Prof. Mlambiti wa SUA - Jiwe lililosahaulika

Prof. Mlambiti wa SUA - Jiwe lililosahaulika

Tatizo mkuu siyo kuandika anachokumbuka,, shida ni kutohoa moja kwa moja kutoka kwenye Kiswahili kwenda Kiingereza. Mkapa, kwenye andiko langu nini nilichokuambia kuhusu kufungua mabarabara ya vijijini? Umeshajaribu kukaa na msafara (sasa hiki ni nini?) wako na kutupatia mrejesho?
acha ligi za kijinga wewe.andika kwa kiingereza basi
 
Nimefatilia hii thread nimegundua humu Jf kuna watu wameenda shule sana, japo nikiwa nyuma ya keyboard nawadharau kuanzia leo wakuu ntakua nawaheshimu sana
 
Sisi wanajamvi tumesikia sifa zao maprof wa SUA. Tungependa kusikia "tangible outcomes on the ground" kutokana na umahiri huu kwenye kazi mnazofanya. Nafikiri kwa kutaja mambo kadhaa aidha ya kuwakomboa kiuchumi yanayotokana na mafunzo yao ndiyo ingekuwa zawadi pekee kubwa kwao.
 
Nashauri vyuo vikuu pamoja na wadau wengine waanzishe Forum.com ya maprof kama hawa. Ingefanya Taifa kuendelea kupata mawazo yao kwa current na noncurrent issues. Sina uhakika kama SUA au vyuo vingine wana jukwaa maalumu kwa wastaafu hawa. Hawa bado ni hazina kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
 
Prof.Mlambiti mtaalamu wa Agricultural Economics and Agribusiness, huyo mzee kwenye lecture zake ilikuwa ni critics mwanzo mwisho kwa serikali sijui walimkosea nini, pia alijaribu mara kadhaa kugombea ubunge jimbo la Ulanga kwa tiketi ya ccm lakini alikuwa anashindwa kwenye kura za maoni.
 
Tatizo mkuu siyo kuandika anachokumbuka,, shida ni kutohoa moja kwa moja kutoka kwenye Kiswahili kwenda Kiingereza. Mkapa, kwenye andiko langu nini nilichokuambia kuhusu kufungua mabarabara ya vijijini? Umeshajaribu kukaa na msafara (sasa hiki ni nini?) wako na kutupatia mrejesho?
 
Leo nimekua nikitafakari mambo mbalimbali yanayoikabili nchi hii na nikajikuta namkumbuka prof.Mlambiti kwa mambo mbalimbali na jinsi alivyokua anaonesha hisia zake anavyoumizwa na mustakabali wa nchi hii.

Kwanza hajawahi kuamini kama CCM inania ya dhati ya kuikwamua nchi hii kiuchumi na kimaendeleo japo anaamini kuna watu ndani ya CCM wangeweza kujilipua na kuifikisha TZ mbali sana na hawakuwahi kufanya hivyo na hawatofanya hivyo... Akiwemo Raisi wa sasa na aliyepita kabla yake (Mkapa).

Prof. Mlambiti (a.k.a Babu) alitufundisha pale SUA miaka ya 2000 mwanzoni ni mtu aliyethubutu mara kadhaa kupingana na Mwalimu Nyerere juu ya Sera za kilimo za nchi hii akiamini ubunifu juu ya kilimo ungekomboa zaidi 80% ya wananchi wa TZ kama serikali ikiamua kuwekeza katika tafiti na rasilimali zingine pamoja na ukuzaji wa viwanda na masoko ndani na nje ya nchi.

Prof. Mlambiti daima fikra zake haziwezi kufa kichwani mwa mtu yeyote aliyemfundisha kwa kuwa aliongea maono, ukweli, na hali halisi bila kujali itikadi zozote na alisema ni kizazi kingine ndicho kitaibadilisha Tanzania na ni kizazi kitakachokuja kuishangaa sana historia ya kizazi hiki cha sasa kwa uzembe na uvivu mkubwa wa kufikiri.

Prof. Mlambiti ambaye alitufundisha sana elimu ya ujasiriamali (japo ilikua kama kitu kigeni sana kwa jamii ya TZ) ni mzee aliyetuhamasisha sana vijana kuumiza akili na kujitengenezea ajira kuondokana na utumwa wa fikra ambao vijana wote wa wakati ule tulikua nao.. Na waliofuata aliyoyafundisha na kuthubutu si wenzetu tena leo hii kiuchumi.

Ni mtu pekee ambaye huja mara nyingi kichwani mwangu kila linapotokea vuguvugu la uchaguzi, scandal za kifisadi,migogoro ya ardhi, migogoro ya kidini na hata migogoro ya kiuchumi kwa sababu ya maono na mafundisho yake na mara zote huwa natamani nijue ni nini anafikiria kwa wakati huo.

Kiufupi mzee yule ni hazina kubwa iliyosahaulika..na yeyote aliyewahi kuhudhuria darasa lake hawezi kusahau maishani mwake mafundisho ya yule mzee.
Mi namkumbuka mwl. Wangu wa pr/school pale singabora Moshi.
Mwl. Ngaraniza ni nouma
 
Punguzeni kelele

Atapangiwa kazi nyingine
 
Back
Top Bottom