Prof. Mark Mwandosya ni mpotoshaji

Pumbavu, Mandela alifungwa kwa makosa ya kisiasa yanaitwaje?
Wewe ni nani umpangie 'Profesa' kitu cha kuongea?!
Eti yupo ccm, anatibiwa na Serikali SO WHAT?! Hela za Serikali ni za familia yako?!
 
Na Jumanne Lutengano Majoka
Mjasiriamali Mbeya Mjini.

Hakuna mashaka kuwa mapokezi ya bashasha na kauli aliyoiandika Prof. Mark Mwandosya katika ukurasa wake wa Twitter baada Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” kuachiwa kwa msamaha wa Rais hapo jana anaungana na kauli ya Sugu mwenyewe kuwa adhabu aliyoipata kwa kumtusi Rais ilikuwa ni kifungo cha kisiasa.

Kwa Prof. Mwandosya na Sugu mwenyewe ni vizuri kujiepusha na upotoshaji huu. Sugu alifungwa kwa kosa la jinai na hivyo alikuwa mfungwa wa kosa la jinai na sio mfungwa wa kisiasa kama anavyodai.

Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.

Lakini Sugu sio mfungwa wa kisiasa, Sugu ni mhalifu, alifanya makosa ya kuvunja sheria za nchi kwa kumtukana Rais. Hata utambulisho wake anaitwa Mfungwa namba 219/2018 na sio Mfungwa wa Kisiasa namba 219/2018 kama anavyodai na kama Prof. Mwandosya anavyounga mkono.

Hizi ni siasa za kipuuzi na zinapoungwa mkono na mtu mwenye utumishi kwa nchi kama Prof Mark Mwandosya inatia wingu zito na inavunja heshima.

Nimejiuliza sana kuhusu lengo la Prof. Mark Mwandosya kumpokea Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyetolewa jana Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais na ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter. Tena Prof. Mwandosya kafunga safari hadi nyumbani kwake Sugu kumpokea na kuandika alichoandika.

Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.

Na akaendelea kwa kimombo “Congratulating Hon.Joseph Mbilinyi-right after graduating from Ruanda Prison Mbeya”

Baadaye Sugu nae kapost picha kwenye Instagram wakiwa wamekaa na Prof Mwandosya nyumbani kwake Sugu na Prof Mwandosya akinywa juisi na kaandika “Nikiwa na Prof. Mwandosya nyumbani kwangu leo. Asante kwa maneno ya busara na ujasiri ulionipa leo na hata ulipokuja kuniona gerezani”

Ukiunganisha nukta za kauli za Prof. Mwandosya na Sugu haileti mashaka kuwa wanaongea lugha moja kwamba Sugu ni mfungwa wa kisiasa na wanataka kuaminisha umma kuwa Sugu alionewa kwa adhabu ile.

Niseme hivi kwa Sugu kutoa kauli hizo haina shida kwa sababu kwa namna yoyote baada ya kukumbwa na adhabu ile ilitarajiwa kuwa atataka kuitumia kwa manufaa ya kisiasa, lakini kwa Prof Mwandosya kuna ukakasi.

Kuna ukakasi kwa sababu Prof. Mwandosya ni Mwanachama wa CCM na aliyetukanwa na Sugu ni Mwenyekiti wake. Kwa alichokiandika Prof. Mwandosya ni wazi kuwa anaamini Sugu alionewa na anamtia moyo kuwa amefuzu chuo cha uanasiasa katika gereza la Ruanda. Anaamini kuwa Rais Magufuli alistahili kutukanwa vile na Sugu na hakubaliani na adhabu aliyopewa na mahakama kwa mujibu wa sheria.

Prof. Mark Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho awali kilifanya kazi ya kutengeneza makada na sasa kinafundisha kozi mbalimbali za uongozi, siasa, uchumi n.k. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chuo hiki na Rais Magufuli ambaye ametukanwa na Sugu na hakukataa uteuzi huu.

Prof. Mwandosya ni Waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne na ni mtu aliyejitokeza mara mbili kutaka ridhaa ya wana CCM ili agombee kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio.

Kwa miaka takribani 7 sasa Prof. Mwandosya amekuwa akisumbuliwa na maradhi makubwa ambayo yamelazimu awe anapatiwa matibabu nchini India kwa gharama za Serikali. Hata sasa anaishi na vyuma ambavyo anahitaji kupatiwa matibabu nje ya nchi.

