Prof.Lipumba Aula Madola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof.Lipumba Aula Madola

Discussion in 'Entertainment' started by Junius, Oct 26, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF,Prof. Ibrahim Lipumba ameteuliuwa na Jumuiya ya Madola kushiriki katika timu ya waangalizi wa uchaguzi Mkuu wa nchini Msumbiji.
  Akiongea na Idhaa ya Kiswahili ya BBC London, Prof.Lipumba amesema hiyo ni heshima kubwa kwake na anakwenda huko si kama Mw'kiti wa CUF bali mtu muhimu aliyeaminiwa kushiriki katika jopo hilo la waangalizi wa madola.
  Katika jopo hilo la waangalizi wa uchaguzi, aliyekuwa rais wa Sierra Leon Bw.Tejan Kabba atakuwa Mw'kiti wake.

  SOURCE:BBC SWAHILI SERVICE
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  waadilifu wanajuulikana bwana we!
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  "Aula?"

  Ushakuwa mradi tena?
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WAKATI HUO HUO.  [​IMG]

  Wagombea kiti cha urais nchini Msumbiji wamefanya kampeni zao za mwisho kabla ya upigaji kura siku ya Jumatano. Wagombea wote watatu walimaliza kampeni zao Jumapili, wakiwasihi wafuasi wao kujitokeza kupiga kura.

  Uchaguzi unatarajiwa kumpatia ushindi Rais Armando Guebuza, ambaye anakabiliana na mgawanyiko wa upinzani. Wapinzani wake ni Afonso Dhlakama, kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Renamo, na Daviz Simango, mwanzilishi wa chama kilichojitenga cha Democratic Movement of Mozambique.
  Simango alijitoa kutoka chama cha Renamo mwanzoni mwa mwaka huu, na kuwachukua maafisa wakuu wa upinzani. Upigaji kura wa Jumatano utachagua pia viongozi wa bunge na majimbo.

  Chama tawala cha Frelimo kimeongoza Msumbiji tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ureno mwaka wa 1975.

  SOURCE:VOA SWAHILI SERVICE
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sasa wewe unaona vipi hapo?
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa wabongo ishakuwa dili hilo!

  Mitazamo ya aina hii ndiyo iliyopelekea taifa letu kuwa hapa tulipo! Kila mmoja anapogombea uongozi wowote na katika level yoyote kabla ya kufikiria majukumu muhimu katika post /cheo kile, anafikiria zaidi maslahi yake binafsi!
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa mtu mwenye mawazo kama hayo anaweza kulalamikia ufisadi? Inaonekana huyu ana endorse ufisadi na yeye anatafuta channel tu, kama si fisadi tayari.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mnatabu kweli mtu akipata kadili kama haka kakuengeza dolari na uzoefu inakuwa kelele, najuwa athari za kunyanyaswa na wezi na mafisadi zinakupelekeeni muwone vifursa fulani fulani kama hivi,mnavionea wivu tu...au kwakuwa hawakuchaguliwa mnaowataka nyinyi?
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Lipumba anaenda kufanya kazi priceless katika kuongeza democracy Afrika, wewe na mwazo yako finyu yasiyoona zaidi ya pua yako all you can see ni ku prostitute hii kazi kwa upeo mdogo wa kutumia lenzi ya fedha.

  Ikiwa vyote unavyofikiri vinaanza na kuishia katika fedha utasemaje kwamba huwezi kuuza demokrasia kifisadi kwa vipande arobaini vya fedha?
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ha ha ha ha ha !!!
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ha ha ha ha ha !!!
  Kwani aliyesema ishakuwa dili ni nani si wewe?
  Mimi niliposema aula nilimaanisha fursa na heshima ya kutambulika na dunia na ukisoma stori vizuri Prof.Lipumba anasema mwenyewe...na ametumia neno "prominent person" kama kuwa heshima yake imetambulika na dunia inajuwa yeye ni nani. Hizo habari za dili na fedha zimetoka kwako kwa hivyo, nani anaakili na mawazo finyu?
   
 12. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hongera lipumba!nafasi ya kujifunza na kutengeneza pesa profesa.safi sana...
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wabongo tunaangalia "kuula" tu.

  Hatuoni responsibility, hatuoni mzigo, hatuoni duty kubwa. Ndiyo maana mkaambiwa msikimbilie positions, ni mizigo, migogoro.

  Sisi tunachekelea "kaula".

  Ndiyo maana Socrates alisema wenye uwezo hawafanyi siasa, wanaofanya siasa hawana uwezo.

  Sie tumebaki "aula"! Njaa yetu inachoona ni kula tu.
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...sasa hii nayo inahusiana vipi kwenye jukwaa la michezo hapa?
  Nyie washabiki wa Manure mkifungwa sijui mkoje!
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni Mistake I admit, Mods, nawataka radhi kwanza halafu naomba mturekebishie.
  Ni kweli Mkuu mi mshabiki wa Man Utd...ukiachilia kwa keyboard...leo sijaongea na mtu kwa kauli toka asubuhi.
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu, kwa kesi ya Prof.Lipumba namtetea hapa...hajakimbilia hiyo nafasi...ni wazungu wenyewe...wameangalia vichwa milioni 30 vya Watanzania, wakaona kichwa kimoja tu ndo kinafaa kwa kazi zao,miongoni mwa vichwa vyote vya Watanzania,ukichanganya na Mprof. wote waliomo nchini...kimeonekana kichwa cha Prof.Lipumba ndo kinafaa zaidi ya vyote..nasisitiza kwa heshima hiyo, kutoka kwa jumuiya inayokusanya nchi kibao...ni wazi kuwa Prof. Lipumba ni maarufu sana kuliko Watanzania wengi tu wanaoonekana maarufu...kwa hiyo kaula, kama kwenu kuula lazima iwe pesa...basi mnafikiri kifisadi fisadi...I don't put blame on you...its the system which raise you.
   
 17. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Ndio hapo nimebaki hoi bin taaban!
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe hujanielewa, labda uende summer school.

  Sijasema prof. Lipumba kakimbilia position, nimesema hii mentality yako ya kushabikia positions na exclamations za "kaula" ndiyo inayokimbilia position.

  Wewe kwa kukosa integrity sasa hivi hata bila uwezo unaweza kukubali kuwa "Secretary General wa UN" apamoja na migogoro yote na politics zote zilizopo pale, kisa tu utaona "unaula"

  Au siyo?

  Halafu unaweza kumlaumu Kikwete kwamba ametaka urais bila ya kuwa na uwezo? Ukiangalia kwa nini alitaka urais wakati uwezo wake mdogo, unaona chanzo ni hii hii mentality ya "kuula".
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Lipumba yupi huyo ni mwadilifu? Yaani kuwa mmoja wa kiranja/mamonita wa darasa, basi ashakuwa mwadilifu!

   
 20. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kujifunza pengine ni sawa. Kutengeneza pesa? No ni kumdhalilisha. Sidhani ameishiwa kiasi hicho
   
Loading...