watu, tembo ndio muamuzi wa kila kitu kwenye awamu hii, he's Alfa & Omega! Ukitaka kujitutumua kwake kitakachokupata muulize aliyekuwa katibu mkuu Wizara ya fedha (Likwilile).
 
Basi anabugi sana. He won't excel.

Regime ya 'One man show'

-Kaveli-
 
Tatizo wanatawala badala ya kuongoza. Na kama ulivyosema... kuongoza ni karama.

-Kaveli-
Sio kila kiongozi anaweza uongozi
JK na wafanyakazi HEWA alitoa mikopo kwa viana wetu karibia wote
JK na kudhihakiwa na utawala huu lkn chanjo Muhimbili tulipata bure
Hawa ni kujisifu tu lkn hamna huduma yyt iliyo imarika
Ifikie hatua wapunguze porojo
Tunacho kiona ni kufukuzwa watu kazi tu lkn huduma za jamii afadhali na JK
 
Aliyemteua anaamini kama waaminivyo Waafrika wengi kuwa anayeitwa "Professor" au "Doctor" ndiye mwenye akili na uwezo wa hali ya juu wa kufanya mambo.
Nadhani hali halisi inajieleza.
Yuko professor mwingine waziri wa utalii bure kabisa.
 
Toka maraika achukue usukani elimu ya nchi yetu inarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Kipaumbele cha maraika ni ujinga kwa wengi.
 
Hapo kwenye GPA 3.0 si mmepewa takwimu juzi tuu kwamba kila wa watatu wanne ana hewa kichwani. Sasa watatowa wapi wakufikia GPA 3.5?
 
Sio kila kiongozi anaweza uongozi
JK na wafanyakazi HEWA alitoa mikopo kwa viana wetu karibia wote
JK na kudhihakiwa na utawala huu lkn chanjo Muhimbili tulipata bure
Hawa ni kujisifu tu lkn hamna huduma yyt iliyo imarika
Ifikie hatua wapunguze porojo
Tunacho kiona ni kufukuzwa watu kazi tu lkn huduma za jamii afadhali na JK

Tunarudi zama za 'kufunga mkanda'

-Kaveli-
 
Aliyemteua anaamini kama waaminivyo Waafrika wengi kuwa anayeitwa "Professor" au "Doctor" ndiye mwenye akili na uwezo wa hali ya juu wa kufanya mambo.
Nadhani hali halisi inajieleza.
Yuko professor mwingine waziri wa utalii bure kabisa.

Hahahaa yule professor ndo huwa simuelewi kabisa.

-Kaveli-
 
Toka maraika achukue usukani elimu ya nchi yetu inarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Kipaumbele cha maraika ni ujinga kwa wengi.

Malaika anataka wananchi wapumulie pua moja!

Kwakweli Elimu ya nchi hii inachezwa danadana vibaya sana.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom