Prof. Lipumba amdai IGP Sirro saa yake

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
2,256
2,000
Yaana mafaraka ni sawa na madawa ya kulevya.
Mama Samia anaona jinsi mwenda kuzimu anavyo laumiwa na kusutwa kwa aliyo watendea watu.
Lakini bado haoni maana ya kujiandalia maisha mema ya baadae.. Bado nae ana fuata ujinga wa mwenda kuzimu.
Ndipo ninapo amni ni vugumu sana hawa watu kuionja pepo.
Tatizo nadhani waliomuweka wanamtisha
 

Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
3,417
2,000
View attachment 1984094
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGPSimon Sirro kuitafuta saa yake ya mkononi aliyonyang'anywana askari wake wakati wa mvutano ulioibuka karibuni.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho na wananchi mkoani Tabora, Lipumba amelishutumu jeshi hilo kwa kuvuruga shughuli za chama hicho zilizopangwa kufanyika, ikiwemo uziunduzi wa mashina katika kata za Mbugani na Mapambano pamoja na kuchangia damu.

Amesema polisiwaliwazuia kufanyia shughuli hiyo kwenye ofisi zao, badala yake wafanyie kwenye ukumbi, na kwamba mwishoni walifanikiwa kuchangia chupa 20.

Amesema atamshauri Rais atembee kwenye kauli zake zakutetea demokrasia ya kweli, yenye msingi wa maendeleo pamoja na kulinda heshima na utu wa Watanzania.

Ameongeza kuwa haki ni muhimu kwani itawezesha wananchi kufanya kazi kwa uhuru, hivyo kujiletea maendeleo na kwamba Rais atakumbukwa na kujipatia heshima kutokana na kusimamia kauli yake, na kwamba akija kugombea tena kazi inakuwa nyepesi.

Lipumba akumbushwe kwamba wepesi wa kazi ya kugombea kwa Rais wa JMT hautegemei wananchi wanamuonaje au wanamchukuliaje bali yote yanategemea ufanisi wa kazi za akina Sirro & co.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom