Prof Muhongo asema Mtwara wamekuwa wakitumia umeme wa Kiihansi kwa muda mrefu. Ni kweli?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,020
Muhongo on Mtwara deomostrators: You stand condemned

By Florian Kaijage
29th December 2012

The Minister for Energy and Minerals, Prof. Sospeter Muhongo has said that people who held demonstrations in Mtwara against government plans to extract natural gas “deserve condemnation” because they contravened the national economic ethic.

In an interview with this paper yesterday, the minister stated that the concept in question -- confining the natural gas use and revenue to Southern regions -- was divisive and therefore unacceptable.

“I plead with all my fellow Tanzanians to condemn the demonstrations in Mtwara … because this portrays national division at the highest degree.

Muhongo says the ongoing campaigns on natural gas were detrimental to national unity.

He also said the campaigns which now pit political parties and other social groups should take into account that prior to the start of gas and mineral extractions the country’s economy used to run on expensive resources.

“What would happen if the concept of regionalism were applied to zones and regions which were sources of valuable cash crops such as coffee producing areas of Kagera, Kilimanjaro and Mbeya … or Tanga which was the country’s main sisal producer … or Iringa and its tea?” he queried.

Prof. Muhongo noted that the government would give a detailed statement on Monday (December 31) on the matters related to the gas sub-sector and its benefits to the national economy -- and to the people in the southern zone in particular.

“I will hold a press conference on January 1, 2013 giving details of revenue made from agriculture, minerals and natural gas sectors. We will also show how the Southern people will benefit and how the confirmed natural gas reserves are huge and can not be utilized in Mtwara and Lindi alone”

According to the energy ministry’s records, Tanzania has confirmed natural gas reserves of 33 trillion standard cubic feet, mainly in Southern Zone of Mtwara Lindi regions and in the deep sea of the Indian Ocean.

In the meantime, Opposition spokesperson on Energy and Minerals ministry, John Mnyika (Ubungo- Chadema) said in a press statement yesterday that what happened in Mtwara was a result of government failure to implement National Assembly’s recommendations on the best way of running the gas-subsector

Mnyika also advised President Jakaya Kikwete to talk on the matter in his New Year speech and explain on how Mtwara people will benefit from gas projects.

The legislator added that the nation should be told how the Southern people had gained from natural gas since the start of extraction in 2004.

On Thursday, thousands of Mtwara residents demonstrated from Mtawanya village to Mtwara town through Msimbati road where the natural gas is being extracted. The demonstrations also drew public interest from several districts -- including Tandahimba and Newala districts.

According to coordinators of the demonstration, the Mtwara Regional Commissioner, Mr Joseph Simbakalia, was supposed to be the guest of honour, but he declined the offer and instead the procession was received by the Chairman of Union of political parties, Mr Hussein Mussa Amiri.

The Union is made up of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR-Mageuzi, SAU, TLP, APPT Maendeleo, ADC, UDP and DP. The parties had one motto ‘Gesi kwanza, vyama baadaye, hapa hakitoki kitu’ (literally meaning, gas first political parties later, nothing will be taken away from here).

Some of the placards that were carried by the demonstrators carried messages opposing the government’s move to extract the natural gas and transport it to Dar es Salaam through the pipeline.

They demand government’s clarification on how natural gas will principally benefit Mtwara residents and benefit the nation at large, avoiding a similar experience drawn from mineral sector where precious minerals producing areas such as Geita and Nzega (Gold) have not been given required attention in terms development.

The demonstrators also voiced laud for the need for the state setting up environment which will attract for construction of various industries that would be vital for job creation and improvement of people’s wellbeing through good income.

Reading a joint report prepared by the Union of Political Parities, Mr Seleman Litope said the southern part of the country is often ignored. He cited the removal of a railway line, poor governance of cashew price, poor infrastructure and now the natural gas as some indicators of neglecting the southern area.

Currently the state is undertaking construction of a 532- kilometer long natural gas pipeline from Mnazi Bay, Mtwara and Songosongo Island in Lindi to Dar es Salam under a soft loan amounting to Sh2.2 trillion from Exim Bank of China. The pipeline is projected to be operational in the next 20 months and would be transporting a minimum of 420 million cubic feet of gas a day, enough to generate more that 2000 megawatts.
Government planners say the gas will end the perennial power crisis.

