Prof. Kapuya atishia kuishitaki JamiiForums...

Prof. Kapuya atishia kuishitaki JamiiForums...

1422673_711656232179813_390042390_n.jpg
 
duuh hapo KP haponyoki labda sijui iweje maana sheria ndio wamezikamatia wao.
 
Si kweli kuwa eti watanzania ni wavivu na washamba kama alivyosema waziri wa nishati na madini. Je kwa mitazamo yake ni kweli watanzania ni wavivu? Jibu ni sio kweli, kama kweli watanzania wangekuwa wavivu basi hata nchi hii ingekuwa ni sifuri katika sekta ya kilimo. Japokuwa wengi wanatumia zana duni za kilimo lakini bado wanajitahidi katika kilimo.

Na pia watanzania sio washamba kama anavyotaka kuaminisha umma. Ushamba ni kwao viongozi wetu kwa kutetemekea hao wawekezaji feki. Prof Muhongo umewatusi wananchi wa Tanzania hivyo tuombe radhi. Yaonesha sasa prof umeshalewa madaraka.
 
Kapuya acha uhuni,hiyo ni maja ya tabia na biashara yako,nani asiyekujua?hapa umekuja kujikosha kwa watu wenye akili zao,unatakiwa ufungwe maisha na uache kuja humu na mboyoyo zako.Kumbuka babu sea yuko gerezani pasipo na hatia sembuse wewe kila mmoja anakusema.ungekuwa china kaburi lako lingekuwa limeisha ota magugu.jiheshimu baba.
 
Kuna watu wazushi lkn huyu bint kiboko!! Ni huyu aliyesema Kapuya alimbaka na kumuambukiza ukimwi!! Ni muongo kabisa duh!! Ni kweli walikuwa wapenzi lkn maelezo meng aliyotoa ni usanii mtupu! Kumbe aliwahi kumtapel hata mama Salma Kikwete na akatupwa Segerea! Tena aliwahi kumtapel Kimei wa CRDB! Hahaha njaa hzi hatar! Aliwahi kumtapel hata bosi wa Global publisher! Si mwanafunzi ni mdada mwenye miaka 21 na ana mtt!! Ana majina zaid ya matano!! Hii hatar kabisa!! Mechoka mie...

Hahaha hivi unamjua mvushi wewe na muongo?

hivi aliyesema namba ameigawa na bado kwenye waraka wake kaiweka na kwenye kumbukumbu za bunge hipo, huyo una muhitaje?
 
Haisaidii kitu, ukweli uko pale pale.
Kauli ya professor ni propaganda tupu!
 
Kwa hiyo na mie mtoboasiri nitashitakiwa na Kapuya au ni kina Katavi tu? Alipokuwa anakata kiuno na kajukuu alitegemea nini? Mwambieni atushtaki alaah!
 
Nashindwa kuelewa hicho kibinti wakati kinabakwa hakikujua kunasheria mbona kilikuwa kinalamba mkwanja wa ada na kupewa gari hakusema leo kimetokea nn.
 
Ili kukidhi takwa la sheria kosa la jinai linalomkabili mtuhumiwa lingethibitishwa kwanza na baada ya kushindwa kuthibitisha ndio mashauri ya 'malicious prosecution' na 'defamation' yangefuata. Kama mwanasheria makini ni vizuri kufikili vizuri kabla ya kumshauri mteja wako,vinginevyo utakua carried away by the client's emotion na hapo utakua 'the client's short gun' and you will be forced to shoot wherever the client wants, a thing that is against the legal professional....!
 
Kapuya! Kapuya! Kapuya kuwa mkweli kwani Mungu anakuona!
SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa kujikanganya.

Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.

Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.

Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo, Novemba 9, mwaka huu, gazeti hili liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi sita iliyopita.

Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.

Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.

Utetezi wake pia unaongeza utata kwani hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.Katika utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Alilishutumu gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye tasnia ya habari.

Hata hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.

Hata alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.

Lakini muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo iliita bila kupokelewa.

Wakili Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.

"Kwa sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima, mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo atavishitaki mahakamani.

"Kama hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi," alisema.

Aliongeza kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.

Memba aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima haiusiani na chama chake wala serikali.

Kwa siku mbili mfululizo gazeti hili lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Prof. Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.Juzi alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: "Chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu."

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Juzi gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili.


CHANZO: TANZANIA DAIMA




TAMKO LAKE:
 
hii thread naiangalia muda mrefu ila mimi kama mwanaume naanza kuchukia thread zote na watanzania woote wanaoanza kugeuza ukweli kuwa siasa, eti wabaya wangu ndani ya ccm na nje ya ccm...huo ni upumbavu na ufirauni. tusiendekeze upuuzi, na ingekuwa vibaya na aibu ya karne kama mimi ningekuwa kwenye jengo la haki na iyo kesi iletwe kwangu...ungepata hukumu ya haki na iliyojaa hasira. Tufike hatua tuache kuchanganya siasa na mambo ya msingi na haki za wengine. Tufike wakati tutambue kuwa hakuna aliye juu ya sheria, yawezekana leo ukakwepa sheria ulizosaidia kuzitunga ila miaka kumi , ishirini ijayo jinai itakuwa ipo hai na awahusika watakupa haki sawia. Naichukia nchi yangu kwa kugeuza kila kitu kuwa siasa....
 
Back
Top Bottom