Prof. Lipumba: CHADEMA wamepoteza dira

Prof. Lipumba: CHADEMA wamepoteza dira

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,051
Wakati akiongea kupitia AzamTwo Television, Prof. Lipumba amesikika akisema, CHADEMA kimepoteza dira ya kisiasa kutokana na mtafaruku uliojitokeza ndani ya UKAWA baada ya kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea Urais wa Tanzania.

Prof. Lipumba amesema, ''Sisi ndani ya CUF tunaweza kukijenga vizuri chama chetu kwa sababu msingi wetu ni kusimamia haki kwa wote lakini wenzetu wa CHADEMA wamepoteza dira kwa sababu itakuwa ni vigumu kuzungumzia suala la mapambano dhidi ya ufisadi''.

''Msingi wa sera zetu ni Haki Sawa Kwa Wote, Rais Magufuli anasema HapaKaziTu na sisi tunasema Hapa ni Haki Tu'' Alisema.

Aliendelea kusema, ''Tuna mahala pazuri pa kuanzia, kutazama namna ya kuikosoa serikali katika kutekeleza hizi sera za HapaKaziTu, Je tunalinda haki za kila mmoja wetu, tunafuata utaratibu mzuri wa sheria''

Alimalizia kwa kusema, ''wenzetu CHADEMA wamepoteza dira''.

VIDEO:
 
Last edited by a moderator:
Lipumba ajili zilisha isha sasa zimebaki pumba tuuuuuu
 
Wakati mwingine hawa wazee wapime kama bado vichwa vyao vinafanya kazi sawa sawa. Mchakato wakumpokea lowasa waliufanya na yeye akiwepo na alimsifia sana sasa kipi tena kinamfanya ageuke na kuwa ndumilakuwili. Ni aibu sana kutumia mdomo wako kuongea huku ukitumia akili ya mtu mwingine
 
Barikiwa sana mkuu nimecheka mpaka basi
 
Wakati mwingine hawa wazee wapime kama bado vichwa vyao vinafanya kazi sawa sawa. Mchakato wakumpokea lowasa waliufanya na yeye akiwepo na alimsifia sana sasa kipi tena kinamfanya ageuke na kuwa ndumilakuwili. Ni aibu sana kutumia mdomo wako kuongea huku ukitumia akili ya mtu mwingine

mwache amlambe miguu jpm 2..amsifie saaana,lkn uongozi hapewi.zile hela zimeisha kwan??
 
MsemajiUkweli
Yuda huyu si wa kuchekea hata kidogo, anajipendekeza kwa viongozi wa CUF apewe ulaji! Tangu awe Mgombea CUF haijawahi kua na viti vingi kama mwaka huu. Huyu kupata uongozi labda Maalim Seif aondoke CUF, Katika watu waliomuudhi sana maalim Seif ni huyu msaliti.yaan wenzi wako katika kipindi kigumu wewe unawakimbia!
 
Last edited by a moderator:
barikiwa sana mkuu nimecheka mpaka basi
hawa wazee wanataka kutugeuza sisi kama shimo la kumwagia ujinga wao leo wanasimamia hiki kesho wanasimamia kitu kingine. Hwaeleweki kama mavi ya kuku leo meupe kesho ya njano siku nyingine meusi. Shida tupu. Na hizi media na zenyewe sijui hazijaliona hili?
 
Wakati mwingine hawa wazee wapime kama bado vichwa vyao vinafanya kazi sawa sawa. Mchakato wakumpokea lowasa waliufanya na yeye akiwepo na alimsifia sana sasa kipi tena kinamfanya ageuke na kuwa ndumilakuwili. Ni aibu sana kutumia mdomo wako kuongea huku ukitumia akili ya mtu mwingine

ama kweli nyani haoni kundule., leo hii Prof Lipumba mnamwita ndumilakuwili? Je chadema tuwaite jina gani? Maana wao walituhubiria habari za ufisadi kuhusu Lowassa for almost miaka 8 leo hii mkageuka ghafla na kutuambia anafaa na ni msafi.,!
ama kweli Mkapa hakukosea kuita malofa
 
MsemajiUkweli

Nadhani akinyamaza sisi wengine ambao tumeendelea kumuheshimu tutaendelea kufanya hivyo .Yeye na CUF ipi? Mtu muungwana huheshimu maamuzi ya kikatiba kupitia vyombo vya juu vya vyama vyetu vinapofanya maamuzi .
 
