Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Mheshimiwa Waziri Sospeter Muhongo kwa kipindi ulipokuwa kwenye nafasi hiyo kama Waziri wa Nishati Na Madini Watanzania haswa wanaoishi vijijini watakukumbuka jinsi ulivyotekeleza mradi wa kupeleka umeme vijijini kwa kasi kubwa bila kujali jimbo hilo linawakilishwa na chama kipo, ulifanya kazi yako kwa weledi mkubwa na ulitembea kila kona ya Tanzania kuhakikisha umeme unapatikana kwa bei nafuu,
mimi mwenyewe nakufahamu ulivyokuwa ukichukia UFISADI ulikuwa ni mtu ulikuwa unapenda kufuata utaratibu katika kutekeleza majukumu yako, hukusita kumwambia kiongozi yeyote ukweli inapokuja maslahi ya taifa.
Nakumbuka wakati ulipoamua kugombea nafasi kama kiongozi mkuu wa UNESCO mataifa yote ya Ulaya yalikuunga mkono kutokana na nafasi ya naibu katibu mkuu wa UN ilikuwa ikishikiliwa na mtanzania Dk Asha Rose Migiro ilikuwa vigumu kwa mtanzania mwingine kushika kupewa nafasi ya kuongoza taasisi nyingine ya UN, ikabidi uondoe jina lako pamoja na ulikuwa na sifa zote za kuwa mkuu wa shirika hilo.
Ulipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Rais wa awamu ya nne ulihakikisha umeme wa uhakika unapatikana hapa nchini na ulihakikisha kuwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha unaisha Tanesco. Najua wewe kama Waziri wa Nishati na Madini ilikuwa ni vigumu kuingilia mikataba ya madini iliyokuwa imesainiwa na mawaziri waliokutangulia.
NDUGU Waziri siku zote mwenyezi Mungu huwa anasimama na watu wanaosimamia haki usivunjike moyo kuna siku ukweli utagundulika na Watanzania watahitaji huduma yako.