SOURCE: THE GUARDIAN
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUFAFANUA KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI

1.0 UTANGULIZI
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi wa miradi ya Gesi Asilia ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na wawekezaji katika Sekta ndogo ya Gesi Asilia na kueleza manufaa makubwa yatakayopatikana kwa wananchi wote wa Tanzania wakiwemo wale wa Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Siku ya Alhamisi, tarehe 27 Disemba 2012, baadhi ya Vyama vya Siasa vya Upinzani viliratibu na kuhamasisha baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara, wengi wao wakitokea Mtwara Mjini kufanya maandamano ya kudai raslimali ya Gesi Asilia iwanufaishe wakazi wa Mtwara na kupinga mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa Wa-Tanzania wote kwa kupitia vyombo vya habari.

Tokea Uhuru, uchumi wa Tanzania umetegemea kilimo cha mazao ya biashara kama vile katani (Tanga na Morogoro), pamba (Mwanza, Mara na Shinyanga), kahawa (Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma na Mara), chai (Iringa) na tumbaku (Tabora). Fedha za mazao haya zimewanufaisha wakazi wa mikoa yote ya nchi yetu bila ubaguzi wo wote wala wakulima wa kutoka mikoa hiyo hawajawahi kufanya maandamano wakidai upendeleo (dhidi ya Wa-Tanzania wengine) wa aina yo yote ile.

Mapato yatokanayo na uchimbaji wa dhahabu (Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga na Tabora), almasi (Shinyanga) na tanzanite (Manyara) yamewanufaisha Wa-Tanzania wote bila ubaguzi wo wote ule! Minofu ya samaki wa Ziwa Victoria (Mara, Mwanza na Kagera) imeliingizia Taifa letu fedha nyingi ambazo zimetumiwa na wakazi wa nchi nzima bila ubaguzi wo wote.

Aidha kuna mikoa ambayo inazalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa manufaa ya Wa-Tanzania wote. Mahindi kutoka Rukwa, Mbeya, Ruvumana Iringa yanasafirishwa kwenda mikoa yote ya nchi yetu bila kujali eneo yanakolimwa na wakazi wa mikoa hiyo hawajawahi kudai mahindi hayo ni kwa ajili ya watu wa mikoa hiyo pekee. Sukari ya Kilombero, Mtibwa na Kagera inatumiwa na wakazi wa mikoa yetu yote bila ya kuwepo madai ya mikoa inayozalisha sukari hii kupewa upendeleo wa aina yoyote ile. Maji ya Mto Ruvu yanatumiwa na wakazi wa Dar Es Salaam bila manung’uniko yo yote kutoka kwa wakazi wa eneo la chanzo cha Mto Ruvu.

Umeme wa kutoka Mtera, Kidatu na Kihansi (Dodoma na Morogoro), Hale (Tanga), na Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro) unatumiwa na wakazi wote wa Tanzania bila ubaguzi au malalamiko ya wenyeji wa sehemu ambazo umeme huo unafuliwa na kusafirishwa kwenye Gridi ya Taifa.

Kwa hiyo, kutokana na mifano hii michache, ni wajibu wa wazalendo na wapenda maendeleo wa kweli na hasa Wa-Tanzania wanaopinga ubaguzi wa aina yo yote ile kujiuliza kwa kina sababu zilizopelekea Vyama Siasa vya Upinzani kupanga, kuhamasisha, kushabikia na kuongoza maandamano ya tarehe 27 Disemba 2012 pale Mtwara Mjini.



2.0 RASLIMALI YA GESI ASILIA TANZANIA
Gesi Asilia ilianza kugundulika hapa nchini tangu mwaka 1974 kwenye Kisiwa cha Songo Songo, Mkoani Lindi. Baada ya hapo Gesi Asilia imegundulika maeneo ya Mtwara Vijijini, yaani Mnazi Bay (1982) na Ntorya (2012), Mkuranga (Pwani, 2007), Kiliwani (Lindi, 2008). Kiasi cha Gesi Asilia iliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa Futi za Ujazo Trilioni 4.5 – 8. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia uliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari. Kiasi cha Gesi Asilia iliyogundulika katika kina kirefu cha maji inafikia takribani Futi za Ujazo Trilioni 27. Kiasi cha wingi wa Gesi Asilia yote iliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafikia takribani Futi za Ujazo Trilioni 35.

