Prof Muhongo asema Mtwara wamekuwa wakitumia umeme wa Kiihansi kwa muda mrefu. Ni kweli?

Wana mtwara kwa kushawishiwa na wanasiasa wameamua kuvuruga amani pasipo na msingi na sababu yoyote. Tujiulize Rais wetu, mawaziri, washauri, wahisani kama IMF, WB nk ambao ni washikadau katika hili suala la gesi ni wajinga na hawajui wananchi wa Mtwara ni moja ya watakao nufaika na huo mradi?

Haingii akilini kabisa kuwa wote hao wanataka kugandamiza wananchi wa Mtwara ila hili suala ni zaidi ya wananchi wa kawaida wanavyofikiria na serikali inajua inafanya nini na Rais Kikwete yeye si mtaalamu wa gesi bali anapewa taarifa na wataalamu, mfano gesi na uzalishaji wake ukiwa Mtwara kuna faida ABC… na ikipelekwa sehemu nyingine ni ABCD hapo wamefikia kuwa gesi iende upande mwingine na si kwa faida ya Rais au waziri bali kwa watanzania wote.

Hoja za watu na wanasiasa uchwara ni kuwa ajira zinatolewa Mtwara gesi ingezalisha umeme hapo, mara umeme utokee Mtwara kutakuwa na ajira, viwanda n.k. Tujiulize gesi ndiyo imepatikana tuna wataalamu wangapi? Kama tukianza ukanda na gesi mtasema ni wanamtwara tu waajiriwe kwenye gesi, mtaanza kuchoma wasio wanamtwara. Elimu ya rasimali kama gesi ni muhimu na hilo ndilo tatizo kubwa Rais Kikwete angeeanza nalo kabla ya kuanza mabishano gesi iwe wapi. Mtwara ni ndogo sana na umeme wanaotaka hata serikali ikiamua kutengeneza power station ndogo ya kuwapa umeme wa gesi inawezekana kwani hata sasa hivi hawapati umeme wa gridi;

Siasa na mambo ya gesi yapuuzwe, kuna wanasiasa wanaoheshimika kwenye vyama pinzani wamekuwa wakisupport ujinga na wengine wametoa hoja za msingi na kuepuka kutoa maoni yao gesi ibaki Mtwara. Hii project ikisimama au kuchelewa kuanza kwa hizi vurugu zisizo na msingi, ndoto ya uchumi kukua na kuondokana na tatizo la umeme itabaki kuwa hadithi. Wataalamu wafanye kazi zao kama waziri wa nishati na madini alivyosema na nchi yetu isonge mbele hata kama kuna uzembe kwenye serikali ya Rais Kikwete lakini hili la gesi wanajitahidi kwa kusaidia watanzania wote. Tukianza kusema gesi ibaki hapa, na huko kwetu Geita tutasema dhahabu iwe processed na kuuzwa Geita.

We kweli unaumwa. Watu wa mtwara wanataka ijengwe kiwanda cha gesi kwao ili vijana wapata ajira na serikali iuze gesi inapotaka. Geita ilipaswa kujengwa kiwanda cha kusafisha madini li vijana wapate ajira, pia tunaweza kuanzaisha soko la kuuza madini Tanzania. Mbona sudan wamejenga kiwanda cha kusafisha madini na watu wanapeleke huko kusafisha madini kabla ya kupelekwa kwenye soko. Wewe ndiyo aina ya hao mawaziri wasiopenda maendeleo ya kusini. Hakuna mtu kusini anataka kuzuia gesi isistoke ila wanataka miundo mbi ijengwe ili vijana wapate ajira. We kwa akili yako ya kitikitimaji unafirikiri mikoa ya Rukwa, kigoma nk. itaendeleaje bila viwanda?.
 
Natamani kusikia kauli ya Mzee wa maamuzi magumu kuhusu ili sakata la GESI.........
 
Huyu Prof. bana kiboko. Kasema Mtwara wana umeme wa grid ya Taifa, duh kazi kweli kweli. Anyway, Watu wa kusini mna sababu ya kudai gesi asilia ilete manufaa kwenu kwanza maana inaonekana hata hao mawaziri hawajui kama mpo. Wamesikia tu gesi basi wamewashwa hadi kunako. Loh

Ngoja nasi tuanze kuadai tanzanite yetu sasa.
 
Gesi ni ya wote

:bowl::bowl:Wana mtwara kwa kushawishiwa na wanasiasa wameamua kuvuruga amani pasipo na msingi na sababu yoyote:nimekataa:nimekataa
 
Vilaza tu, nani mtu wa Mtwara humu atuambie wanachotaka ni nini, nyie wengine make kimya msiwaongelee matatizo yao maana mnatoa points zinapishana ovyo, wao kama ni hospital, barabara na bandari wajengewe sasa, ila kusema gesi ni yao tu huo ni ujinga uliopindukia, ila kama wanachotaka ni kurekebishiwa mambo kama hayo wako very right japo gas ni ya manufaa kwa nchi nzima. Unless mnaanza kuleta mgawanyo wa nchi mwishowe mikoa mingine itafuata na kuanza kugoma umeme usitoke, wengine samaki zisitoke, wengine Cement, tutajikuta tumegawanyika... Wana Mtwara tuambieni mnachotaka ni nini hasa tuache siasa! kama si wa mtwara hata usijibu utakua kimberembere kuongelea usilolijua
 
Gesi ni ya wote

:bowl::bowl:Wana mtwara kwa kushawishiwa na wanasiasa wameamua kuvuruga amani pasipo na msingi na sababu yoyote:nimekataa:nimekataa

Kweli kabisa, hawa wanasiasa wanapotosha watu na watanzania wengi wafata mkumbo bila hata kuumiza kichwa
 
Kama huna cha kiandika kaa kimya utaonekana una akili kuliko kujaza pumba hapa. Wewe ni msemaji wa nani na kwa manufaa ya nani? Know inakuwa siri hata kuweka huo mkataba hadhrrani
 
Wewe na wao nani kilaza mana unaonekana hujui lolote!!! Uliza kistaarabu ufafanuliwe si maneno ya kishenzi shenzi kama hivi!!! Unadhani wana-Mtwara wote hawana akili mpaka walishupalie hili????

Vilaza tu, nani mtu wa Mtwara humu atuambie wanachotaka ni nini, nyie wengine make kimya msiwaongelee matatizo yao maana mnatoa points zinapishana ovyo, wao kama ni hospital, barabara na bandari wajengewe sasa, ila kusema gesi ni yao tu huo ni ujinga uliopindukia, ila kama wanachotaka ni kurekebishiwa mambo kama hayo wako very right japo gas ni ya manufaa kwa nchi nzima. Unless mnaanza kuleta mgawanyo wa nchi mwishowe mikoa mingine itafuata na kuanza kugoma umeme usitoke, wengine samaki zisitoke, wengine Cement, tutajikuta tumegawanyika... Wana Mtwara tuambieni mnachotaka ni nini hasa tuache siasa! kama si wa mtwara hata usijibu utakua kimberembere kuongelea usilolijua
 
attachment.php

Moja ya bango katika maandamano ya Mtwara

nchi haikuwa na pesa. subirini ifike b'moyo pesa itapatikana na mtapata mnachotaka.
 
Pesa ipi unazungumzia Mkuu!? Unasikia misamaha ya kodi kwa mwaka ni sh trillion tatu, hujaweka ufisadi na wizi unaofanywa na makampuni ya uchimbaji wa madini miaka nenda miaka rudi.

nchi haikuwa na pesa. subirini ifike b'moyo pesa itapatikana na mtapata mnachotaka.
 
Back
Top Bottom