CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
NICHAGUENI NIWE RAIS WA NCHI HII ILI NIWEZE KUTOKOMEZA NJAA KWA WOTE NA KUHAKIKISHA LISHE BORA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO "PROF.LIPUMBA"ILOLANGULU AKIPITA KUSALIMIA.
Nitahakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na uwezo au kuwezeshwa kupata milo mitatu kwa siku. Hatua za makusudi zitachukuliwa kuhakikisha kuwa kinamama wajawazito na watoto wachanga wanapata lishe bora itakayowasaidia watoto kujengeka vizuri katika viungo vya mwili, kinga ya mwili na ubongo, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujielimisha na kujiendeleza.