Prof. Muhongo ampiga dongo Zitto Kabwe(?)

Prof. Muhongo ampiga dongo Zitto Kabwe(?)

Swat

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
4,201
Reaction score
2,002
Anasema hakuna haja ya kuwa na mambo ya umeme wa dharura kwani ndio chanzo cha ufisadi. Asisitiza hakuna na hakutokuwa na mgao wa umeme. Asema kila mtu anaongelea mambo ya gesi,hata wasiokuwa na utaalamu wanaongelea kama wataalamu na hivyo wanapotosha umma. Kwa hayo na mengine mengi angalia ITV saa 3 usiku leo,kipindi cha dakika 45.
 
Kumbe Hakijarushwa bado. Jamani mnaoshika ITV huko mtujuze hapa waziri kasema nini?
 
Umejuaje kama atasema hivyo BAADE? Au ndio yale ya JF imekua shimo la uchafu?
 
JF sasa inachosha, mtu anasema live halafu anakwambia angalieni saa tatu.

Mods wasumbufu kama hawa kwa nini wasile ban hata ya siku mbili viherehere viwaishe, mnatuchosha!!
 
Pia usikose kuangalia sTAR TV jumapili saa moja unusu atakuwepo Freeman mbowe na mtu mwenye hadhi yake toka ccm kuongelea Rushwa kwenye vyama vya siasa ,kipindi kinaratibiwa na YAHAYA M.
Hiyo itakuwa live!
 
Ebu badili heading yako mwenzio nikaenda ITV nkakuta mziki umeniboa
Ila nashukuru kwa kunikumbusha icho kipindi maana uyu mheshimiwa huwa namkubali sana he is a professional not a politician
 
Wadau samahani kwa kusema LIVE. Ni kwamba ITV wamerusha vidokezo vya kipindi hicho kitakachorushwa hewani saa tatu usiku wa leo.
 
Wadau samahani kwa kusema LIVE. Ni kwamba ITV wamerusha vidokezo vya kipindi hicho kitakachorushwa hewani saa tatu usiku wa leo.

Huna haja ya kuomba msamaha mkuu. Tatizo ni kuwa uelewa wa watu wengi humu ni wa shule za kikatakata tu. Watu wanataka kutafuniwa hadi madem zao wenyewe.
 
Ebu badili heading yako mwenzio nikaenda ITV nkakuta mziki umeniboa
Ila nashukuru kwa kunikumbusha icho kipindi maana uyu mheshimiwa huwa namkubali sana he is a professional not a politician

Well said mkuu.
 
Wadau samahani kwa kusema LIVE. Ni kwamba ITV wamerusha vidokezo vya kipindi hicho kitakachorushwa hewani saa tatu usiku wa leo.

Hongera kwa kukiri kosa na asante kwa taarifa......
 
Hatakuja na jipya am telling you, kiapo kinasema kuwa atatunza siri za baraza la mawaziri na atakuwa mtiifu kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania so usitegemee jipya ni zilezile kelele za kila siku
 
Wadau samahani kwa kusema LIVE. Ni kwamba ITV wamerusha vidokezo vya kipindi hicho kitakachorushwa hewani saa tatu usiku wa leo.

Tunasubiri aongee kiboko wa mgawo wa Umeme. Hongera Prof. Keep it up.
 
Hatakuja na jipya am telling you, kiapo kinasema kuwa atatunza siri za baraza la mawaziri na atakuwa mtiifu kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania so usitegemee jipya ni zilezile kelele za kila siku
Mbona una mchecheto subiri mwana JF vuta Subira uwe na Subira usikie atakayosema mkombozi anayetuepusha na mgawo wa umeme
 
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Mhongo amesema kamwe hatafuata ushauri unaohusu gas kwa watu ambao wamehudhuria mafunzo ya wiki moja ya gas na kupata cheti cha mahudhurio 'certificate of attendance' na amekemea tabia ya watu hao kujifanya wanajua sana masuala ya gas kuliko wataalam wenyewe.

Binafsi hili nimeona kama ni dongo kwa ZZK ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akikosoa utendaji kazi wa Prof Mhongo hasa kuhusiana na sector hii ya gas.

Zitto amewahi kujinasibu kwamba yeye si mtaalam wa madini na gas lakini akasema, namnukuu,
Kutojua si makosa, inawezekana kuwa wengine hatukusomea miamba lakini tumesomea masuala ya kodi kwenye madini na mafuta. Waziri makini anayejali nchi yake anawezaje kukutana na mwekezaji anayekataa kukulipa kodi yako bila wewe hata kuulizia utalipwa lini?

Nimuombe Mheshimiwa waziri si kila ushauri unaotolewa na mtu ambaye si mtaalam wa sector husika basi si mzuri, namuomba aache kurusha madongo kwa watu wanaomkosoa, kiongozi asiyetaka kukosolewa hafai kuwa kiongozi.

Naomba ofisi ya wizara ya nishati na madini isikufanye ujisahau sasa, chukua kukosolewa kama ni challenges za wewe kufanya vizuri. Kama huelewani na ZZK kama mtu lakini chukua ushauri wake.
 
Back
Top Bottom