Kwa mazingira hayo hapo juu, Prof. Mwandosya angepaswa kuwa makini na kauli zake na ikiwezekana aamue moja ama kujipambanua kuwa yeye sasa anaunga mkono siasa za upinzani na kujihusisha na upinzani kwa uwazi ama kuchunga kauli zake. Aamue ama kuwa moto ama kuwa baridi aache double standards.

Ni jambo linalokanganya kwamba anatumikia cheo alichopewa na Rais Magufuli, anatibiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na ni mwanachama wa chama kinachoongozwa na Rais Magufuli halafu anamuunga mkono mtu anayemtukana Rais Magufuli.

Na hii sio mara ya kwanza kwa Prof. Mwandosya kufanya double standards hizi. Mwaka 2015 alipokosa kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM aliibuka na kumshambulia Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipinga mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Ilitushangaza wengi kwa sababu Prof. Mwandosya alipaswa kujua kwa nini chama kiliamua kumteua Magufuli na angepaswa kuelewa hata manufaa ambayo chama kimeyapata maana ni wazi kwamba kama wangepitishwa waliokuwa wanatajwatajwa pengine chama kingepoteza kwenye uchaguzi mkuu.

Nakusihi Prof Mwandosya kama una mahaba na upinzani hamia huko, mimi kama Mtanzania ninayeamini katika utawala wa sheria, na ninajitahidi kupambanua mambo kwa maslahi ya Taifa naona unachokifanya sio sawa, kama wanavyosema vijana inawezekana unataka kupata Kiki au uendelee kupata umaarufu wa kisiasa, lakini kwa heshima yako hili unalolifanya unakuwa Kivuruge.

Sipendezwi na aina ya siasa zinazofanywa na upinzani na ni miongoni mwa watu wanaopenda kuwepo upinzani wenye tija na sio upinzani unalivuruga Taifa kama huu tulionao Tanzania. Tuna upinzania ambao hauna dalili za kushika dola na hauna tija.

Namsihi Rais Magufuli kuwa makini na Prof. Mwandosya, tunaojua mienendo ya kisiasa tunajua kuwa huyu ana visilani vya kisiasa na alihofiwa sana kwa siasa za ukanda.

Alituhumiwa hivyo kutokana na namna alivyofanya siasa zake mwaka 2005 alipochuana na Jakaya Kikwete katika ngazi ya chama. Kwa wakati ule zilikuwa ni nguvu za mtandao. Mtandao wa Prof. Mwandosya ulibeba sura ya kikanda zaidi.

Nionavyo mimi kama Prof. Mwandosya hatojisahihisha ni wakati sasa wa Rais Magufuli kumuengua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni. Aachwe huru ili afanye siasa za upinzani kwa uhuru zaidi, aungane na Sugu na wanasiasa wengine wa upinzani kufanya siasa bora zaidi.

Prof Mwandosya aamue kuwa baridi au kuwa moto.

Mimi ni mwananchi wa Tanzania
Naitwa Jumanne Lutengano Majoka.
Kila mtu kaochoka ccm ni wajinga wenye elimu ndogo masikini wa kutupwa wasio na vision na kina mama wa vijijini ndiyo wana i support ccm

Mwanahabari Huru Mshana Jr BAK FaizaFoxy Ritz
 
Acheni kumshambulia mleta mada, Jibubi hoja zake. Mleta mada yuko sahii, Sugu alifanya kosa la jinai na alihukumiwa kifungo baada ya kutiwa hatiani. Hili halina ubishi, na utabaki kuwa ukweli daima.

Kosa alilohukumiwa sugu ni kosa la jinai na si kosa la kisiasa kama inavyopotoshwa. Sheria zimetungwa, makosa na adhabu zikabainishwa. Hilo kosa na adhabu yake lipo kwa mtu yeyote. Hata Nyangema mchoma mikaa kule tuliani akifanya kosa hilo atashtakiwa na kuhukumiwa tu.
hivi aliyeiwaita wanasiasa wenzake malofa na wapambavu naye alitenda jinai???
 
Ni rahisi tu kumpa huru achague njia aipendayo,wengine walizaliwa kuishi kwa teuzi serikalini sasa bila teuzi maisha hayaendi sawa!

Mwandosya alitangaza mwenyewe kustaafu na kuonyesha jinsi gani alivyo serious hadi diplomatic passport alirudisha
 
Na Jumanne Lutengano Majoka
Mjasiriamali Mbeya Mjini.

