Prof. Muhongo ateuliwa kuwa Mshauri Mkuu FEMATA

Prof. Muhongo ateuliwa kuwa Mshauri Mkuu FEMATA

Federation of Miners Association of Tanzania (FEMATA) kwa kauli moja wamemteua Prof Sospeter Muhongo kuwa MSHAURI MKUU wao. FEMATA ilifikia uamuzi huo (28.02.2015) kwa kuzingatia elimu, maarifa, uzoefu, uwezo, uadilifu na uzalendo wake.

Prof Muhongo ndiye aliyetengeneza Ramani ya kisasa ya Jiolojia na Madini ya Tanzania (2004) kwa kushirikiana na rafiki zake wa Ufaransa. Tanzania haikutoa malipo ya aina yo yote au kupewa mkopo kutengeneza Ramani hiyo.

Jamani mkumbuke kuwa baba akikomba mboga atamsingizia mtoto hapo kwa muhongo kuna kitu baba anakifahamu
 
Mwizi tu huyu..femata na mewata wote sawa tu
 
Federation of Miners Association of Tanzania (FEMATA) kwa kauli moja wamemteua Prof Sospeter Muhongo kuwa MSHAURI MKUU wao. FEMATA ilifikia uamuzi huo (28.02.2015) kwa kuzingatia elimu, maarifa, uzoefu, uwezo, uadilifu na uzalendo wake.

Prof Muhongo ndiye aliyetengeneza Ramani ya kisasa ya Jiolojia na Madini ya Tanzania (2004) kwa kushirikiana na rafiki zake wa Ufaransa. Tanzania haikutoa malipo ya aina yo yote au kupewa mkopo kutengeneza Ramani hiyo.
hiyo ndio kazi yake , huyo ni mtaalamu wa udongo na miamba huku kwingine alipotea njia , ila waangalie kama kuna akaunti yoyote yenye mgogoro asiione .
 
Ajui tu kwamba, sheria ya utumishi wa umma hairuhusu, atabanwa nayo kama inavyomtokea change sasa.
 
Kama unajua unajua tu na kwa kila kitu Mungu ndo mpaji,hongera sana Prof binafsi naukubali sana uwezo wako na mbele utasonga tu make changamoto na hira in kazi ya Giza na Siku zote nuru haizimwi kamwe
 
ha ha ha hapo ndio nawavulia kofia watanzania wa kati kwa kuwa wafalme wa wapumbavu, hata kama ana dhahabu is the timing okay? hivi ni stakeholder gani serious atafanyakazi na hiyo NGO? na mtashangaa wachimbaji wadogo wenye akili wakijitangazia jimbo na kuanzisha association yao? kwa nini serikali kama kweli inaamnini Muhonog was a bad influence isi block huo upumbavu wa kutumia fedha za escow kununua positions? haya ndio yaliyosababisha traders kujitoa TCCIA na hivyo kukidhoofisha chama kilichoanzishwa na mashujaa wa nchi hii walioona mbali sasa kimebakia kijiwe cha watu kusubiri safari za rais za kwenda nje, wachovu, hawana hata hela ya kujisafirishia, suti zimechakaa, viatu vichafu, mara wengine wamevaa makofia zilipendwa, wakitokea kila mtu anajua wametoka taifa lililochoka watafanyabiashara gani?

Mzee unaoga nje au, mbona hueleweki tulia uandike.uzi utakaosomwa na wanaume
 
usafi wake ni pale alipokubali kuumia lakini asitowe siri za kikwete,wacha aendelee kushuka chart,na kama ni msafi si arudi huko ulaya akafanye kazi za jiolojia yake....

Utasubiri sana hahahahaha Muhongo anaendelea kata mawimbi
 
Duh... Kutoka uwaziri wa nishati na madini hadi ushauri mkuu wa wachimbaji madini, ni bora kwa mfanyabiashara wa juisi na soda kumiliki leseni za uchimbaji gesi.

Hafanyi ushauri kwa njaa anatumia taaluma yake kwa manufaa ya nchi, ikiwemo wapiga debe kama wewe
 
Jambazi ni jambazi hata uwe na digrii 800.ang'olewe tu.hatumtaki akafie mbele

Jambazi wewe na wote mliomuundia zengwe sasa mmeanza kuanguka mmoja baada ya mwingine, anyway saivi mtamtumia nani kuchafua watu, mana mwamba umeanguka
 
na cv ya prof LIPUMBA umeisoma? isome afu nitajie hapa bongo nani mwenye nayo kama ya PRO LIPUMBA?
YAANI kwa ukali wake mpaka CCM wamegoma kuitumia....dadadeki.....

Hiyo cv aitumie akiingia ikulu miaka 2000 ijayo, kwa sasa aitumie kwwnye maandamano
 
Back
Top Bottom