Prof. Kabudi ni mtu sahihi, amebobea katika ushauri, majadiliano na utetezi wa rasilimali za Taifa

Kama kweli kwa kuhutubia kule ndio uwe mfano wa kuigwa basi watanzania tuna safari ndefu sana bado. Ehee Mungu tujaalie upeo mpya sie wadanganyika.

 
Makinikia iliishia ju ju tu.kabudi huyuhuyu aliyesomea sheria pekupeku kapotosha umma kwenye issue ya makinikia.Leo hii majadiliano hayo ya kabudi hana maana??
hapa umebugi. jamaa ni pompous hamna maelezo kuhusu academic achievement. so far hajafanya kitu mpaka tuone fruits za majadiliano ya makinikia. subiri hizi sifa umpe noah zikishafika.
 
Ni vyema,katika kumzungumzia mtu,uwe unamfahamu vyema. Wahenga walisema,kuuliza si ujinga. Na pia,usilolijua ni kama usiku wa giza. Jana,nimesoma humu makala ya unaoitwa uchambuzi wa gazeti la Citizen kuhusu majadiliano kati ya Serikali na Barrick.

Mwandishi wa makala hiyo amezungumza mambo kadhaa. Amejitambulisha kama Wakili Msomi Raphael Mgaya. Amezungumzia mambo mengi ya muhimu na ya kupotosha. With due respect,naamini amepotosha kwakuwa hamjui vyema Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi,Mwenyekiti wa timu yetu ya majadiliano

Jambo la mbolea alilolisema Mwandishi wa makala Mgaya ni kuhusu kuwa na mbinu na malengo kama Taifa kwenye majadiliano hayo. Lakini,Wakili Msomi Mgaya amemuelezea Prof. Kabudi katika ufinyu na giza nene. Amemsema kama mwanataaluma tu na asiye na utaalamu wala uzoefu katika majadiliano.

With respect to the author,naomba nieleze kidogo juu ya umahiri,ubobezi na uzoefu wa Prof. Kabudi katika ushauri,majadiliano na utetezi wa rasilimali za taifa kitaifa na kimataifa. Mosi,mwaka 1999-2004, Prof. Kabudi aliazimwa toka UDSM kwenda kuwa Mratibu wa Institutional Framework for Environmental Management Program (IFEMP) Ofisi ya Makamu wa Rais.

IFEMP ilihusisha Benki ya Dunia,DANIDA,USAID na Serikali ya Uholanzi. Mafanikio makubwa ya IFEMP ni kupatikana kwa Sheria mpya ya Mazingira na Kanuni zake. Pili,wakati wa awamu ya nne,Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliteuliwa mmoja wa Wasuluhishi wa mgogoro wa Ivory Coast

Prof. Kabudi alikuwa ni mmoja wa Washauri katika kutatua mgogoro huo. Mikutano yote ya jopo iliyofanyika Nouakchott,Mauritania; Abijan,Ivory Coast na Addis Ababa,Ethiopia ilimjumuisha Prof. Kabudi kama Mshauri muhimu. Tatu,Prof. Kabudi alikuwa kwenye timu ya Tanzania katika majadiliano ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yaliyopelekea kusainiwa Protokali ya Soko la Pamoja (the Common Market Protocol)

Sote tunakumbuka jinsi suala la ardhi lilivyokuwa na mvutano mkubwa. Hatimaye,Prof. Kabudi alikuwa ni mmoja wa watetezi wa maslahi yetu kama watanzania na kutetea ardhi yetu. Nne,hivi karibuni Prof. Kabudi alikuwemo kwenye timu ya majadiliano juu ya mkataba wa TICTS.

Majadiliano hayo yalifanyika kati ya Serikali na Mamlaka ya Bandari kwa upande mmoja na kampuni ya Hutchinson Port ya Hong Kong (mwenyehisa kwa wingi TICTS). Matunda ya majadiliano hayo ni kupatikana kwa mkataba mpya kati ya Mamlaka ya Bandari na TICTS wenye masharti ya manufaa kwa nchi yetu

Pia,Prof. Kabudi amekuwa akikodiwa na Kampuni mbalimbali za Mawakili hapa nchini kuhudhuria na kusimamia usuluhishi na uamuzi wa migogoro ya kimataifa. Kwake,majadiliano ni jambo la kawaida. Hata Mabaraza ya Migogoro ya Kimataifa yanamfahamu.

Tena,majadiliano kati ya Serikali na Barrick yataratibiwa na Sheria mpya za Rasilimali za taifa zilizotungwa mwaka huu. Ni Prof. Kabudi ndiye aliyesimamia mchakato wote wa kutungwa kwa Sheria hizo. Hivyo,atakuwa uwanja wa nyumbani.