Hakuna mashaka kuwa mapokezi ya bashasha na kauli aliyoiandika Prof. Mark Mwandosya katika ukurasa wake wa Twitter baada Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” kuachiwa kwa msamaha wa Rais hapo jana anaungana na kauli ya Sugu mwenyewe kuwa adhabu aliyoipata kwa kumtusi Rais ilikuwa ni kifungo cha kisiasa.

Kwa Prof. Mwandosya na Sugu mwenyewe ni vizuri kujiepusha na upotoshaji huu. Sugu alifungwa kwa kosa la jinai na hivyo alikuwa mfungwa wa kosa la jinai na sio mfungwa wa kisiasa kama anavyodai.

Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.

Lakini Sugu sio mfungwa wa kisiasa, Sugu ni mhalifu, alifanya makosa ya kuvunja sheria za nchi kwa kumtukana Rais. Hata utambulisho wake anaitwa Mfungwa namba 219/2018 na sio Mfungwa wa Kisiasa namba 219/2018 kama anavyodai na kama Prof. Mwandosya anavyounga mkono.

Hizi ni siasa za kipuuzi na zinapoungwa mkono na mtu mwenye utumishi kwa nchi kama Prof Mark Mwandosya inatia wingu zito na inavunja heshima.

Nimejiuliza sana kuhusu lengo la Prof. Mark Mwandosya kumpokea Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyetolewa jana Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais na ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter. Tena Prof. Mwandosya kafunga safari hadi nyumbani kwake Sugu kumpokea na kuandika alichoandika.

Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.

Na akaendelea kwa kimombo “Congratulating Hon.Joseph Mbilinyi-right after graduating from Ruanda Prison Mbeya”

Baadaye Sugu nae kapost picha kwenye Instagram wakiwa wamekaa na Prof Mwandosya nyumbani kwake Sugu na Prof Mwandosya akinywa juisi na kaandika “Nikiwa na Prof. Mwandosya nyumbani kwangu leo. Asante kwa maneno ya busara na ujasiri ulionipa leo na hata ulipokuja kuniona gerezani”

Ukiunganisha nukta za kauli za Prof. Mwandosya na Sugu haileti mashaka kuwa wanaongea lugha moja kwamba Sugu ni mfungwa wa kisiasa na wanataka kuaminisha umma kuwa Sugu alionewa kwa adhabu ile.

Niseme hivi kwa Sugu kutoa kauli hizo haina shida kwa sababu kwa namna yoyote baada ya kukumbwa na adhabu ile ilitarajiwa kuwa atataka kuitumia kwa manufaa ya kisiasa, lakini kwa Prof Mwandosya kuna ukakasi.

Kuna ukakasi kwa sababu Prof. Mwandosya ni Mwanachama wa CCM na aliyetukanwa na Sugu ni Mwenyekiti wake. Kwa alichokiandika Prof. Mwandosya ni wazi kuwa anaamini Sugu alionewa na anamtia moyo kuwa amefuzu chuo cha uanasiasa katika gereza la Ruanda. Anaamini kuwa Rais Magufuli alistahili kutukanwa vile na Sugu na hakubaliani na adhabu aliyopewa na mahakama kwa mujibu wa sheria.

Prof. Mark Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho awali kilifanya kazi ya kutengeneza makada na sasa kinafundisha kozi mbalimbali za uongozi, siasa, uchumi n.k. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chuo hiki na Rais Magufuli ambaye ametukanwa na Sugu na hakukataa uteuzi huu.

Prof. Mwandosya ni Waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne na ni mtu aliyejitokeza mara mbili kutaka ridhaa ya wana CCM ili agombee kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio.

Kwa miaka takribani 7 sasa Prof. Mwandosya amekuwa akisumbuliwa na maradhi makubwa ambayo yamelazimu awe anapatiwa matibabu nchini India kwa gharama za Serikali. Hata sasa anaishi na vyuma ambavyo anahitaji kupatiwa matibabu nje ya nchi.

Kwa mazingira hayo hapo juu, Prof. Mwandosya angepaswa kuwa makini na kauli zake na ikiwezekana aamue moja ama kujipambanua kuwa yeye sasa anaunga mkono siasa za upinzani na kujihusisha na upinzani kwa uwazi ama kuchunga kauli zake. Aamue ama kuwa moto ama kuwa baridi aache double standards.

Ni jambo linalokanganya kwamba anatumikia cheo alichopewa na Rais Magufuli, anatibiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na ni mwanachama wa chama kinachoongozwa na Rais Magufuli halafu anamuunga mkono mtu anayemtukana Rais Magufuli.