Last edited by a moderator:
ama kweli nyani haoni kundule., leo hii prof lipumba mnamwita ndumilakuwili? Je chadema tuwaite jina gani? Maana wao walituhubiria habari za ufisadi kuhusu lowassa for almost miaka 8 leo hii mkageuka ghafla na kutuambia anafaa na ni msafi.,!
Ama kweli mkapa hakukosea kuita malofa
you are using an invalid proposition to justify an invalid proposition. Chadema kumpokea lowassa kwa kutumia vikao halali vya chama haimanishi watu wakubali porojo zinazotolewa na wanasiasa wachovu.
Lipumba anapaswa ajiheshimu naamini na wengine tutamheshimu pia
 
Ngoja wakunywee viroba waje
Sijawahi kunywa pombe maishani mwangu. Jee nikimpinga Lipumba nitakuwa nimekunywa kiroba? Ujinga wenu ndiyo mauti ya taifa, kwani kwa bahati mbaya sana chama chenu ndiyo kinaongoza Serikali ya taifa letu kwa sasa! Ni kama laana kuwa na CCM Madarakani.

Hapo wengine tunajua Lipumba anazungumzia nini na nini kitafuatia baada ya hapo. kwa taarifa yako Lipumba atateuliwa na Magufuli kuwa Mbunge, halafu yeye kwa ujinga wake anatengeneza mazingira kwamba CUF ndiyo yenye uhalali wa kushutumu serikali kwa hivyo ndiyo yenye haki ya kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na yeye ndiye anatamani kuwa kiongozi wake. CCM imekuja na mkakati mpya wa kuisambaratisha UKAWA.

Kama Lipumba ni mtu anayeaminika ndani ya chama chake kwa nini alishindwa kukataa muungano wa UKAWA kumpokea Lowassa. Falsafa haijengwi kwa tukio bali kwa jinsi tukio linavyotafsiriwa na anayeliona, kwa maana nyingine Lipumba analiona tukio la CHADEMA kumpokea Lowassa kama vile vile anavyoliona Kinana au Slaa. Ni ajabu sana mitizamo ya watu hawa watatu kwa sasa kufanana kama watoto mapacha wanaotoka kwenye mfuko mmoja wa uzazi.

Hoja yangu hapa ni kwamba ukimkuta Msabato au Muislam ukawauliza Nguruwe ni Nyama haramu au halali, bila shaka watakwambia ni haramu, dini mbili tofauti lakini mtazamo mmoja. Na ukikutana na Mkatoliki au na Mtu anayeabudu mzimu bila shaka kwao nguruwe ni nyama halali kabisa tena inanoga kupita nyama zote. Hawa nao dini mbili tofauti toka kwenye misingi isiyofanana kabisa lakini wana mtazamo mmoja!

Kufanana kwa mitazamo hakuji kiholela bali kunatokana na misingi mahsusi ambayo hujengwa juu ya falsafa. CCM wanaigopa UKAWA ikiwa na Lowassa na Lipumba naye UKAWA ikiwa na Lowassa imemtumbukia nyongo. Wote Lipumba na CCM wanahofia nafasi zao kisiasa kwa uwepo wa Lowassa.

Kuna swali Lipumba ameulizwa mara nyingi kuwa kama Mwenyekiti amefanya nini kukijenga chama kabla ya "Fisadi" Lowassa kukaribishwa UKAWA mpaka sasa hana jibu, na wala hatapata jibu kwani anakodokolezea (CCM) nao hawana jibu au wanajua wao ndiyo chanzo cha CUF kuwa hivi ikiwa mikononi mwa Lipumba hivyo hawatamwambia jibu ni nini!
 
Lipumba hana hata aibu. Anadai sisi CUF ................... CUF ipi wakati alijitoa kabla ya kupigwa boot!!

Dhambi ya usaliti inamtesa ............ hata Yuda alitaka kurudisha vile vipande 30 vya sarafu ili jamaa wamuachie Yesu lakini ilikuwa too late ............ mwisho wa siku akajinyonga!!!
 
Wakati mwingine hawa wazee wapime kama bado vichwa vyao vinafanya kazi sawa sawa. Mchakato wakumpokea lowasa waliufanya na yeye akiwepo na alimsifia sana sasa kipi tena kinamfanya ageuke na kuwa ndumilakuwili. Ni aibu sana kutumia mdomo wako kuongea huku ukitumia akili ya mtu mwingine

Weka hiyo clip hapa ...
 
Lakini alishakiri kuwa pamoja na yote yy hakuridhika na ndio maana alijitoa uli kujiepusha na kumnadi mtuhumiwa wa Ufisadi!
 
Back
Top Bottom