Kufuatana na Sheria za nchi yetu zinazotumiwa kugawa mipaka ya mikoa iliyopo kando kando mwa bahari (isivuke 12 nautical miles au 22.22 km kuingia baharini), Gesi Asilia iliyogunduliwa hadi sasa katika Mkoa wa Mtwara pekee ni asilimia 14 tu ya gesi yote iliyogundulika nchini. Kwa kutumia kigezo hicho cha Sheria za mipaka ya ki-utawala ya mikoa yetu, Lindi inayo 7% ya gesi yote, Pwani 1% na huku Kina Kirefu cha Bahari (Deep Sea) ndicho chenye gesi nyingi (78%) kuliko mikoa yote ikiwekwa pamoja! Kwa hiyo, hakukuwa na haja ya kufanya maandamano kwa sababu Gesi Asilia nyingi inapatikana kwenye bahari ya kina kirefu ambayo iko ndani ya mipaka ya nchi yetu bila kujali mipaka ya mikoa yetu. Isitoshe Gesi Asilia imegundiliwa kwenye miamba tabaka (sedimentary rocks) yenye umri wa Miaka kati ya Milioni 199.6 hadi 23.03. Mipaka ya Bara la Afrika, ya nchi yetu na ile ya mikoa yetu haikuwepo wakati huo!

Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia pia unaendelea tukiwa wa mategemeo makubwa ya upatikanaji wa raslimali hizi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi, Morogoro na Tabora pamoja na kwenye kina kirefu cha maji baharini kuanzia mpaka wetu na Msumbiji hadi mpaka wetu na Kenya. Hatutarajii mikoa hii nayo ifanye maandamano ya kutaka kuhodhi raslimali za Gesi Asilia na Mafuta zitakapogunduliwa mikoani mwao.


3.0 MATUMIZI YA GESI ASILIA YA MNAZI BAY (MTWARA) NA SONGO SONGO (LINDI)

Mpaka hivi sasa Gesi Asilia inayozalishwa na kutumika nchini ni kutoka Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) na Songo Songo (Kilwa, Lindi). Gesi ya Mnazi Bay kwa sasa huzalisha umeme kwa ajili ya Mikoa ya Mtwara na Lindi tu. Mitambo ya kufua umeme kutokana na Gesi Asilia iliyopo Mtwara Mjini inao uwezo wa kuzalisha MW 18 lakini matumizi ya umeme ya Mikoa ya Mtwara na Lindi haijavuka MW 12. Umeme huo wa Mtwara unafuliwa na TANESCO huku Kampuni za Wentworth na Maurel & Prom zikizalisha Gesi Asilia (inayotumiwa na TANESCO) kiasi cha Futi za Ujazo Milioni 2 kwa siku. Ikumbukwe kwamba ufuaji wa umeme wa hapo Mtwara Mjini ulikuwa mikononi mwa Kampuni ya Artumas iliyofilisika. Tangu Desemba 2006 hadi leo hii kiasi cha gesi kilichotumika kufua umeme kwa ajili ya mikoa hiyo miwili ni chini ya asilimia 1 ya gesi yote iliyogundulika Mnazi Bay (Mtwara Vijijini).

Vilevile ikumbukwe kwamba kuna visima vinne vya Gesi Asilia pale Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) na kinachotumika kwa sasa na tena kwa kiwango cha chini kabisa ni kimoja tu!

Aidha ni vizuri ndugu zangu Wa-Tanzania wakaelewa kuwa Gesi Asilia hii inatafutwa na kuchimbwa na wawekezaji wenye mitaji mikubwa, wataalamu na teknolojia ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi Asilia ambao wanapaswa kurejesha mitaji yao. Uchorangaji wa kisima kimoja cha utafutaji wa Gesi Asilia nchi kavu unahitaji Dola za Marekani Milioni 40, na kwenye kina kirefu cha maji baharini zinahitajika zaidi ya Dola za Marekani Milioni 100. Ikumbukwe kwamba, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Mafuta la Tanzania (TPDC), inatumia fedha za walipa kodi wa nchi nzima kwa shughuli za kuvutia, kuratibu na kusimamia utafutaji na uendelezaji wa Gesi Asilia nchini kote ikiwemo Mikoa ya Mtwara na Lindi. Walipa kodi Wa-Tanzania bado hawajalalamika wala hawajafanya maandamano ya kudai fedha zao za kodi zisitumike huko Mtwara!

