Prof. Ndalichako anafaa kuwa Rais 2025

Prof. Ndalichako anafaa kuwa Rais 2025

sijajua ni akili ipi imetumika hapo kwenye kufikiri rais wa 2025. Sio akili ya kawaida huenda ni ya kiroba
 
Kuwa mbele ya wakimbiaji 600 wa marathon katika mita 400 za mwanzo katika mbio za masafa ya kilometa 21 utasemaje huyo ndiyo anafanya vizuri na ndiye mshindi?

Unakumbuka JK alianzaje na kauli mbiu yake ya kasi mpya, nguvu mpya na maisha bora kwa kila mtanzania, sema mwenyewe hali ilikuaje wakati wa utawala wake.

Ni kweli Ndalichako kaanza vizuri lakini ebu tujipe muda tupime mafanikio yake hasa watoto hawa walioanza darasa la kwanza mwaka huu watafauluje mtihani wa darasa la saba na walioko kidato cha kwanza watafauluje mitihani ya kidato cha nne na cha sita, lazima tuwe na kipimo.
 
Ungetumia lugha hii from the beggining tungeelewana mapema tu, ulichonitisha na ambacho niliendelea kuwa kinyume na wewe ni kuwaita wale waliotoka kuwa ni wezi na ni mafisadi! Nafikiri hata kama mkuu ameamua kuwaweka kando tuheshimu kazi waliyofanya, maana wengine inafahamika kuwa wamewekwa kando kwa sababu tu kwenye halmashauri zao walishinda wapinzani, na si ubadhilifu au wizi kama ulivyokuwa ukionyesha!

Pole sana, lazima uwe na kasi katika
sisi waithilamu hatutampa kura zetu
Kwa thababu anapendelea wathilithitu sio!? Acha hizo bhana, angalia maslahi mapana ya thaifa letu, mama anakwenda vithuli thana!
 
Kwa speed ya huyu Mh. Waziri, umakini na uzalendo anaouonesha katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku katika kuisimamia wizara nyeti ya elimu pamoja na taaluma za wanataaluma wengine, waziri huyu anastahili kuwa Rais 2025. (2020 Rais atabaki huyuhuyu tuliyenae).

Mtaje wa kwako unaemuona anafaa pia bila kujali anatoka chama gani.
Kwenye siasa wiki tu ni nyingi sana
 
Kwa speed ya huyu Mh. Waziri, umakini na uzalendo anaouonesha katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku katika kuisimamia wizara nyeti ya elimu pamoja na taaluma za wanataaluma wengine, waziri huyu anastahili kuwa Rais 2025. (2020 Rais atabaki huyuhuyu tuliyenae).

Mtaje wa kwako unaemuona anafaa pia bila kujali anatoka chama gani.
Mtakuja kujua tu kua huyu mama ni mzigo. Mawazo yake yalishapitwa na wakati sana. Mifumo ambayo anataka kuileta ni very old, wenzetu walishatoka huku. Labda kwa suala la wanafunzi hewa hapo sawa lakini kutaka kubana ufauli bila kuzingatia miundo mbinu iliyopo kwa sasa ni kuwaumiza watoto wa kimaskini sana.
 
Kama ni mwanamama kuwa rais 2025, Prof. Mdalichako comes second to Dr. Tulia. Hawa wameanza vizuri sana na yeyote anafaa iwapo wata maintain tempo hii waliyoanzanayo.
 
Kwa lipi hasa? Watanzania mkisikia watu wanafukuzwa kwa idadi kubwa mnakua na mihemko ya ajabu.
Huyu mama sio mtu smart kiasi hicho, ni wa kawaida tu. Kusema ana~invalidate watu wote ambao wameshagraduate ati kwa kua hawakua na kigezo cha kuingia chuo fulani ni very stupid, the only reason ya kuinvalidate ambayo ningekubaliana nayo ni kama wangekua wamefoji vyeti, ila kama walitumia matokeo yao na bado wakachaguliwa there's absolutely no reason to invalidate them.

Huwezi ukatunga sheria leo ati kuvuta shisha ni kosa kisheria alafu ukamfunga mtu aliyevuta wiki iliyopita, sheria inaanza kutake effect leo, ndivyo dunia inavyokwenda miaka yote. So stupid.

Honestly watanzania nawaonea huruma, kila kitu kikifanyika cha kufukuzisha watu kwenu ni raha, sawa kuna sehemu nyingine wanapatia, ila sehemu nyingine wanakosea, hamna muda wa kureason nyie ni kushangilia tu, umaskini huu hautowaacha miaka nenda rudi, we'll see.
 
Huyu Mama ananikosha sana kwa kweli, nampenda sana huyu mama, Mungu ambariki sana na amjaalie maisha marefu na mafanikio ya baadae...

Kwa type ya huyu mama kufanya kazi na JPM hujutii, hebu assume kama angekuwa waziri wa elimu Enzi za KIKWETE kama angekuwa hivi...
 
Hizi ni mada za kihisia na mihemko tu.
 
Back
Top Bottom