Na hii sio mara ya kwanza kwa Prof. Mwandosya kufanya double standards hizi. Mwaka 2015 alipokosa kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM aliibuka na kumshambulia Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipinga mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Ilitushangaza wengi kwa sababu Prof. Mwandosya alipaswa kujua kwa nini chama kiliamua kumteua Magufuli na angepaswa kuelewa hata manufaa ambayo chama kimeyapata maana ni wazi kwamba kama wangepitishwa waliokuwa wanatajwatajwa pengine chama kingepoteza kwenye uchaguzi mkuu.

Nakusihi Prof Mwandosya kama una mahaba na upinzani hamia huko, mimi kama Mtanzania ninayeamini katika utawala wa sheria, na ninajitahidi kupambanua mambo kwa maslahi ya Taifa naona unachokifanya sio sawa, kama wanavyosema vijana inawezekana unataka kupata Kiki au uendelee kupata umaarufu wa kisiasa, lakini kwa heshima yako hili unalolifanya unakuwa Kivuruge.

Sipendezwi na aina ya siasa zinazofanywa na upinzani na ni miongoni mwa watu wanaopenda kuwepo upinzani wenye tija na sio upinzani unalivuruga Taifa kama huu tulionao Tanzania. Tuna upinzania ambao hauna dalili za kushika dola na hauna tija.

Namsihi Rais Magufuli kuwa makini na Prof. Mwandosya, tunaojua mienendo ya kisiasa tunajua kuwa huyu ana visilani vya kisiasa na alihofiwa sana kwa siasa za ukanda.

Alituhumiwa hivyo kutokana na namna alivyofanya siasa zake mwaka 2005 alipochuana na Jakaya Kikwete katika ngazi ya chama. Kwa wakati ule zilikuwa ni nguvu za mtandao. Mtandao wa Prof. Mwandosya ulibeba sura ya kikanda zaidi.

Nionavyo mimi kama Prof. Mwandosya hatojisahihisha ni wakati sasa wa Rais Magufuli kumuengua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni. Aachwe huru ili afanye siasa za upinzani kwa uhuru zaidi, aungane na Sugu na wanasiasa wengine wa upinzani kufanya siasa bora zaidi.

Prof Mwandosya aamue kuwa baridi au kuwa moto.

Mimi ni mwananchi wa Tanzania
Naitwa Jumanne Lutengano Majoka.
Kumbe na wewe hukuelewa
 
Maandishi unajichanganyaaa hadi unasahau ulipoanzia!
Kwanza unakiri kuwa Sugu alifungwa, tatizo ni kwa kosa lipi! Tafsiri yako ni kosa la kawaida (jinai), n.a. kuwa si vinginevyo.

Swali: Maneno aliyotamka Sugu ni TUSI kwa tafsiri ipi,alikuwa wapi n.a. alikusudia nini?
Pili ni Sugu pekee anayetumia lugha aina hiyo (Lusinde,Magufuli,Mkapa) wameshafiikishwa mahakama ipi kama makosa ya kutumia lugha aina hizo ni jinai kawaida?.

Tatu uwoga wa kusema ukweli ili mtu aendelea kupata stahiki zake ni sumu Kali! Mwandosya kutumia haki yake ya kujieleza,wewe unaleta habari ya kutibiwa kwa gharama ya serikali (kujipendekeza,kujikomba).Roho mbaya kama ya Rais alivyodai kutoidhinisha malipo ya Maalim Seif kisa kamnyima Shein mkono)!

Ni aibu kwa mtu mzima kujivua nguo hadharani.
 
UCD: Nyie CCM mnajivunia mbeleko ya vyombo vya dola kushinda uchaguzi lakini siyo ushawishi.
 
Kuteuliwa na Rais hakumfanyi kuwa kipofu kwa matendo yanayomhusu aliyemteua. Anabaki na HAKI zake zote,vinginevyo kwa wale wasiojitambua(Hii haihusiani na mkasa wa Sugu bali maelezo yako)

Pili,usitarajie kuwa ni jambo rahisi kumkuta mfungwa wa kisiasa gerezani na akawa na namba ya utambulisho kuonesha ni mfungwa wa kisiasa. Usiwafanye waliomfunga hawalijui hilo,naamini hata wewe unajua ila upo katika kutekeleza kazi zako.

Tatu,utofauti wa vyama hauwezi kutuondolea utu hadi tusifarijiane baada ya matatizo. Vinginevyo utuelze kama unafurahishwa na kifungo cha Sugu? Hapa usilisemee kundi lako bali nafsi yako.

