Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...

Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...

Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao

Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi

Wakati maalimu ana deal na mutungi professor huku Yeye anasafisha, da kazi kwelikweli
 
Daah uchaguz wa mameya dar CCM wanabeba mameya wote....lakin inakuwaje mtu alirjizuru kihalali msajili anasema stil ni kiongoz halali!!!!!
 
But, yawezekana napata shida kuunganisha dots. Hivi ni kweli CUF ndiyo great threat kwa CCM? I'm just curious, I guess there is something wrong within CUF itself, I'm not happy with what happens to CUF but I think the party members should open up the box and see what eats them inside
Not a direct threat to CCM but with it wthin ukawa is a big threat......there may be problems within cuf itself but ccm is taking advantage of the situation
 
AF PICHA LIKIISHA HAPO NA DR NAYE ANARUDI KWENYE KITI CHAKE.....ILI WAMALIZANE WAO KWA WAO
 
CUF kurudi kwa lipumba ndio inajimaliza. maamuzi ya wanachma hayaheshimiwi, msajili wa vyama ndio ana dictate nani awe mwenyekiti! AIBU
Siyo kwamba Waarabu wamegonga mwamba? Walimuweka Lipumba wakidhani atakubali kuwa figurehead. Walipotaka kuvunja Muungano ili wagawane mbao ili Waarabu wachukue Zanzibar na mafisadi wa UKAWA wachukue Tanganyika kwa hila, Professor na wazalendo wenzakei Wabunge wa Tabora, Mtwara na Tanga wakakataa kusaliti nchi. Mwacheni Professor apange safu - uinzani imara ni utawala imara. Hiki chama ni cha Mapalala mtu ws Bara, lakini Waarabu wakakiteka nyara kama utumwa.
 
Nalikumbuka swali lako... na wakati watu tunaelezea uhalisia, wengine walitukejeli! Leo hii inashangaza kuona mtu asiye na wafuasi lakini bado ameweza kuingia HQ! Na tukiweka unafiki pembeni, hata hapa JF tunaowaona wapo sana upande wa akina Mtatiro ni watu wa CHADEMA ndio wengi kuliko CUF!
Huu ni ukweli
 
Kama mchezo mnaotaka kuucheza Lumumba ni kumtumia huyu pro wenu kumhujumu Maalim,basi mnakosea sana.Hili jipu mnalitengeneza nawaambieni!Likitumbuka mwili mzima utaugua.
 
Hahahahaa The Boss huu mchezo hauhitaji hasira.. wakina Mtatiro badala ya kukaa pembeni ndio kwanza amehamia Zanzibar kutumika vizuri na Sefu...

Kwa hiyo hata zile barua walizo kuwa wana tuma UN prof anaweza sema ni batili kwakuwa haku sign yeye? Da siasa ni mchezo mchafu.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom