Asante sana Ben:
1. Tumemsikiliza Prof. na hakutaja jina la mtu endapo Zitto na yeyote kwa sababu za upambe au binafsi au kuchonganisha watu atafikiria hivyo basi ni wao ndio wenye hayo matatizo tena watakuwa wamethibitika kuwa ndio wanaosemwa maana duniani wapotoshaji wapo kila mahala. Mimi nikisema hapa kuwa kuna wapotoshaji wanasema kuwa JF ni mtandao wa usalama wa Taifa Tanzania. Halafu wewe kati ya watu zaidi ya milioni 45 (Watanzania) ukafikiria kuwa nakusema wewe basi itakuwa ni kweli kuwa wewe ndiye unayesema hayo!!Nitakuwa sina cha kukusaidia zaidi ya kuendelea kukufuatilia miendo yako ili nijue unachotafuta ni nini zaidi?
2. Prof. Sospeter amefafanua vyema alipoulizwa kuwa je, sasa tusiosoma tusitoe mawazo au tusisikilizwe; alisema la hasha, wananchi wote watoe mawazo yao kwenye kuchangia sera nzuri ya gesi lakini alisema anawazungumzia WAPOTOSHAJI tena wenye elimu ndogo ya certificates of attendance ambao amewapa onyo.
Naumuunga sana mkono huyu Waziri. Kwanza lazima taaluma za watu ziheshimiwe maana hata yeye mwenyewe hajifanyi kujua mambo ya mafuta maana hiyo si taaluma yake ambayo alibobae ndio maana anawaheshimu wataalamu wa eneo uzalishaji wa gesi na amesema watahusishwa sana. Pili kuna watu wenye elimu ndogo katika jambo hujifanya wajuaji na kupotosha ukweli ni lazima tuwamulike na kuwaseme maana ni wa hatari sana! Hii si ajabu kukuta hata form two students wakawa wasumbufu (kiujuaji)kuliko a form four or six student, au Private akawa mkali na mwenye majingambo (Kijeshi)kuliko Luteni au Captain wa jeshi ndivyo ilivyo watu wachache wenye vyeti vya chini wanaweza kujifanya kuwa wajuzi wa kila kitu na kudharau kazi anayoifanya Prof. Sospeter eti kwa vile tu wamepata mafunzo fulani ya muda mfupi au kaenda ziara mahala na kuuliza kuhusu Uranium au natural gas exploration.
Nimemsikiliza huyu mtu, nampa muda atekeleze anachosema na kuamini na nitamuhukumu baada ya kupima alipofikia katika yale anayoahidi lakini si upuuzi wa kupotosha. Mfano watu walisema kuwa alitaka tu bajeti ipite baada ya hapo nchi yote ingeingia gizani!! Upuuzi mtupu!! maana tunajua kuwa kuna utofauti kati ya umeme kukatika kwa sababu za uchakavu wa mitambo na miundombinu kwa ujumla na mgawo wa umeme kwa sababu za uchache wa umeme (megawatts) zinazozalishwa!! Na hili pia amelifafanua leo- well done!
Huyu jamaa kweli si mwanasiasa hata utamsikia utofauti wake na mtu anayetaka kujiingiza katika malumbano yasiyo na tija. Nilifurahia jibu alilotoa kuwa hawana mkakati wa kuwadhibiti wapotoshwaji bali wao wataendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika na hayo ndiyo tunayatafuta ukiongezea kuwa uwe ambao tunaweza kumudu gharama zake.