Siku anateuliwa kuongoza Wizara ya elimu (wizara ambayo ndiyo 'backbone' ya ustawi wa Taifa), nilifurahi sana. Nikajisemea moyoni kwamba sasa gari limepata 'suka' na safari itakuwa salama.
Safari ikaanza suka akiwa imara. Lakini kadri safari ilivyoendelea, nikagundua kuwa kumbe suka wetu ni 'deiwaka' tu, na sio 'profesheno' !
Akaanza ubabaishaji. Siku akalala akaota GPA ya 3.5... na kweli kesho yake tu rukwili ikapitishwa GPA ya 3.5! Nikajisemea moyoni... ohooo sasa suka kaanza kuacha reli, ngoja ni-fasten my belt kabisa mapema.
Haijaisha week, akalala akaota GPA ya 3.0... na kweli kesho yake tu rukwili GPA ya 3.0 ikapitishwa! Nikasema "toba, suka kaanza kupiga ramli kwenye safari yetu?!!"
Yote tisa.... kumi kwenye mikopo ya chuo! Hapa sasa ndiyo nimeconclude kuwa kumbe Wizara ya Elimu bado haina suka, bali deiwaka tu!
75% kukosa mkopo hii ni ajabu ya mwaka!
Mtoto wa maskini kapanda ngorika kutoka sitimbi kijijini kaja mjini kusoma chuo, eti anapewa mkopo wa Tsh. 77,000 ajikimu chuoni! Seriously kabisa Officer mzima yupo Heslb kwenye kiti cha kuzunguka ana-approve Tsh 77,000 kwa ajili ya mkopo wa mwanafunzi wa chuo??!! Hizi ni dharau kwakweli. Otherwise naanza kuamini ule utafiti kwamba nchi hii wengi wana matatizo ya akili. Heslb wanastahili wachapwe bakora nyingi sana kama mvua!
Tanzania inahitaji overhaul ya hali ya juu sana. La sivyo, dharau hizi za viongozi zitazidi kuwafanya wananchi waishi kama mashetani kweli.
Mama Ndali, absolutely sasa kiatu kinakupwaya! Ubabaishaji kwenye elimu ya nchi, Taifa mnaliweka bondi.
Mhe. Rais Magufuli anahitaji kuona Tanzania ya viwanda. Ni jambo jema sana. Ili kuifikia Tanzania ya viwanda, basi tuacheni siasa na ubabaishaji kwenye sekta ya Elimu.
-Kaveli-