Site tunajua watoto wetu wa kidato Cha Tano waliaanza shule mwezi wa 8 badala ya mwezi 7. Hii ilienda sambamba na kubadilisha mihula na kupanga wasome mpaka 22 Desemba. Lakini hili limeshindikana na tayari watoto wetu wa kidato cha 5 wameshafanya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza na wenzao wa kidato cha sita?
Nilihoji hili kwa Mkuu mmoja shule baada ya kuambiwa nitume nauli ya mwanangu. Sababu ya kutotekelezwa hili majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo. Kwanza, shule yao ni kituo cha kusahihisha mitihani ya kidato cha nne, wasahihishaji wanatakiwa kutumia madarada, viti, vitanda mabweni ya wanafunzi na wanaripoti wiki hii.
Na hata zile shule ambazo siyo vituo walimu wengi wa shule mbalimbali wanatakiwa kwenda kusahihisha mitihani hiyo na NECTA hawakuzingatia anafundisha kidato cha 5 au laa. Tatu, walimu wengi likizo yao ya siku 28 zinaanza wiki hii Ili wakifungua ziwe zimeisha.
Kwa sababu hizo hata ukiwaacha watoto mpaka hiyo tarehe 22 mliyopendekeza watoto watafundishwaje. Kwa nini nasema waziri Mkenda na maafisa wake wanakurupuka. Wakati wanapanga mihula hiyo walipaswa kuweka utaratibu mzuri kuhakikisha kuwa likizo za walimu, walimu watakaohusika na zoezi la usahihishaji na vituo vya usahihishaji haviathiri shule zenye kidato cha Tano.
Sijajua kama Wizara inaweza kusitisha likizo ya mwalimu kwa kumlipa kama wanavyolipana wao. Nitakuja na kutotekezeka kwa mitaala mipya kuanza mwakani hata kama ataanza kwa shule chache. Hili angewaachia VETA tu.