garikicah
Member
- Oct 29, 2010
- 71
- 18
Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...
Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...
Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao
Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi
Wakati maalimu ana deal na mutungi professor huku Yeye anasafisha, da kazi kwelikweli