Prof. Kitila Mkumbo, umeanza kwa kuchemka

Prof. Kitila Mkumbo, umeanza kwa kuchemka

Kwa taarifa yako Wizara ya maji ndiyo wamiliki wa maji yote hapa nchini ,wizara ya kilimo haiwezi kuanzisha mradi wa umwagiliaji bila kibali cha wizara ya maji.
Halafu wizara yake inaitwa wizara ya maji na umwagiliaji unafikiri neno umwagiliaji limewekwa hapo kimakosa?

Kipi kinaanza Kilimo au umwagiliaji? ukiniambia kilimo basi hakutakiwa kuna na kipaumbele cha namna hiyo.. Lakini kwa nijuavyo, Kilimo huanza then consultation hufanywa kwa wana maji pale maji yanapohitajika. There4 umwagiliaji haufanyiki hewani lazima kuwe na kilimo kwanza na yeye hakutakiwa ku-stress katika kilimo rather upatikanaji wa maji safi na salama iliyo katika scope yake ya kazi. Anyway, most of leaders fails to realize their scope of work.
 
Prof. Kitila Mkumbo amesona PCB ila wakati anasoma education (yaani 2nd year wakati wa ku-specialize) ali-drop somo moja aka-major education ndo maana degree yake ya kwanza ni Bed (Science) na baadae aka-specialize kwenye Psychology. Hii ina-apply pia kwa Prof. Ndalichako aliprop chemistry akabaki na mathematics na ku-major education.
Alimejaje education mkuu,mi sidhani kama kuna kumeja nakumaina education,bali najua kuna kumeja nakumaina masomo mtu anayosoma,au mimi sijakuelewa mkuu?
 
Nilipitia juu juu wasifu wa Prof Kitila, alishawahi kuwa Mwenyekiti wa UDASA, Mkuu wa kitivo cha Elimu, mjumbe wa kamati ya chedema, mshauri wa chama cha ACT, nk.

Sijaona tofauti ya majukumu hayo hapo juu na nafasi aliyoteuliwa. Unless kwa mtizamo wenu mnataka/ mnadhani angepelekwa huko Wizara ya Elimu basi ataenda kushika chaki na huku Wizara ya maji na umwagiliaji hawezi kushika spana ya bomba au drill ya kuchimba visima.

Tulitakiwa kujiuliza/ kufahamu ni nini haswa majukumu ya msingi ya Katibu Mkuu wa Wizara.
Katibu mkuu wa wizara anatakiwa awe mtaalamu wa kile anachokisimamia,siyo katibu unakua hujui chochote kuhusu wizara ufikiri kua utafanya kazi kwa ufanisi kama ambavyo baadhi yenu mnafikiria.Kitila anatakiwa awe mtaalamu ambaye kupitia yeye waziri wa maji na umwagiliaje awe anaongozwa nayeye kitaalamu,sasa hapo mi nashindwa kuelewa kama atafanyaje kazi kiufanisi huku yeye ni mtaalamu wa saikolojia.Mimi mwenyewe nimesoma saikolojia chuo,hakuna sehemu wanakofundisha utaalamu wa maji na umwagiliaji.
 
Alimejaje education mkuu,mi sidhani kama kuna kumeja nakumaina education,bali najua kuna kumeja nakumaina masomo mtu anayosoma,au mimi sijakuelewa mkuu?
By that time kulikuwa na waalimu wa aina nne: 1. Secondary teachers (Arts or Science);
2. Teachers' Education;
3. Adult Education na
4. Physical Education
Sasa No.1 tu ndio wenye masomo mawili ya kufundishia yaani kama ulikuwa PCB, PCM, HGE, etc unachagua mawili unakwenda nayo mpaka mwisho sasa hao walikuwa wanaminor education na degree zao zanaitwa either BSc (Education) or BA (Education) na ndo waliokuwa wanapelekwa Secondary kufundisha A-Level

Wale wengine wote wana major Education na wanachagua somo moja tu la kufundishia mengine yanakuwa ya education na degree zao zinaitwa ama BED (Science) au BED(Arts) kulingana na somo lile mojawapo alilobaki nalo kama ni la science au arts. Hawa walikuwa wanapelekwa vyuo vya Ualimu; kwenye Halmashauri kama Maafisa Elimu ma wale wengine Maafisa Michezo na Waalimu wa Michezo
Ni hayo tu mkuu!
 
