Prof. Mark Mwandosya: Mchakato wa kumpata mgombea urais CCM uligubikwa na utata

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Baada ya kimya kirefu hatimaye leo aliyekuwa anawania kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mark Mwandosya amebainisha wazi kuwa mchakato wa kumteua Atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika ngazi ya urais uligubikwa na utata mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya chama hicho.

Aidha Prof. Mwandosya amekiri kufedheheshwa na hatua ya kamati ya maadili ya chama hicho kujivika madaraka ya kupanga na kuamua ni wakina nani wapelekwe halmashauri kuu ya chama hicho pasipo hata kusikiliza maoni yao kwa mashtaka waliyotumia kama vigezo vya kuwaengua.

Hata hivyo amesema kuwa kukata majina ya wagombea lilikuwa ni jukumu la kamati kuu ya chama hicho.
Hakika chama kimeyumba.

Prof. Mwandosya amenukuliwa akisema kuwa Magufuli haifahamu na haijui CCM kwa kuwa hajawai kuwa hata mjumbe wa tawi la CCM.

Aidha ameweka wazi kutoridhishwa na mchakato uliofanywa na Kamati Kuu kuipata tano bora na hatimae Magufuli.

Anasema kamati kuu haikuwa na mvuto kiasi kwamba Mwenyekiti J.Kikwete hakuwa anajiamini,alifika wakati ana-adress kwa mwenyekiti na kujishtukia "kumbe mwenyekiti ni mimi mwenyewe".

Profesa amesisitiza kuwa watu walikuja na majina mifukoni kwani majina yalivuja kabla hata vikao.
Waziri mwandamizi katika serikali J.K amemtuhumu bosi wake kuwa alikuwa na majina ya wagombea tano bora mfukoni mwake.

Rais Kikwete ndiye aliyeongoza kikao cha maadili cha CCM, kilichowakata akina EL, Mwanndosya, Pinda, Dr Bilal.

Chanzo: RFA, Habari magazetini
Leo ni siku inayofuatia jana, siku ambayo Ndugu yangu Edward Ngoyai Lowassa aliacha rasmi uanachama wa CCM na kupewa kadi ya uanachama wa Chadema. Si yeye tu bali alisindikizwa na mke wake mpendwa Mama Regina Lowassa.

Nilidhani leo mitandao yote ingesheni habari hiyo kubwa. Kumbe nami nimekuwa "staa" katika mitandao ya kijamii. Kuanzia asubuhi nimekuwa nikipokea na kujibu simu mbalimbali nikiulizwa maoni yangu kuhusu tukio la jana, kuhusu mchakato wa Dodoma uliomalizika hivi karibuni, na "habari" kubwa imekuwa Mwandosya, Mwapachu na ole Medeye wahamia Chadema!

Kuhusu Ndugu Lowassa kuhamia Chadema nionavyo mimi ni jambo la kawaida sana katika demokrasia ya vyama vingi.

Wanachama hutoka na kuingia karibu kila siku. Hivyo basi tukio la jana lisingegonga vichwa vya habari kama isingekuwa kwa umaarufu wa mhusika. Jambo la msingi kwa CCM ni kutafakari, bila ghadhabu, na kwa utulivu, ni sababu zipi za msingi zilizofanya hili jambo litokee?
Je tunaweza kujifunza lolote katika hili ili kukiimarisha Chama?

Tunaweza kuboresha nini katika taratibu na kanuni zetu?

Nimeulizwa pia kitendo cha Ndugu Lowassa kuhamia Chadema kina athari gani kwa CCM?

Pamoja na kutotokuwa msemaji rasmi wa Chama, tukio hili lina maslahi ya umma kwa ujumla hivyo kukwepa kujibu hakusaidii. Siasa ni takwimu, hasa tunapoelekea Oktoba. Kwa mantiki hiyo mtu mmoja kukihama Chama kuna maana kura moja iliyopungua.

Kwa kuwa haiwezekani kuirudisha, basi changamoto ni kuwa na mkakati wa kutafuta kura ya kufidia, kuzuia kupotea kwa kura nyingine, na kuongeza idadi ya wanaoingia ili iwe kubwa kuliko ile ya wanaotoka.

