mcubic unadhani tatizo letu kama taifa ni "ukemeaji" wa masuala ya Rushwa? Tatizo letu ni dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa. Na rushwa ya tanzania ni ya kimfumo bila ya kuufumua huo mfumo tutaishia kuwa na matamko yasiyoisha na kuoneana bila ya sababu. Agenda dhidi ya ufisadi CHADEMA walikuwa wanaifanya kuwa ni ya taifa nyie mmeigeuza kuwa ilikuwa ni ya CHADEMA. Aibu ilioje!!
Mwambieni akiwa muongo asiwe msahaulifu. Clip za mapokezi ya Lowasa Ukawa zinaonyesha ushiriki wake ila lililomuuma ni kule kuenguliwa katika kazi yake ya kudumu ya " Mgombea Urais"
Wakati akiongea kupitia AzamTwo Television, Prof. Lipumba amesikika akisema, CHADEMA kimepoteza dira ya kisiasa kutokana na mtafaruku uliojitokeza ndani ya UKAWA baada ya kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea Urais wa Tanzania.
Prof. Lipumba amesema, ''Sisi ndani ya CUF tunaweza kukijenga vizuri chama chetu kwa sababu msingi wetu ni kusimamia haki kwa wote lakini wenzetu wa CHADEMA wamepoteza dira kwa sababu itakuwa ni vigumu kuzungumzia suala la mapambano dhidi ya ufisadi''.
''Msingi wa sera zetu ni Haki Sawa Kwa Wote, Rais Magufuli anasema HapaKaziTu na sisi tunasema Hapa ni Haki Tu'' Alisema.
Aliendelea kusema, ''Tuna mahala pazuri pa kuanzia, kutazama namna ya kuikosoa serikali katika kutekeleza hizi sera za HapaKaziTu, Je tunalinda haki za kila mmoja wetu, tunafuata utaratibu mzuri wa sheria''
Alimalizia kwa kusema, ''wenzetu CHADEMA wamepoteza dira''.
VIDEO:
Allen Kilewella
Kwa hiyo ajenda yenu ni ipi?
CCM wanakemea ufisadi.....mmeporwa hoja yenu.
ACT- utu, miiko na uzalendo
CUF- haki sawa kwa wote....hapa haki tu.
Mimi ningetafsiri hivi "Mfumo ni Mbinu yakinifu, utaratibu na kanuni zilizobuniwa kufanikisha shughuli fulani, kutimiza wajibu, au kutatua tatizo" Kwa maana hii ni lazima kwanza mfumo ubuniwe, pia ndani yake kuwe na utaratibu wakufuatwa na kanuni za kuzingatia katika kutatua tatizo. Kwa tafsiri hii yangu sidhani kama kushughulika na watu ni kushughulika na mfumo!
"A set of detailed methods, procedures and routines created to carry out a specific activity, perform a duty, or solve a problem"
Kwa tafsiri isiyo rasmi mfumo ni : "Aina ya mbinu mbalimbali zinazofanywa khaua kwa hatua na mara kwa mara katika shughuli fulani, kufanya kazi au kutatua matatizo"
Prof. Lipumba bado ni mwanachama wa CUF.Lipumba hana hata aibu. Anadai sisi CUF ................... CUF ipi wakati alijitoa kabla ya kupigwa boot!!
Dhambi ya usaliti inamtesa ............ hata Yuda alitaka kurudisha vile vipande 30 vya sarafu ili jamaa wamuachie Yesu lakini ilikuwa too late ............ mwisho wa siku akajinyonga!!!
Na wewe unatetea udikteta wa MboweHuku ni sawa na kumchikoza gwajima sisi sio watu wa mchezo mcheO
Inasikitisha chadema kuuzwa kwa mafisadiPROF LIPUMBA yupo sahihi SLAA alipigania chama sana ila alilipwa mabaya ila ipo siku chadema watajuta dhambi walio ifanya itawarudia
Kati ya Lipumba na Mbowe nani yuko bize kupokea majizi na wauza madawa ya kulevya??Lipumba anavyouharibu upinzani kwa uswahili na unafki hawezi kuinyooshea mkono CDM . Ametumika vibaya na hata akiachiwa hiyo Cuf haiwezi tena kusimama dhidi ya wanaomlipa(CCM)
Awaache CDM wafanye yao naye aendelee kuichuuza CUF huko Lumumba
Tukubal tukatae, chadema tulibugi kumtema dr slaa kisa lowasaLipumba anavyouharibu upinzani kwa uswahili na unafki hawezi kuinyooshea mkono CDM . Ametumika vibaya na hata akiachiwa hiyo Cuf haiwezi tena kusimama dhidi ya wanaomlipa(CCM)
Awaache CDM wafanye yao naye aendelee kuichuuza CUF huko Lumumba