Ni muhimu pia tukaelewa kwamba Gesi Asilia iliyopo Mnazi Bay (Mtwara Vijijini) inazalisha umeme peke yake kwa ajili ya Mikoa ya Mtwara na Lindi. Gesi Asilia ya Songo Songo (Kilwa, Lindi) ndiyo inayotumika kuzalisha umeme kwa ajili ya Gridi ya Taifa, na pia kwa ajili ya wananchi wa Kisiwa cha Songo Songo (Lindi), maeneo ya Somanga Fungu (Lindi) na viwandani (Dar Es Salaam). Tangu Oktoba 2004 ambapo mitambo ya kufua umeme ilipoanza kazi hadi leo hii, kiasi cha Gesi Asilia ya Songo Songo kilichotumika ni asilimia 7 tu ya Gesi Asilia yote iliyogunduliwa huko. Kwa hiyo, takwimu zinaonyesha kwamba hata uchumi wa Jiji la Dar Es Salaam unatumia kiasi kidogo sana cha Gesi Asilia (7%) iliyopo Songo Songo (Kilwa, Lindi). Ikumbukwe kwamba waajiriwa kwenye viwanda vya Dar Es Salaam wamo wanyeji wa kutoka Mtwara Mjini ambako maandamano yalifanyika na vilevile wamo wafanyakazi ambao ni wanachama wa Vyama vya Siasa vya Upinzani vilivyopanga, ratibu na kushabikia maandamano ya Mtwara Mjini ya tarehe 27 Disemba 2012.


4.0 MIPANGO YA MATUMIZI YA GESI ASILIA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5 HADI 10

(a) Ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia hadi Dar Es Salaam:
Kuuza Gesi Asilia Jijini Dar es Salaam, kitovu cha uchumi wa Tanzania (80% ya mapato ya nchi yetu yanazalishwa Dar Es Salaam) ni uamuzi mzuri wa ki-uchumi. Tayari kuna viwanda 34 vinatumia Gesi Asilia ambavyo vinahitaji kupanua shughuli zao endapo gesi zaidi itapatikana. Soko kubwa la Gesi Asilia lipo tayari Dar es Salaam (na siyo Mtwara), ambapo ipo mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta. Serikali inatumia fedha nyingi za kigeni kununulia mafuta ya kufua umeme tunaoutumia kila siku. Takribani Dola za Marekani Bilioni Moja (sawa na Shilingi Trilioni 1.6) kwa mwaka zitaokolewa kutokana na mitambo iliyopo nchini ikifua umeme kwa kutumia Gesi Asilia na kuachana na mafuta ambayo ni ya bei kubwa sana. Bei ya umeme kwa uniti moja (KWh) ya umeme unaofuliwa kutumia dizeli na mafuta ya aina nyingine ni kati ya Senti za Marekani 30 hadi 45 na huku bei ya uniti moja hiyo hiyo ni Senti za Marekani 6-8 kwa umeme utokanao na Gesi Asilia na zinapungua na wakati wa matumizi.

Vilevile, takribani Dola za Marekani millioni 202 kwa mwaka zitaokolewa iwapo Jiji la Dar Es Salaam litatumia Gesi Asilia badala ya mafuta katika magari, taasisi na majumbani. Fedha hizi zikiokolewa zitatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa letu kwa manufaa ya Wa-Tanzania wote wakiwemo wale waliondamana na wale walioratibu maandamo ya Mtwara Mjini ya tarehe 27 Disemba 2012.

(b) Umeme mwingi zaidi kutokana na Gesi Asilia:
Bomba la Gesi Asilia linalojengwa litasafirisha gesi nyingi zaidi ambayo itawezesha mitambo mipya itakayojengwa Kinyerezi (Dar Es Salaam) kufua umeme wa zaidi ya MW 990. Umeme mwingine utafulia Somanga Fungu (Lindi) wa kiasi kisichopungua MW520.

(c) Usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini mwetu:
Dar es Salaam ndiko kuna miundombinu mikubwa ya usafirishaji na usambazaji wa umeme kuliko mikoa mingine yote, hivyo ni uamuzi wa ki-uchumi unaotulazimisha kusafirisha Gesi Asilia kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara na kuipeleka Dar Es Salaam ambako itatumika kufua umeme, na kutumika moja kwa moja viwandani, majumbani na kwenye magari.

(d) Kwa kuzingatia mahitaji ya Gesi Asilia yatakayojitokeza:
Bomba la kusafirisha gesi litawekewa matoleo ya kuchukulia gesi (tie-off) katika maeneo ya Mtwara, Lindi, Kilwa na Mkuranga ili kuhakikisha kuwa miji hii inakuwa na Gesi Asilia ya uhakika wakati wowote itakapohitajika. Kwa hiyo kuweka mitandao ya usambazaji wa gesi kutoka kwenye Bomba la Gesi Asilia linalojengwa kutarahisisha matumizi ya Gesi Asilia viwandani na majumbani katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, na kwenye mikoa mingine kwa siku za baadae.

(e) Serikali imetenga maeneo katika pwani ya Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) kwa ajili ya uanzishwaji wa maeneo ya viwanda (Industrial Parks/Estates) vikiwemo viwanda vya mbolea, Liquefied Natural Gas (LNG) na Petrochemicals.

Ujenzi wa kiwanja cha sementi uko katika hatua za mwisho za maandalizi.

(f) Ili kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ya Gesi Asilia na Mafuta kwa kampuni za huduma, malighafi na vitendea kazi, Serikali imetenga eneo maalumu Mtwara, ambalo litawekewa miundombinu ya msingi ili kutoa vivutio mbalimbali kwa makampuni hayo. Eneo hilo litapewa hadhi ya Ukanda Huru wa Bandari (Freeport Zone).

Ni lazima shughuli za kusafisha na kusafirisha Gesi Asilia zitatoa ajira katika maeneo husika. Kwa mfano kwa mitambo ya kusafishia gesi inayojengwa Madimba (Mtwara Vijijini) na SongoSongo (Kilwa, Lindi), kila mtambo utahitaji wafanyakazi na wengine watatoka Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Watanzania wanakumbushwa kuwa raslimali zilizopo nchini ikiwemo gesi asilia, madini, makaa ya mawe, wanyama pori, misitu, milima ya utalii, mito, maziwa, bahari n.k ni za Wa-Tanzania wote kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raslimali hizi zinapatikana, zinatunzwa na kuzalishwa maeneo mbalimbali nchini mwetu na mapato yake yanatumika kwa maendeleo ya Wa-Tanzania wote bila kujali maeneo raslimali hizo zilipo.

Tusikubali kuvunja nchi yetu vipande vipade kwa kisingizio cha raslimali zilizopo mikoani mwetu. Tusikubali kuvunjavunja mikoa yetu kwa kisingizio cha raslimali zilipo kwenye wilaya zetu.

Tusikubali kuvunjavunja wilaya zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye tarafa zetu. Tusikubali kuvunjavunja tarafa zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye kata zetu. Tusikubali kuvunjavunja kata zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye vijiji vyetu na mitaa yetu.


MUNGU IBARIKI TANZANIA, DUMISHA UHURU NA UMOJA WETU

Prof Dr Sospeter Muhongo (Mb)
WAZIRI YA NISHATI NA MADINI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
attachment.php

Moja ya bango katika maandamano ya Mtwara
 
Ukimsoma Muhongo hapo juu ndiyo kishapotezea hili swali muhimu sana kwa wenyeji wa Mtwara.

Hili swali ni muhimu sana kujibiwa, na wanatakiwa wawaeleze watu wa Mtwara, hizo barabara zitajengwa lini?
 
He is the one who stands condemned for uttering such comments instead of addressing critical issues that were raised by the demonstrators.
 

Lipumba aunga mkono maandamano Mtwara

na Betty Kangonga
Tanzania Daima


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameunga mkono maandamano ya wakazi wa Mtwara na kusema kuwa wana hoja nzito ya kuchukua uamuzi huo.

Lipumba alitoa kauli hiyo siku moja baada ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara kuandamana kupinga uamuzi wa serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba kutoka mkoani mwao kwenda Dar es Salaam.

Akizungumza na Tanzania Daima, Profesa Lipumba, alisema kuwa wakazi hao wana kila sababu za kuchukua hatua hiyo kwa kuwa hawajatendewa haki katika mipango iliyoandaliwa na serikali.

