Prof. Lipumba ajiuzulu Uenyekiti CUF

Prof. Lipumba ajiuzulu Uenyekiti CUF

Status
Not open for further replies.
Wakati Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia akiudanganya umma kwamba Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba anashughulikia kesi yake mahakamani na huenda ndio sababu ya kutohudhuria mkutano wa leo, imebainika tayari Lipumba hayupo tena CUF.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zinasema, Lipumba amekusanya kila kitu kinachomuhusu kwenye ofisi za chama hicho na kuondoka. Inaelezwa, wakati anaondoka Lipumba alitoa maneno makali dhidi ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif na kumuita mhuni huku akisisitiza hawezi kufanya nae kazi.
Taarifa zaidi zinasema, Lipumba anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari wakati wowote kuanzia sasa kuelezea sakata hilo.

Seek psychiatric assistance! vinginevyo Milembe inakuita!
 
Pesa za ESCRO ndio kazi yake kwa wakati huu! Wananchi inabidi waamke. CCM isirudishwe madarakani kwa namna yoyote ile!
...pesa ya escrow itatumika kwa kila namna kuwarudisha ccm madarakani...In fact pesa ya escrow ndio imechangia kwa kiasi kikubwa kushusha thamani ya shilingi ya TZ...inaskitisha hili halizunumzwi laini ukweli ndo huo....yale mapesa tele yaliyosombwa kwa mabegi na viroba huko kwenye mabenki ya mkombozi na stanbic ndio yame saturate soko la pesa mtaani na hata kupunguza kiasi cha dola sokoni...Hii inflation ya shilingi ya TZ itaongezeka hadi mwisho wa uchaguzi.....maana sasa ndio wakati mapesa haya yatatumika haswa kununua kura....
 
Wakati Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia akiudanganya umma kwamba Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba anashughulikia kesi yake mahakamani na huenda ndio sababu ya kutohudhuria mkutano wa leo, imebainika tayari Lipumba hayupo tena CUF.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zinasema, Lipumba amekusanya kila kitu kinachomuhusu kwenye ofisi za chama hicho na kuondoka. Inaelezwa, wakati anaondoka Lipumba alitoa maneno makali dhidi ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif na kumuita mhuni huku akisisitiza hawezi kufanya nae kazi.
Taarifa zaidi zinasema, Lipumba anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari wakati wowote kuanzia sasa kuelezea sakata hilo.

Maalim Seif akanusha Lipumba kujiuzulu


Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amekanusha taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.

Amesema akiwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, hajapokea taarifa zozote za kujiuzulu kwa Prof. Lipumba, na kwamba hadi saa nne za usiku wa jana Jumatatu ya tarehe 03/08/2015, alikuwa na mazungumzo ya faragha na Prof. Lipumba na wala hajamzungumzia juu ya jambo hilo.
Maalim Seif ametoa taarifa hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakati akihutubia kwenye mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambao umewajumuisha pia viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.
Amesema kwa mujibu wa Katiba ya CUF, kiongozi yeyote wa Kitaifa wa Chama hicho iwapo ataamua kujiuzulu, anatakiwa kuiandikia barua mamlaka iliyomchagua ambayo ni Mkutano Mkuu wa Chama hicho, lakini akiwa katibu wa Mkutano huo, bado hajapokea taarifa hizo.
Amefahamisha kuwa gazeti lililochapisha taarifa hizo katika toleo lake la leo tarehe 4/8/2015 lilikuwa na malengo maalum ya kuvuruga Muungano wa vyama vinavyounda UKAWA, na kwamba malengo hayo hayatofanikiwa.
Katika hatua nyengine Mkutano Mkuu wa Chadema umempitisha kwa kauli moja Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho, na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF Mhe. Juma Duni Haji kuwa mgombea mwenza kupitia Chadema.
Mkutano huo pia umeridhia Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea pekee wa urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, kwa kuwakilisha vyama vinavyounda UKAWA ambavyo ni CUF, CHADEMA, NCCR MAGEUZI na NLD.
katika hatua nyengine Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amekubali kujiuzulu kwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 48 na kifungu 129 vya Katiba ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la kujiuzulu Mh. Juma Duni Haji, WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO kuanzia tarehe 01 Agosti, 2015.
 
Waandishi wa habari wameitwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari makao makuu ya CUF yaliyopo Buguruni, ambapo hawajatoa briefing ni kitu gani kitazungumziwa, ingawa tayari kwenye chumba chetu cha habari tumeambiwa kuna tetesi kuwa Profesa Lipumba anaweza kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uongozi ndani ya CUF.

Tutafahamu saa tano kamili mkutano ukianza.
 
Ngoja tuone na akijiuzulu itakuwa poa sana maana chama kimeshamezwa na Chadema.
 
Ajiuzulu tu huyu ndio alimsaidia jk 2010 kama alivyokiri mwenyewe mskitini.
 
Kama anajiuzulu asingewaita ofisini angetafuta sehemu nyingine. Kama waandishi wameitwa hapo ni kwa shughuli za kichama
 
Mtakufa mkipiga ramli.kuna mwenzenu aliitabiria chadema kufa lakini alishindwa kujua kuwa jina lake lingetupwa Dustbin kwenye mchujo.shame on animals
 
Lipumba inasemekana alichukua milioni 200 toka CCM ili avuruge ukawa..sasa naona zimemtokea puani ...atajiju sisi tumeshatangaza mgombea wa UKAWA na tunasonga mbele sasa
 
Kama anajiuzulu asingewaita ofisini angetafuta sehemu nyingine. Kama waandishi wameitwa hapo ni kwa shughuli za kichama

Mkuu kujiuzulu sio lazima kuwe kwa ubaya kama ilivyokuwa Slaa anaweza kuwa anapisha wengine lakini akaendelea kuunga mkono juhudi za UKAWA
 
Nauliza hivi kwasababu sijaona jambo lolote la maana wanalolifanya katika jamii zaidi ya kuwafanyia kampeni wagombea wa nafasi za urais kutoka vyama vyao. Je, huu ni wajibu wao kwa wananchi waliowaongoza au wanawajibika kwa vyama vyao tu? Ina maana kipindi cha uongozi wao waliwatumikia wanachama wa ccm tu na kuwabagua wasio ccm? Au kuna kitu gani wanakipigania kisijulikane kwa wengine? Hivi nchi ikipata shida ni nani wa kusimama kati ili kuleta suluhu? Ushauri wangu ni kuwa marais wastaafu wasiwe na upande wowote na ni bora wakae kimya na wabakie kuwa washauri na si wapiga kampeni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom