PROF Ndalichako kaa na wadau wa elimu meza moja:


B

Biyani

Member
Joined
Aug 7, 2016
Messages
76
Likes
144
Points
40
B

Biyani

Member
Joined Aug 7, 2016
76 144 40
Wazir wa elimu Prof Ndalichako toka ateuliwe kuwa Wazir wa wizara hiyo mwaka mmoja uliopita amekuwa akiongoza wizara hiyo kwa matamko.

Hali hiyo ya kuendelea kutoa matamko kwa waziri Ndalichako imewafanya wadau wengi wa elimu nchini wabaki vinywa wazi.

Miongoni mwa wadau wakubwa waliobaki na mshangao na matamko ya Ndalichako ni Rais mstaafu Ben mkapa.Mkapa akiutubia kule yule UDOM alisikitishwa na hali ya matamko ya wizara,na kuitaka iache matamko na ikae na wadau wa elimu.

Miongoni mwa matamko ya Ndalichako ,ni kufuta kozi za foundation ambazo zilikuwa zinatumika kama daraja kwa wanafunz mbalimbali waliokosa sifa za juu za kujiunga na vyuo vikuu.

Ndalichako anadai kuwa wale walioshindwa kupata maksi za juu ,wasiende kufanya foundation kwenye vyuo Bali warudie mitihani ya form six au form four kwanza.

Swali la muhimu ,ni je Prof Ndalichako haumini mitihani ya vyuo vikuu ya foundation ,bali unaamini mitihani ya baraza la mitihani tu?Je,baraza la mitihani na vyuo vikuu ni kipi chenye hadhi kubwa?

Prof Ndalichako umetoa tamko lingine kuwa vyuo visidahili wanafunzi ,bali wanafunzi wote wadahiliwe na TCU.Je,umewasiliana na Senate za vyuo?Au umetoa tu tamko?TCU ambao wamekuwa wanadahili wanafunzi wamekuwa wakifunga madirisha ya kudahili.Je,kwa vyuo vyenye nafasi kama chuo kikuu huria ,uoni kuwa unavinyima nafasi ya kudahili ?

Naomba Prof Ndalichako ukae na wadau wa elimu ,kuliko kuendelea kutoa matamko unaua elimu ya Tanzania.
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
21,524
Likes
16,322
Points
280
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
21,524 16,322 280
Huyu mbibi namtafutia jina linalomfaa.
 
mafimboo

mafimboo

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Messages
2,418
Likes
775
Points
280
mafimboo

mafimboo

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2014
2,418 775 280
Huyu lazima ashindwe asifikiri hii ni nchi ya babake ,asicheza na bongo,mkapa akishaongea ujue kitu kinakuja,
 

Forum statistics

Threads 1,273,538
Members 490,428
Posts 30,484,489