Miss use huyo jamaa angebakia pale mlimani,si mtaalamu katika wizara hiyo labda personnel officer au afisa tawala.Katibu mkuu wa wizara sio mambo ya hit or miss,kama ni waziri inawezekana lakini PS tegemea wrong debliefing,wrong interpretation,atasumbua sana technocrats.
Lakini labda ameingia kwenye mtego,siku akija mess up ni ONE WAYTICKET KUTUMBULIWA ndo kifo chake kisiasa.
 
By that time kulikuwa na waalimu wa aina nne: 1. Secondary teachers (Arts or Science);
2. Teachers' Education;
3. Adult Education na
4. Physical Education
Sasa No.1 tu ndio wenye masomo mawili ya kufundishia yaani kama ulikuwa PCB, PCM, HGE, etc unachagua mawili unakwenda nayo mpaka mwisho sasa hao walikuwa wanaminor education na degree zao zanaitwa either BSc (Education) or BA (Education) na ndo waliokuwa wanapelekwa Secondary kufundisha A-Level

Wale wengine wote wana major Education na wanachagua somo moja tu la kufundishia mengine yanakuwa ya education na degree zao zinaitwa ama BED (Science) au BED(Arts) kulingana na somo lile mojawapo alilobaki nalo kama ni la science au arts. Hawa walikuwa wanapelekwa vyuo vya Ualimu; kwenye Halmashauri kama Maafisa Elimu ma wale wengine Maafisa Michezo na Waalimu wa Michezo
Ni hayo tu mkuu!
Asante kwa ufafanuzi,mimi ambacho sijaelewa nikwamba UTAMEJAJE/UTAMAINAJE education badala ya somo,mi ninavyojua mtu anaweza akameja linguistics halafu akamaina literature in English huku akiwa katika college ya education au nyingine yoyote inayofanana na education.
 
Okay! Unatakiwa kuelewa kuwa hayo ni mambo ya miaka ya tisini sijui siku hizi maana miaka hiyo Education na Engineering pekee ndo ilikuwa miaka 4 degrees zingine ilikuwa 3yrs
 
Dah, kweli ni Tabutupu , hivi ameteuliwa kuwa Katibu mkuu wa Wizara gani?
Waziri wa Maji anashughulikia maji. Kama no kichagua kilimo au maji ya kufulia nguo au kukosha magari, zote ni kazi yake. Rais aliona anafaa huku na wewe upo la sivyo angekuchagua wewe. Nyamaza!
 
Waziri wa Maji anashughulikia maji. Kama no kichagua kilimo au maji ya kufulia nguo au kukosha magari, zote ni kazi yake. Rais aliona anafaa huku na wewe upo la sivyo angekuchagua wewe. Nyamaza!
mbona hajasema atashughlikia maji ya kuzalisha umeme?
 
Kama lazima angeteuliwa Mkuu wa Parole maana mzee Mrema amezeeka sana, au?
 
Sasa psychology na umuagiliaji wapi na wapi! Mambo ya kitaalamu unampa mwana siasa hatari sana,apo ilibidi akae mtaalamu au engineer kabisa wa mambo ya irrigation nk! Au MTU kilimo kutoka sua basi
Atakaaje hapo wakati sio wa chama....chama cha MAPINDUZI. Nyie mnafiriki Kitila alikuwa upinzani?? Inawezekana mchana alikuwa upinzani, lakini usiku anaenda kimya kimya kwa mkulu kama Nicodemu yule farisao aliyetajwa kwenye Biblia, kuuliza "eti Yampasa afanye nini apate kuokoka?
 
Kama lazima angeteuliwa Mkuu wa Parole maana mzee Mrema amezeeka sana, au?
Nadhani Mrema amezeeka sana, mm nashindwa kuelewa; mbona vijana wapo wangepewa fursa kama hiyo wakaonesha ujuzi na kukumaza CV zao, badala ya kuendelea na wazee kama hao ambao kimsingi they are retired and completely tired!
 
Katika hotuba yake ya kwanza amezungumzia Kilimo cha umwagiliaji kama ndio kipaumbele chake katika kutimiza majukumu yake katika wizara ya maji.

Swali langu, toka lini kipaumbele cha wizara ya maji ni kilimo cha umwagiliaji? Kilimo cha umwagiliaji ni kipaumbele cha wizara ya kilimo kimkakati.

Wizara ya maji tunahitaji utwambie tutapataje maji safi na salama . Kwani hujui ni kiwango gani cha wanchi hawana maji salama?

