Prof.Lipumba Aula Madola

Ni Mistake I admit, Mods, nawataka radhi kwanza halafu naomba mturekebishie.
Ni kweli Mkuu mi mshabiki wa Man Utd...ukiachilia kwa keyboard...leo sijaongea na mtu kwa kauli toka asubuhi.

...:D pole sana mkuu, ndio ukubwa huo.
 
Wewe hujanielewa, labda uende summer school.
Labda,lakini nimetangulia kusema "..kwa kesi ya Prof.Lipumba...", kama kwa mimi Mkuu mi sina haja ya position hata ya Mw'kiti wa mtaa bila kupingwa...presha ya nini...na kuota mvi mapema...wanatafuta nafasi ndo wanauwezo hao ww mtazamo wako tu ndo unawaona hawana uwezo.
Lipumba yupi huyo ni mwadilifu? Yaani kuwa mmoja wa kiranja/mamonita wa darasa, basi ashakuwa mwadilifu!
Watanzania wapo zaidi ya Milioni 30,Mlimani pale pana Phd holders zaidi ya 300...ukijumlisha na kutoa...wazungu wenye vichwa vyao vyenye almost 0% ya ku-think kifisadi fisadi...wameona Prof.I.H.Lipumba, ndiye anafaa kufanya kazi na timu teule ya madola ya kuangalia kama uchaguzi wa Msumbiji ni huru na haki...Mkuu, katika kazi kama hiyo panahitaji mtu muadilifu wa kutazama kama kweli haki inatendeka si yeyote...mbona hawajukufata ww?
Mtakumbuka Prof. R.Mukandara, nasikia ni VC wa UDSM siku hizi, alikuja na timu yake ya waangalizi katika moja ya chaguzi za rais Zanzibar,kule...licha ya ushenzi uliofanywa na chama tawala kuiba kura na kuvuraga uchaguzi kwa madhumuni ya kulazimisha chama tawala kushinda...Mukandara na timu yake walikuja na ripoti ya kudai kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki...kwa hiyo Karume ni rais halali. Yaani msomi mtu mzima wa heshima yake,anakuwa ovyo kwa kuendekeza ukereketwa mbele badala ya haki na ukweli kama mtaalamu...failure kabisa na ndo Prof.yule! sasa kwanini jumuiya ya madola wasimchakue Lipumba ambaye anaongoza chama ambacho siku zote kipo mstari wa mbele kudai haki na uadilifu, na kwa vitendo wanaonyesha hivyo?
Chama ambacho hata falsafa yake ni HAKI SAWA KWA WOTE, hii ni dhana nzima ya uadilifu, na kama kiongozi anapatiakana kutoka chama chenye falsafa na dhana kama hii,huyo anatosha na anafaa kusimamia zoezi linalotakiwa kufanyika kwa uhuru na haki kama uchaguzi...hata ugomvi wa kuku anaweza akausimamia kwa haki...kwanini asiaminiwe...kwanini wasichaguliwe Mprof. wengine...hakuna baada ya kuondoka Marehem Prof.Haroub Othman waliobakia (ukiondoa Prof.Lipumba) ni kama akina Rwekaza Mukandara...ushabiki na ukereketwa mbele...haki na uadilifu nyumba ya visogo vyao.
 
Back
Top Bottom