Profesa Lipumba, alisema kuwa ujenzi wa bomba hilo umefanywa kwa haraka kwa kuwa hakuna mipango madhubuti iliyowekwa ili wakazi hao waweze kufaidika na rasilimali hiyo.

Alisema kuwa serikali ilipaswa kuangalia namna ya kuongeza uzalishaji wa rasilimali hiyo kwa kuunganisha na ile ya Mnazibay pamoja na Songosongo ili iweze kuwanufaisha wakazi wa maeneo hayo na yale ya jirani.

Profesa Lipumba ambaye kitaaluma ni mchumi, alisema kuwa serikali haikupaswa kukimbilia kujenga bomba hilo bali ilipaswa kutekeleza maamuzi ya kujenga kiwanda cha mbolea na kituo cha kufua umeme ambao ungeunganishwa katika gridi ya taifa.

Alisema kuwa hakuna utaratibu uliofanyika hadi sasa wa kutekeleza maagizo hayo zaidi ya serikali kuonekana kuharakisha ujenzi wa bomba hilo.

"Unajua tatizo la ombwela uongozi linachangia kuvuruga mambo wakati wa uchimbaji. Rais Jakaya Kikwete aliwaahidi wakazi hao kuwa wangelijengewa kituo cha kufua umeme pamoja na kiwanda cha mbolea lakini kabla ya kutekelezwa hayo wakakimbilia kujenga bomba," alisema.

Profesa Lipumba alisema kuwa hata meneja wa kampuni inayojenga bomba hilo aliwahi kusema kuwa kama kiwanda hicho kingejengwa wakazi hao wangepata manufaa zaidi kuliko ujenzi wa bomba hilo.




 
Nilishasema katika thread nyingine.

1. Watu wa Mtwara hawapaswi kupuuzwa. Katika kupanga miradi inayohusisha rasilimali zilizo sehemu fulani, ni uungwana na utaratibu wa kawaida kuwajulisha wakazi wa eneo husika kwani ni wadau no. 1. Hili halikufanyika. Katika madai yao wameomba walau wapewe maelezo, badala yake waziri analaani.

2. Hii ni political issue, ambayo CCM itakuja kujikanyaga baadaye. Kumbukeni jinsi JK alivyowahi kusema hahitaji kura za walimu, baadaye kwenye kampeni akarudi na kufuta kauli. Mtasikia wakati wa kampeni CCM wanaenda na danganya toto na kutoa ahadi nyingi. Lakini watu waliokuwa wanakupenda na kukuamini wakishaghairi ni ngumu kuwarudisha.

3. Watu wa Mtwara wanahitaji kuona serikali inachukuwa hatua za makusudi za kuongeza fursa za kiuchumi kwa kutumia rasilimali hii ya gesi, na kufufua zao la kahawa linalosuasua. Njia mojawapo ni viwanda vinavyohusiana na rasilimali hizo. JK aliahidi, watu wanaona wamedanganywa.

CCM jipangeni upya, suala hili ni nyeti na kisiasa ni la kufa na kupona.
 
Kumbe tuna akina Mulugo wengi ktk baraza lla mawaziri la Jk -- hata Waziri Muhongo? Leo kanishtua ktk kioindi cha Nipashe Radio One alipotamka kuwa wananchi wa mtwara na Lindi wamekuwa wakipokea umeme kutoka Kihansi. jamani hii ni kweli Mikoa ya Kusini imeunganishwa katika gridi ya Taifa hivyo kupata umeme wa Kihansi?
 
Kumbe tuna akina Mulugo wengi ktk baraza lla mawaziri la Jk -- hata Waziri Muhongo? Leo kanishtua ktk kioindi cha Nipashe Radio One alipotamka kuwa wananchi wa mtwara na Lindi wamekuwa wakipokea umeme kutoka Kihansi. jamani hii ni kweli Mikoa ya Kusini imeunganishwa katika gridi ya Taifa hivyo kupata umeme wa Kihansi?

Nami nimemsikia akihojiwa na Joseph Ndamalya na nilishangaa kwa nini mtangazaji hakumbana kwa hilo. Pro Muhongi alkikuwa anajaribu kuonyesha kwamba Watu wa kusini hawana fadhila kwa kuwa nao sehemu yao imekuwa ikiendeshwa na mapato kutoka sehemu zingine za nchi na kutaja mkonge wa Tanga na Morogoro nk.