Msaafu wa dini unasema mchungaji bora ni yule anayeweza kuwaacha kondoo wake tisini na tisa walio salama ili amtafute yule mmoja aliyepotea! Suala la kujiuliza katika mazingira ya yaliyotokea ni je tulikuwa wachungaji bora?

Nadhani moja ya mambo ya msingi CCM itabidi tulitafakari kuhusiana na mchakato wa kumpata mgombea wetu kwa nafasi ya urais ni je tunamtafuta mwanachama ambaye atakuwa Rais? Je tunamtafuta mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama? Au tunamtafuta mtu atakayekuwa Rais na Waziri Mkuu?

Vigezo vya kumtafuta mtu huyo vinapishana kama ambavyo orodha wa wenye nia au mifumo ya kumpata itapishana. Naamini tungelitafakari haya yote huenda tusingefika hapa tulipo. Lakini Taifa ni kubwa kuliko sisi watu na uhai wake ni mpaka "kiama cha wafu".

Tujadili masuala haya na mengine muhimu, kwa ujasiri, uwazi na ukweli.

Nahitimisha kwa kujibu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na watu wengi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari kuhusu Mwandosya kuhama kwenda Chadema.

Misingi iliyojengwa na waasisi wa Chama, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume naendelea kuamini bado ni sahihi. Ndiyo iliyotuletea heshima kubwa kama Taifa.

Kama tumeyumba turudi katika misingi. Itikadi ya Chama inajengwa juu ya misingi hiyo. Hivyo basi kwangu mimi
Ilihali misingi ipo, na imara, nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM ili kwa pamoja na wanachama wenzangu tuendelee kulijenga Taifa juu ya misingi hiyo, kila wakati tukikumbuka kile alichotuasa Baba wa Taifa, Tujisahihishe!

Na Profesa Mark Mwandosya
 
Alikaa siku ngapi Dodoma??!!!
Alichukua posho baada ya kugundua hayo madudu??!!

Katika maambo yooote hili kaliona lina utata??!! Utata uko katika mambo mengi makubwa sana yenye athari za maisha ya wananchi kila siku. . . . . aaanze huko kama mzalendo otherwise ya chama chao apeleke hukohuko chamani. . . .

Namuheshimu sana huyu mzee sidhani kama ataingia kwenye maneno ambayo yatamvunjia heshima mwishoni kiasi hiki. . . . . .
 
Mkuu taarifa hiyo ipo na clip zinazunguka whatsap
mzee amefunguka..
 
Alikaa siku ngapi Dodoma??!!!
Alichukua posho baada ya kugundua hayo madudu??!!

Katika maambo yooote hili kaliona lina utata??!! Utata uko katika mambo mengi makubwa sana yenye athari za maisha ya wananchi kila siku. . . . . aaanze huko kama mzalendo otherwise ya chama chao apeleke hukohuko chamani. . . .

Namuheshimu sana huyu mzee sidhani kama ataingia kwenye maneno ambayo yatamvunjia heshima mwishoni kiasi hiki. . . . . .

Hutaamini Utakaposikia Kavua Gamba na kuvaa Gwanda hawa wazee hawana cha kupoteza kwa sasa
 
Hutaamini Utakaposikia Kavua Gamba na kuvaa Gwanda hawa wazee hawana cha kupoteza kwa sasa

Itakuwa sawa tu ila kuhama sababu kakatwa ndio kitu inanisababisha niwachukulie kama watu wengine tu japo wanastahili heshima sana, pia ntamshukuru akifanya hivyo ili kuwe na conflict zaid na zaid ambazo ndio engines for a real change. . . .
 
Alikaa siku ngapi Dodoma??!!!
Alichukua posho baada ya kugundua hayo madudu??!!

Katika maambo yooote hili kaliona lina utata??!! Utata uko katika mambo mengi makubwa sana yenye athari za maisha ya wananchi kila siku. . . . . aaanze huko kama mzalendo otherwise ya chama chao apeleke hukohuko chamani. . . .

Namuheshimu sana huyu mzee sidhani kama ataingia kwenye maneno ambayo yatamvunjia heshima mwishoni kiasi hiki. . . . . .

Mkuu kudai haki yako au kulalamikia kuvunjwa kwa katiba, sheria na kanuni ilimradi haki yako ikiukwe ni kujivunjia heshima..?
 
Back
Top Bottom