Tunkamanin
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 955
- 866
Nikirejea kwenye bunge la katiba, nadhani ndiye alikuwa mwanasiasa mahili kwa kujenga hoja za kutetea katiba pendekezwa ya wananchi, Umoja wa katiba ya wananchi ukawa umezaliwa kwa hoja zake, japo baada ya wateule kutengana wabakiaji wanautumia umoja huo kama mtaji wa kisiasa, hoja zote za kutetea katiba zimekufa, imebaki kumletea fitna prof, na maneno ya matusi na kejeli kwake, mlango huu wa shari umefunguliwa na mtu wake wa karibu mno, anaombwa kila siku aufunge mlango huo, lakini amekua msusuavu wa moyo. prof anaitwa msaliti, anatumika nk lakini nimjuavyo msomi huyu ni mtu mwenye msimamo thabiti, na alianza hivyo muda mwingi tu na mkashangilia, ila alipojitoa kwa jambo ambalo mlikua na maslahi nalo mkaanza kurusha mikuki yenu, ama kweli......Ombi langu kwenu, tusiwe wasahaulifu wa haraka kiasi hiki, na tusipende kukubali ubora wa kitu baada ya kuwa kimeshaondoka au hakipo tena katika himaya yetu. Majuto mjukuu..........