Prof. Lipumba: Kusiwe na upendeleo wala uonevu kwenye uwanja wa siasa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema Baraza Kuu la Chama hicho limetoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Uongozi wake kuheshimu Sheria zinazoruhusu kufanyika mikutano ya hadhara na maandamano halali

Chama hicho kimeutaka Uongozi huo kuheshimu Sheria za Nchi ikiwa ni pamoja na kutoa usawa kwa Vyama vyote bila upendeleo wala uonevu katika uwanja wa kisiasa

Prof. Lipumba amesema, "CUF inaahidi kutoa ushirikiano muda wowote ambapo Nchi inaongozwa kikatiba na kisheria"
 
Kama alikuwa anataka usawa ilikuwaje akaunga mkono juhudi akalamba bilioni 3 za Meko?
Hata yule alielamba hela za Lowasa kwa masharti ya kumwaachia agombee uraisi kupitia chama chake, anafaa kubeba lawama. Kwa tamaa zake amesababisha chama kimerudi hatua elfu 1 nyuma.

By the way wanasiasa wote wa upinzani ni wachumia matumbo yao na familia zao.
 
Back
Top Bottom