pamoja na mambo mengine, ametahadharisha watz kuhusu watu wanaojifanya wataalmu wa gesi na uranium kwa kuwa tu wamehudhuria kozi za mambo hayo za wiki tatu na kupata "certificate of attendance", ila hawajui lolote juu ya mambo hayo!
Pia hakuna kitu kinachoitwa mgao wa umeme (power rationing) kwa kuwa uwezo wa kuzalisha umeme ni mkubwa kuliko hata mahitaji ya siku! Hitaji la juu kabisa ni megawati 850 lakini wanazalisha megawati 1000+, kwa hiyo kwa hali hiyo hakuna mgao!
Pia kasema ewura na tanesco walikuwa na mpango wa kupandisha gharama za umeme january mwakani, amewapiga stop! Kwa kuwa hawana sababu kwani hata madeni ya tanesco serikali inawalipia!!!!!
Kasema pia ili kuondoa hiyo sura ya "mgao", inatakiwa viongozi wa tanesco mahali mahali wawe na utaratibu wa kutoa taarifa umeme ukatikapo ama kabla ya kukatika, na kueleza sababu za kukatika! Hii kitu kweli hawa jamaa huwa hawafanyi!
La mwisho nililopata ni kwamba, haka ka sura ka "mgao" kanaonekana kuna watu wanakafurahia kwa sababu za kisiasa, kiuchumi(wana maslahi yao- business), ama chuki binafsi! Yaani wanakalazimishia kaonekane kapo kumbe maskini hata hakuna mgao wa ukweli!!!!
Yangu ni hayo tu mkuu