Prof. Ndalichako apiga marufuku uvaaji wa Majoho kwa wahitimu ngazi za chini

the happiest man

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
253
215
Siku hizi hata mwanafunzi akihitimu chekechea Anavarisha JOHO.....amependekeza yavaliwe pale mwanafunzi wa shahada na si vinginevyo,lengo lake na hawa wengine watamani kufika huko. "Nafikiri haya majoho yangebaki kwa wanaohitimu digrii pekee, ili hawa wengine nao watamani siyo kila mtu anavaa" amesema Prof. Ndalichako

Personally naliunga mkono 100% nini maoni yako.

=========

Ndalichako apiga marufuku matumizi holela ya joho

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amepiga marufuku matumizi ya vazi aina ya ‘Joho’ kwenye sherehe za mahafali ya ngazi za chini za elimu na kutaka litumike kuanzia ngazi ya Shahada ili kulipa heshima vazi hilo.
majoho.JPG

Baadhi ya wahitimu wa elimu ya sekondari katika moja ya shule nchini wakiwa katika vazi aina ya joho

Waziri Ndalichako ameyasema hayo jana jijini Mbeya wakati alipokuwa anawatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa njia ya masafa, iliyotolewa na wakala wa usimamizi na uongozi wa elimu nchini (Adem).

Amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho serikali inafanya jitihada za kuboresha sekta ya elimu ili kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni lazima kutofautisha ngazi za elimu ili mwanafunzi wa ngazi ya chini atamani kufika ngazi ya juu.
NDALICHAKO.jpg

Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako

Amesema kuwa kwa sasa vazi hilo linaonekana kuwa ni la kawaida kwa kuvaliwa na wanafunzi mpaka wa darasa la awali hali ambayo alisema kuwa haitakiwi kuendelea na badala yake livaliwe na wanafunzi wa kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea.

Kwenye sherehe hizo, jumla ya wahitimu 860 wa mafunzo hayo wametunukiwa vyeti na Waziri Ndalichako, ambapo amewataka kutumia taaluma waliyoipata katika mafunzo hayo ili kuinua elimu nchini.

Chanzo: EATV
 
Siku hizi hata mwanafunzi akihitimu chekechea Anavarisha JOHO.....amependekeza yavaliwe pale mwanafunzi wa shahada na si vinginevyo,lengo lake na hawa wengine watamani kufika huko....personally naliunga mkono 100% nini maoni yako
Ni sahihi,hata zamani vazi hili lilikuwa na heshima kutokana na kiwango cha elimu aliyofikia muhitimu wa masomo,lakini sasa hivi hata chekechea wanavaa na madoido kibao.Na hii kisaiolojia inamfanya mtoto mdogo asione umuhimu wa kusoma zaidi elimu ya juu kwa kuvutiwa na heshima ya joho kwa sababu atakuwa ameanza kulitumia angali mdogo.Kwani kitu kikizoeleka sana kinakuwa ni cha mazoea ya kawaida.Waziri yupo sahihi kabisa,ni sawa na vibirth day vinapokuwa vingi mtaani na vikorombwezo vyake tukio hukosa maana.
 
Safi kabisa.Nilikuwa nakereka sana nikiwaona chekechea wamevaa majoho.Frankly ilikuwa ni kudhalilisha elimu.Nilikuwa naona elimu yangu yote ni kama haina maana hivi! Ni sahihi kabisa kwa kweli majoho kuwa reserved for first degree onwards.
Siku hizi hata mwanafunzi akihitimu chekechea Anavarisha JOHO.....amependekeza yavaliwe pale mwanafunzi wa shahada na si vinginevyo,lengo lake na hawa wengine watamani kufika huko....personally naliunga mkono 100% nini maoni yako
 
kuvaa joho au kutovaa hakuna effect yoyote na maendrleo au elimu yako uloipata chuo,kwan shahada kitu gani bwana? tofauti itaonekana tu kam umesoma shahada si jamii ipo inakuangalia so utaweza kutofautishwa vema na hao chekechea.ach watot nao wadgo wapate raha kuvaa ivo au nao waone watafika hyo level wakianza kuvaa now,kam ishu iko ivo mvojadili hapo juu.
 
Katika kile kinachoonekana ni njia ya kuonyesha heshima ya elimu ya kiwango cha degree na kuendelea, Professor Ndalichako amepiga marufuku uvaliwaji wa Majoho kwa wahitimu wa elimu ya awali, msingi, sekondari nk ili kuweka chachu kwa wahitimu hao kufika ngazi za juu zaidi kielimu.

Source: Star TV

My take:
serikali imefanya vyema kwa kuliona hilo, lakini wayaone na mengine mengi yanayodidimiza kiwango na heshima ya elimu nchini ikiwemo kuboresha maslahi ya Walimu na vitendea kazi.
 
Naunga mkono kuvaa majoho ngazi ya chin somtym n kutafta sifa zisizokua na maana na.hiyo nd sabb ckuwai kufany shereh hata moja toka nmeanza shule.mpk leo nmemaliza levo zote za sekondari
 
Awamu Ya Vioja Hii Na Matamko Yasiyo Na Tija Kwa Taifa Kuna Waziri Mwingine Kajipa Majukumu Ya Kila Mara Kaenda Kukamata Gongo
 
Back
Top Bottom