Kimakusudi aliacha kutambua kwamba korosho ya kusini nayo ilichangia maendeleo ya sehemu nyiongine za Tanzania.
 
Katika radio One leo asubuhi Waziri Muhongo alikuwa akilaani maandamano ya wanaMtwara kupinga gesi kuletwa Dar. Waziri muhongo alisema wakazi hao wa Mtwara hawana shukurani kwa sababu nao wamekuwa wakitumia umeme kutoka Kihansi.

Kimsingi, Umeme wa Kihansi haujafika Mtwara.
 
Kakosea neno lakini Mtwara na Lindi wana umeme wa uhakika unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia inayochimbwa hapo Mtwara sehemu ya Mnazi Bay takilibani miaka 7 sasa na kusambazwa katika mikoa hiyo miwili.Sema wana matumizi kidogo ukilinganisha uwezo wa mitambo ya kufua umeme na uzalishaji wa mkubwa wa gesi mkubwa.la msingi ni kuwekeza kama PTA na EPZA walivyoanza kugawa maeneo.

"Investors flock to Mtwara for gas and oil exploration"


Foreign investors are showing increased interest in Tanzania's Mtwara Freeport Zone ahead of gas and oil exploration activities next year.Already, the Export Processing Zones Authority (EPZA) and the Tanzania Ports Authority (TPA) have invited bids for leasing plots of between 6,200 square metres and 15,900 square metres area earmarked for oil and gas firms supply base.

EPZA research and planning manager James Maziku described the response to the invitation so far as positive.

"Many companies have shown interest to invest in the (Mtwara Freeport) zone - it's an indication that investors are eager to operate in the area," he said, noting that the respective authorities will meet soon to evaluate applications.

The Special Economic Zone Act 2006 and the EAC Customs Union (Freeport Operations Regulations) stipulate that companies seeking to undertake operations that provide services to oil exploration and gas extraction companies, should be limited to warehousing and storage, as well as labeling, packaging and repacking; sorting, grading, cleaning and mixing; breaking bulky; simple assembly and grouping of packages.

Gas-rich but underdeveloped Mtwara region has earmarked about 110 hectares for the Free Port Zone, with the first phase of the EPZA/TPA joint project on 10 hectares scheduled to operate as an oil and gas supply base.

According to EPZA infrastructure development manager Kenneth Haule, Mtwara is attractive for its depth as it allows bigger ships to anchor.

"The zone is also at a central location, meaning investors would be able to export oil and gas to Mombasa (Kenya), Mozambique, Zambia and other neighbouring countries," he said.

Investors are already flocking to the southern region to invest in manufacturing plants. Deep sea exploration is in progress by multinational companies -Petrobras, British Gas and Orphir, making it inevitable to have a logistical centre to supply materials and services to the companies for efficient operations. soureBy HELLEN NACHILONGO Special Correspondent
 
Kweli Hata pro.? Hawezi kufanya utafiti kidogo? hii habari imenistua sana! Siasa inaweza ikakutoa akili!
I will never practice it! shame on you muhongo! no muongo.
 
Aisee...mikoa ya kusini hawapo kwenye gridi ya taifa,huyo warizi kawekwa tu pale kwa kujuana
 
Kakosea neno lakini Mtwara na Lindi wana umeme wa uhakika unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia inayochimbwa hapo Mtwara sehemu ya Mnazi Bay takilibani miaka 7 sasa na kusambazwa katika mikoa hiyo miwili.Sema wana matumizi kidogo ukilinganisha uwezo wa mitambo ya kufua umeme na uzalishaji wa mkubwa wa gesi mkubwa.la msingi ni kuwekeza kama PTA na EPZA walivyoanza kugawa maeneo.

"Investors flock to Mtwara for gas and oil exploration"


Foreign investors are showing increased interest in Tanzania's Mtwara Freeport Zone ahead of gas and oil exploration activities next year.Already, the Export Processing Zones Authority (EPZA) and the Tanzania Ports Authority (TPA) have invited bids for leasing plots of between 6,200 square metres and 15,900 square metres area earmarked for oil and gas firms supply base.
gg

EPZA research and planning manager James Maziku described the response to the invitation so far as positive


"Many companies have shown interest to invest in the (Mtwara Freeport) zone - it's an indication that investors are eager to operate in the area," he said, noting that the respective authorities will meet soon to evaluate applications.



