Prof. Mkenda una maamuzi ya kukurupuka kwenye elimu. Unajua hata Form 5 haitekelezeki kusoma mpaka 22 Desemba. Iweje mitaala mipya mwakani?

Tozo

Member
Aug 23, 2021
76
154
Site tunajua watoto wetu wa kidato Cha Tano waliaanza shule mwezi wa 8 badala ya mwezi 7. Hii ilienda sambamba na kubadilisha mihula na kupanga wasome mpaka 22 Desemba. Lakini hili limeshindikana na tayari watoto wetu wa kidato cha 5 wameshafanya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza na wenzao wa kidato cha sita?

Nilihoji hili kwa Mkuu mmoja shule baada ya kuambiwa nitume nauli ya mwanangu. Sababu ya kutotekelezwa hili majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo. Kwanza, shule yao ni kituo cha kusahihisha mitihani ya kidato cha nne, wasahihishaji wanatakiwa kutumia madarada, viti, vitanda mabweni ya wanafunzi na wanaripoti wiki hii.

Na hata zile shule ambazo siyo vituo walimu wengi wa shule mbalimbali wanatakiwa kwenda kusahihisha mitihani hiyo na NECTA hawakuzingatia anafundisha kidato cha 5 au laa. Tatu, walimu wengi likizo yao ya siku 28 zinaanza wiki hii Ili wakifungua ziwe zimeisha.

Kwa sababu hizo hata ukiwaacha watoto mpaka hiyo tarehe 22 mliyopendekeza watoto watafundishwaje. Kwa nini nasema waziri Mkenda na maafisa wake wanakurupuka. Wakati wanapanga mihula hiyo walipaswa kuweka utaratibu mzuri kuhakikisha kuwa likizo za walimu, walimu watakaohusika na zoezi la usahihishaji na vituo vya usahihishaji haviathiri shule zenye kidato cha Tano.

Sijajua kama Wizara inaweza kusitisha likizo ya mwalimu kwa kumlipa kama wanavyolipana wao. Nitakuja na kutotekezeka kwa mitaala mipya kuanza mwakani hata kama ataanza kwa shule chache. Hili angewaachia VETA tu.
 
Mods badirisha heading. Wanafunzi kidato 5 wafunga kabla ya tarehe iliyopangwa na Wizara, 22 Desemba. Ushahidi upo, wanafunzi kidato 5 wapo mitaani. Hata wakuu wa shule wanao ogopa kuwatoa hawasomi na wameshafanya mitihani ya kufunga kabisa
 
Nishawaambia huyu mzee anajiita prof nkenda ni mkurupukaji..

Hiyo wizara haimfahi kabisa.. sijui kwanini kaachwa wizara hiyo. Kila kitu anakurupuka tu
 
Madogo mitihani wanamaliza trh 15 halafu nyie mnajifanya kuipeleka shule mpaka 22 dec.
***** mtafika wenyewe.
Dogo akimaliza tu pepa naenda kukiwasha shuleni kwao.
Huu upuuzi haijawahi kutokea.

Kama uongozi umewashinda si muachie ngazi.
Kwani ni lazima mtawale nyinyi kila siku.
Matusi mengine mnajitafutia wenyewe
 
Kupima afya ya akili ni muhimu Kwa Kila. Waziri wa afya fanya mchakato wa sera ya afya akili Kwa Kila mtanzania mwenye akili timamu
 
Ukisikia prof unawez kusema huyu zimo, ukifatilia mambo yake unajiuliza huyu profesa gani, mbona chenga hivi. 😂🤣
 
Hii wizara ni nyeti sana lakini cha kushangaza huwa inachezewaga mno, sijui kwanini mamlaka za juu yake huwa hailioni hili.
 
Huu ujinga umekaakaaje, mbona wananichanganya hawa?
Safari hii naona wengi jela watatupeleka. Haiwezekani watoto wetu wakumbwe na ujinga huu!
 
Hii wizara kila mtu anakuja na mambo yake.Kuna waziri aliwahi kuchanganya physics na Chemistry, mwingine akaja na mfumo wa GPA na sasa tunaenda na "mwisho darasa la 6"....
 
Wizara haina mawasiliano na idara zake. Kila mmoja anajiamulia tu aonavyo yeye inafaa.
 
Back
Top Bottom