Hadi hapo,ni wazi kuwa Prof. Kabudi ana uzoefu na umahiri wa majadiliano na utetezi wa maslahi ya Taifa letu. Yeye,si kwa kusomea,ana umahiri na uzoefu wa mambo ya kibiashara na hata ya kisiasa. Mwandishi Raphael Mgaya namfahamu tangu akiwa anaitwa Bahati Tweve. Najua kuwa alishindwa kuwa Mhandisi na kufanikiwa kuwa Mwanasheria mwaka 2006. Kama Mwanasheria,alipaswa kutafiti kabla ya kuandika. Hakuna mashaka juu ya uwezo wa Prof. Kabudi

Prof. Kabudi si mpenda promo. Anaamini kuwa 'kizuri chajiuza,kibaya chajitembeza'!
Hakika umeumbuka!!
 
Kwa sheria ile mpya ya madini isiyoweza kutekelezeka, isiyoweza kuongeza mapato, isiyoweza kuimarisha uwekezaji katika sekta ya madini, ni uthibitisho tosha kuwa Prof. Kabudi ni mwanataaluma asiye na uzoefu wa masuala ya kibiashara na uwekezaji. Anachoelewa ni kuwa unapokuwa na kodi kubwa basi mapato yatakuwa makubwa. Hizo ni fikra za mtu mwenye uelewa mdogo kuhusu biashara.

Sasa hivi ilitakiwa tuwe na kanuni ya sheria mpya lakini wataalam wamekwama kwa sababu sheria iliyopitishwa haitekelezeki, na hakuna muda wa mpito uliowekwa na sheria mpya. Mpaka sasa sekta ipo ICU, hakuna kinachoendelea, na wataalam wote wa ofisi zote za madini hawaelewi wafanye nini, na wala hawakushirikishwa katika uandaaji wa mswada kama ilivyostahili.

Kwa upande wa wawekezaji, sheria ile imekuwa ya kuwafukuza kwa sababu cimmulative revenue of the government for an average profit making mine will be 60-65%, leaving 30-35% to the investor. Mgawanyo huu hautavutia uwekezaji kutoka kwa wawekezaji makini, labda kwa wale wababaishaji ambao wanajua watacheza namna gani ili kuubadili huo mgawanyo.

Sheria mpya ya madini imeandaliwa na Kabudi na wanasheria wenzake bila kuwahusisha wataalam wa sekta ya madini ambalo ni kosa kubwa. Kutokana na kutoelewa, wameishia kuweka taratibu ngumu sana za ufanyaji utafiti kwa kudhani kuwa tunaibiwa madini kwa kupitia sampuli.

Kabudi na wenzake, hawajui kuwa kufanya utafiti kuna uhakika wa zaidi ya 95% wa kupoteza fedha. Unapoweka utaratibu mgumu kwenye shughuli ambayo haina uhakika wa kupata faida, maana yake unawafukuza wote. Na ukweli hautabadilika, 'Hakuna mgodi wowote bila utafiti'. Professor na wenzake hawajui kuwa zaidi ya kampuni 400 zilizokuja kufanya utafiti Tanzania, ni 3 tu zina migodi ya dhahabu, na mbili zipo katika harakati za kujenga migodi. Kampuni nyingine zote zimepoteza fedha zao ingawa serikali imepata kilicho chake kwa kupitia ada na kodi mbalimbali.

Dunia nzima inaondokana na urasimu, Kabudi na wenzake, karne hii wanaweka sheria yenye urasimu mkubwa usio na manufaa na unaoua uwekezaji kwa sababu unaongeza gharama za uwekezaji bila kuwa na faida yoyote kwa yeyote.

Kwa sheria ile ni aheri tungewatumia wanasheria wenye certificate na diploma lakini wenye mtazamo wa kibiashara na wanaoweza kuwashirikisha wadau, nina hakika tungekuwa na sheria nzuri zaidi. Shida ya wanaojiita wasome (hasa maDr. na maProf.) wa Tanzania, ni kutopenda kuwashirikisha watu wanaojua kuliko wao wakiamini kuwa neno Dr au Prof linamfanya ajue kila kitu.
Uliyoyasema kuhusu Kabudi yametimia!!
 
Hakika wewe ni wakili msomi, kulikuwa na miruzi mingi twezo kibao, ili utengue kauli yako na ukasimama kwa kile ulicho kiamini Leo yametimia.
 
Back
Top Bottom