Nimalize kwa kusema kuwa,ukiachilia mbali CV ya Prof. Mwandosya..........anayo haki ya kutoa maoni yake kama mwananchi mwingine. Tusiishi kwa fitina na kutafutiana makosa. Mwacheni mzee wa watu
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Dragoon: Mbona hamtutajii sasa hilo kosa la jinai alilofanya Sugu? Kwani kama ni tusi halina jibu? Hivi yule hakimu yuko wapi maana nasikia alitoweka mara tu baada ya kusoma hukumu. Kwani mlienda kumficha wapi? Tunajua Lipumba mlimpeleka Rwanda na mzee wa mihogo Dr. Slaa mkampeleka akale bata Canada. Huyu mmempeleka wapi?
 
Ninasikia hata Mbeya hajafanya kitu chochote. Mbeya vijana wengi ninasikia ni wasomi na ni jobless, naambiwa hajafanya chochote na ni mselfish. Mbeya wanamkumbuka Mwakangale, Mwambulukutu, Mwaikambo kidogo kwa mbali sasa wanatumaini na Dr Tulia. Mwandosya ni mtu wa Visasi na Hana msaada Wowote kwenye Chama au serikali Mbeya. Ukiona kijana wa Mbeya yupo kwenye nafasi yoyote Jua kajipigania na si kwa sababu ya Mwandosya

Mkuu sema wew ndio unatumaini na Dr Tulia. Unazunguka zunguka nini. Unaogopa nini kusema hilo. Ndio mbinu zenu, mnaanza kampeni, au sio?
 
Pole sana kwa kuumizwa kwako. Inaonekana kwako upinzani sio watanzania. Na mtu akiwaunga mkono anakuwa mpungufu wa utanzania. Ama kweli Mungu ni mwaminifu kiasi ambacho ukiomba akupe akili za kipuuzi anakupa tu. Hana hiana kabisa
Kwa hiyo Sugu hakuwa kufungwa wa kisiasa kama wanavyodai. Hizo tuhuma tuhuma za kusema mkuu wa nchi alizisemea baa au kwenye mikutano wa kisiasa? Na je wakati anamtuhumu mfalme walikuwa na ugomvi wa binafsi au kwa mwamvuli wa kisiasa? Naomba jibu siyo matusi na kama huna jibu afadhali naomba usinijibu
 
KADA08: Kwa kweli wana CCM mnatukatisha tamaa sana kwa uelewa wenu finyu. Tunajiuliza inakuwaje tunawapa nchi watu wenye uelewa duni wa mambo kama huu? Kwa hiyo kwa akili yako unaamini kwamba hakimu aliyemsomea hukumu Mandela alisema " Unafungwa maisha kwa sababu ya siasa". Hivi kwa uelewa wako mtu kuwa mwanasiasa kama alivyokuwa mmandela
ni kosa la jinai? Hapo kilichofanyika ni kumtafutia kosa la jinai ili afungwe maana hakuna sheria itamfunga mtu eti kwa sababu ni mwanasiasa. Kwa kweli CCM ni adui wa maendeleo hasa ya kitaaluma na ufahamu wa mambo.
 
Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.
Kwa maneno yako mwenyewe Mwandosya yuko sahihi anaposema kuwa Sugu alikuwa ni mfungwa wa kisiasa kwa kuwa Makaburu nao walipomfunga Mandaela hawakusema kuwa wamemfunga kwa sababu za kisiasa walisema kuwa wamemfunga kama muharifu wa kosa la uhaini aliyetaka kuipindua serekali ya Makaburu lakini ukweli ulibaki palepale kuwa Mandela alifungwa kwa sababu za kisiasa.

Sawa na alivyofungwa Sugu kwa maana kuna watu wanatoa udenda kwa kulimendea Jimbo la Mbeya mjini utafikri hawajawahi kula tangu CCM izaliwe.
 
Kuna umri ukifika ukastaafu Ni vizuri kuendelea na Mambo mengine Kama kulea wewajukuu nk sio kuendelea na Yale uliyostaafia .Mwandosya umri umeenda Bado anaota siasa na wazee wenzie akna Sumaye

Ni upumbavu wa hali ya juu mkuu kufikiria kuwa siasa haipaswi kufanywa na wazee. Wewe unasema wazee wasifanye siasa, mkulu kakataza vijana wa chuoni wasifanye siasa, ccm mnataka watu wepi na wa rika lipi wafanye siasa? Toaka lini siasa zikafanywa kwa kubagua umri?
 
Back
Top Bottom