Hicho sio cheo cha kisiasa.
Dr. Mkumbo inawezekana amechemka kukubali kufanya kazi katika serikali kinyumena maneno yake ya awali.

Lakini Wizara ya Maji kuweka kipaumbele cha kwanza kuwa kilimo cha umwagiliaji katika taifa linalotegemea kilimo si kuchemka.

Wizara za Kilimo na Maji zinatakiwa kushirikiana kuhakikisha wakulima wanapata maji kuendesha kilimo cha umwagiliaji.

Ili kuweza kusambaza maji nchi nzima, serikali inahitaji fedha.

Kilimo ni biashara. Kimsingi, serikali inaweza kutumia kodi inayopata katika kilimo kusaidia kusambaza maji kwa wakulima.

Maji haya yakitumika vizuri na kuzalisha, uchumi utapanda na fedha za kusambaza maji zaidi zitapatikana.

Dr. Mkumbo kuna mengi amekosea na atakosea.Msemeni kwa hayo.

Mkitaka kumsemahata kwa yasiyostahili, hata mtakapomsema kwa yanayostahili mtaonekana ni kawaida yenu kumpinga mtu anayefanya kazi na serikali katika yote.

Zaidi,inabidi watu waelewe kwamba kilimo cha umwagiliaji hakihitaji gharamakubwa ya kusafisha maji (treatment plants). Kimsingi unawezakutafuta mito na kuvuna maji ambayo hayajasafishwa kwa ajili ya kilimo.

Maji safina salama ninavyoelewa mimi -ondoa habari za visima visivyo na uhakika wa usafi wa water table- ni lazima yawe treated, kitu ambacho nchi yetu kufanya priority kwa watu ni habari ya kinyumenyume.
 
Kwa taarifa yako Wizara ya maji ndiyo wamiliki wa maji yote hapa nchini ,wizara ya kilimo haiwezi kuanzisha mradi wa umwagiliaji bila kibali cha wizara ya maji.
Halafu wizara yake inaitwa wizara ya maji na umwagiliaji unafikiri neno umwagiliaji limewekwa hapo kimakosa?
Pamoja na hayo kipaumbele cha umwagiliaji hakina mantiki ikiwa Manzese hakuna maji

Huko vijijini watu wanatembea KM 10 kupata maji. Leo unawaambia kilimo cha umwagiliaji wakati wana hara damu na kipindi pindu kwa kukosa maji. Priority ipo wapi?
 
U
Katika hotuba yake ya kwanza amezungumzia Kilimo cha umwagiliaji kama ndio kipaumbele chake katika kutimiza majukumu yake katika wizara ya maji.

Swali langu, toka lini kipaumbele cha wizara ya maji ni kilimo cha umwagiliaji? Kilimo cha umwagiliaji ni kipaumbele cha wizara ya kilimo kimkakati.

Wizara ya maji tunahitaji utwambie tutapataje maji safi na salama . Kwani hujui ni kiwango gani cha wanchi hawana maji salama?

Hicho sio cheo cha kisiasa.
Una negative attitude tu kwa Prof Kitila nadhani hata hujui anaongoza Wizara gani.

Prof Kitila ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.Sasa yeye kama amesema kipaumbele chake ni Umwagiliaji tatizo liko wapi.

Na hilo ndiyo tatizo letu watanzania,Prof anataka kubadili kabisa kilimo chetu na kuweka miundo mbinu bora ya Umwagiliaji ili kuondoa tatizo kilimo DINI na kukuza pato la Taifa ambalo ndilo litaleta hayo maji na safi na salama kwasababu Chakula itakuwa siyo tatizo tena kwa familia moja moja na Taifa kwa ujumla.

Nakupongeza Prof kwa mtazamo huo tuwekee Misingi mazuri ktk irrigation system maisha ya mtanzania yatabadilika kama ni water bodies zimejaa Tanzania.
 
Kazi au majukumu ya KATIBU Mkuu wa Wizara ni nini? Sifa zipi unatakiwa uwe nazo? Nilizoea kuona DAP Afisa Utumishi Mkuu akipandishwa kuwa KM anapostaafu/kufa. Watumishi wa Umma msahau Succession planning
Siku hizi ni importation Planning. We mtu anatoka kusikojulikana anachukua nafasi ya walizozisotea for 25 years. Huku ni kutiana BP.
 
Lipumba atafutiwe kazi serikalini...ana tia huruma ..le profeseli
 
Back
Top Bottom