Prof. Mwajabu Possi wa UDSM aula TBC

Namfahamu Prof. Possi kama ni mama mwadilifu na mwenye heshima kwa watu wa rika zote na mchapa kazi sana. Kwa kuzingatia hilo, naamini kwamba atakuwa ni agent mhimu wa mabadiliko ya TBC, maana kwa hivi sasa TBC ni kama shirika la utangazaji la CCM. So ni wakati mzuri wa kulifanya liwe la taifa badala ya kuendelea kuwa la chama.

Ni dada yake Prof. Mlacha wa UDOM
 
Masuala ya Habari hayapo katika mambo ya muungano. Mjumbe namba (viii) Mkurugenzi wa habari idara ya Zanzibar anateuliwaje kuwa kwenye chombo/bodi ambayo haihusiki na mambo ya Muungano?

Mkuu hii ndo Tz..ndo maana Mwinyi ni waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wizara ambayo si ya Muungano
 
Namfahamu Prof. Possi kama ni mama mwadilifu na mwenye heshima kwa watu wa rika zote na mchapa kazi sana. Kwa kuzingatia hilo, naamini kwamba atakuwa ni agent mhimu wa mabadiliko ya TBC, maana kwa hivi sasa TBC ni kama shirika la utangazaji la CCM. So ni wakati mzuri wa kulifanya liwe la taifa badala ya kuendelea kuwa la chama.

Yeye anaweza akawa na mawazo mazuri. Ila hao wajumbe vipi? Mimi siwajui.
 
Kwenye hiyo list ya wajumbe wa bodi, mbona namba (ii) haipo? Wamekosea kuweka namba ama kuna mjumbe wamesahau kumweka? Hii ndio Tanzania.

Labda kulikuwa na jina lillilokuwa limependekezwa awali lakini taarifa za kiintelijinsia zikaonyesha hafai au hakidhi viwango, wamekata!!!! Halafu Tangazo lenyewe halina saini ya msemaji, labda ni first draft, ikija ile final itakuwa imekamilika, tuvute subira!!! Ni hisia tu, sina source!!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
jamani Gachuma wa nini tena hapa, mafisadi wanaotemwa

na wananchi kwao ndo chakula, Gachuma hakubaliki hata kidogo...........wizi mtupu
 
Jamani mnapopata post mkumbuke na washikaji,cheki wajumbe wa hii bodi wangapi wantoka mlimani alipokuwepo waziri! Serikali ya ulaji hii! Du !
 
Jaman profesa amekuwa mwenyekiti wa bodi sio mkurugenzi mtendaji,, yeye anakuwa passive member na sio passive member sawa sawa na kina mboma walivyokuwa tanesco,, so hawez kuibadili tbc kwa chocote zaidi ya mkurugenzi mtendaji wa tbc as ye ndo active member... So yeye sio employee wa tbc... Anakuja kwenye vikao tu, wakat wa recruitment ya director nae anashiriki mchakato wa mzima,,,, so angekuwa managing director wa tbc hapo ndo tungejua uwezo wake

????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
 
Masuala ya Habari hayapo katika mambo ya muungano. Mjumbe namba (viii) Mkurugenzi wa habari idara ya Zanzibar anateuliwaje kuwa kwenye chombo/bodi ambayo haihusiki na mambo ya Muungano?

Nampongeza sana Pro.POSSI, ni mama mbunifu sana na mchapa kazi - Hongera sana. Mama chairperson naona kama kuna kosa la kiufundi limefanyika katika uteuzi wa baadhi ya members i.e Nadhani uteuzi wa Mkurugenzi kutoka Zanzibar si sahihi, habari inahusikana kivipi na Masuala ya muungano, wamu-incorporate katika masuala ya kutoa ushauri kama kuna ulazima lakini not otherwise.
 
And so what? Kwani pale UD kuna maprofesa wangapi ndugu, tena wapo waliooana... inamaana wasipewe vyeo kama wana qualify?... jitahidi na wewe uwe prof upate cha kwako... utaishia kuhesabu ndugu tu...
 
Back
Top Bottom