Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Unadhani Kitila ndio elimu?

Cha kushangaza ni kwa nini m-bobezi wa taaluma ya elimu asipelekwe wizara ya elimu? Angefaa sana hata km ni kuwa naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
 
Yetu macho tukisubiria mkumbo akatae uteuzi ili kusimamia kauli yake yakupinga wahadhiri kuteuliwa teuliwa hovyo.
 
Mungu ibariki JF
 
Naona alikosa maneno ya akiba!
ngoja tusubiri
 
Nakumbuka alisema hivi:

*"Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo kikuu cha Dar es salaam si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma
"*- Prof. Kitila Mkumbo. ITV 2016/4/17

Lakini Prof Kitila ni mtumishi wa umma,kupandishwa cheo toka Uhadhiri mpaka Ukatibu Mkuu ni "promotion" as far as he is a civil servant.

Zenobius,Mwanafalsafa wa Uyunani aliwahi kusema miaka hiyoo hata kabla ya Afrika kuwa hivi ilivyo.Zenobius alisema "Kila uchwao,kituko kipya huzaliwa Afrika"
 
Acha ubishi wa kijinga unaweza kuwa na madarasa bora kama huna wakufunzi ni bure, lakini ukiwa na wakufunzi bora hata chini ya mwembe elimu inapatikana

Ukibishana na mjinga nawe mjinga. We unadhani Kitila akiondoka chuo ndio wlimu imekufa? Walikuwepo walimu mahiri kina Prof Shivji, nani angedhani law school ingesurvive bila wao?! Acha mawazo ya kijima.
 
Unakumbuka mtu anaitwa Humphrey Polepole? Alikuwa ni mpingaji mzuri wa vyeo vya ukuu wa wilaya na mikoa. Alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya alisahau kila kitu na akakubali hicho cheo alichokuwa anakipinga. Tusubiri Mkumbo atakuja na lipi. Binadamu wanabadilika, tena kwa kasi ya ajabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…