The Special Economic Zone Act 2006 and the EAC Customs Union (Freeport Operations Regulations) stipulate that companies seeking to undertake operations that provide services to oil exploration and gas extraction companies, should be limited to warehousing and storage, as well as labeling, packaging and repacking; sorting, grading, cleaning and mixing; breaking bulky; simple assembly and grouping of packages.

Gas-rich but underdeveloped Mtwara region has earmarked about 110 hectares for the Free Port Zone, with the first phase of the EPZA/TPA joint project on 10 hectares scheduled to operate as an oil and gas supply base.

According to EPZA infrastructure development manager Kenneth Haule, Mtwara is attractive for its depth as it allows bigger ships to anchor.

"The zone is also at a central location, meaning investors would be able to export oil and gas to Mombasa (Kenya), Mozambique, Zambia and other neighbouring countries," he said.

Investors are already flocking to the southern region to invest in manufacturing plants. Deep sea exploration is in progress by multinational companies -Petrobras, British Gas and Orphir, making it inevitable to have a logistical centre to supply materials and services to the companies for efficient operations. soureBy HELLEN NACHILONGO Special Correspondent


Issue hapa si wananchi wa Mtwara kuwa na umeme kutokana na gesi asilia; issue kuu ni kauli ya Prof. kuwa wananchi hawa kuwa wamekuwa wakitumia umeme wa Kihansi (Hydrothermal power) uliounganishwa ktk National Grid! Mleta uzi anauliza kama kuna ukweli ktk hili!
 
Nami nimemsikia akihojiwa na Joseph Ndamalya na nilishangaa kwa nini mtangazaji hakumbana kwa hilo. Pro Muhongi alkikuwa anajaribu kuonyesha kwamba Watu wa kusini hawana fadhila kwa kuwa nao sehemu yao imekuwa ikiendeshwa na mapato kutoka sehemu zingine za nchi na kutaja mkonge wa Tanga na Morogoro nk.

Kimakusudi aliacha kutambua kwamba korosho ya kusini nayo ilichangia maendeleo ya sehemu nyiongine za Tanzania.

ndo maana mwakyembe alisema waandishi wasome,,,,,,AKAELEWEKA TOFAUTI,
 
Aisee...mikoa ya kusini hawapo kwenye gridi ya taifa,huyo warizi kawekwa tu pale kwa kujuana

siasa zimeshaanza kumtafuna watu walikua wakimsifia hapa,wengine tukasema bado hajaanza kula utam.
Juz kawaita WENZIE WAHAINI,kwani waloandamana mtwara si sawa na wakurya wanaoandamana kwa ajili ya yale madini tu,
 
Issue hapa si wananchi wa Mtwara kuwa na umeme kutokana na gesi asilia; issue kuu ni kauli ya Prof. kuwa wananchi hawa kuwa wamekuwa wakitumia umeme wa Kihansi (Hydrothermal power) uliounganishwa ktk National Grid! Mleta uzi anauliza kama kuna ukweli ktk hili!

Umejichanganya kama alivyojichanganganya Profesa,wewe umesema Hydrothermal power sio sahihi. Kihasi inafua hydropower.hivyo nyote mnaeleweka kiundani japo mananeno si sahihi
 
Kweli Hata pro.? Hawezi kufanya utafiti kidogo? hii habari imenistua sana! Siasa inaweza ikakutoa akili!
I will never practice it! shame on you muhongo! no muongo.

nyie si ndo mlimuona bora sana enzi zile mnamtukana Zitto kwa kejeli wakati wa bajeti?mkashangilia kama mazuzu alipowatangazia sasa mgawo wa umeme basi coz unasababishwa na mafisadi?leo mnamgeuka?yaani sasa naanza kuamini kile nilichokidhania miaka mingi kuwa tatizo letu sio viongozi ni sisi wenyewe!!!!tuna akili za kushikiwa na hao mafisadi wanalitambua hilo so its just kutafuta namna nzuri ya kucheza na akili zetu coz they know that we are good ktk kuchezewa!!!damn luzaz
 
yule muhongo keshakua mwanasiasa sasa hivi, aache propaganda lini mikoa ya kusini imetumia huo umeme wao?
 
maajabu haya umeme wa kihansi mtwara! masikini prof. hata hajui grid ya taifa imeunganisha mikoa gani!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom