Prof. Kabudi ni mtu sahihi, amebobea katika ushauri, majadiliano na utetezi wa rasilimali za Taifa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Ni vyema,katika kumzungumzia mtu,uwe unamfahamu vyema. Wahenga walisema,kuuliza si ujinga. Na pia,usilolijua ni kama usiku wa giza. Jana,nimesoma humu makala ya unaoitwa uchambuzi wa gazeti la Citizen kuhusu majadiliano kati ya Serikali na Barrick.

Mwandishi wa makala hiyo amezungumza mambo kadhaa. Amejitambulisha kama Wakili Msomi Raphael Mgaya. Amezungumzia mambo mengi ya muhimu na ya kupotosha. With due respect,naamini amepotosha kwakuwa hamjui vyema Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi,Mwenyekiti wa timu yetu ya majadiliano

Jambo la mbolea alilolisema Mwandishi wa makala Mgaya ni kuhusu kuwa na mbinu na malengo kama Taifa kwenye majadiliano hayo. Lakini,Wakili Msomi Mgaya amemuelezea Prof. Kabudi katika ufinyu na giza nene. Amemsema kama mwanataaluma tu na asiye na utaalamu wala uzoefu katika majadiliano.

With respect to the author,naomba nieleze kidogo juu ya umahiri,ubobezi na uzoefu wa Prof. Kabudi katika ushauri,majadiliano na utetezi wa rasilimali za taifa kitaifa na kimataifa. Mosi,mwaka 1999-2004, Prof. Kabudi aliazimwa toka UDSM kwenda kuwa Mratibu wa Institutional Framework for Environmental Management Program (IFEMP) Ofisi ya Makamu wa Rais.

IFEMP ilihusisha Benki ya Dunia,DANIDA,USAID na Serikali ya Uholanzi. Mafanikio makubwa ya IFEMP ni kupatikana kwa Sheria mpya ya Mazingira na Kanuni zake. Pili,wakati wa awamu ya nne,Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliteuliwa mmoja wa Wasuluhishi wa mgogoro wa Ivory Coast

Prof. Kabudi alikuwa ni mmoja wa Washauri katika kutatua mgogoro huo. Mikutano yote ya jopo iliyofanyika Nouakchott,Mauritania; Abijan,Ivory Coast na Addis Ababa,Ethiopia ilimjumuisha Prof. Kabudi kama Mshauri muhimu. Tatu,Prof. Kabudi alikuwa kwenye timu ya Tanzania katika majadiliano ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yaliyopelekea kusainiwa Protokali ya Soko la Pamoja (the Common Market Protocol)

Sote tunakumbuka jinsi suala la ardhi lilivyokuwa na mvutano mkubwa. Hatimaye,Prof. Kabudi alikuwa ni mmoja wa watetezi wa maslahi yetu kama watanzania na kutetea ardhi yetu. Nne,hivi karibuni Prof. Kabudi alikuwemo kwenye timu ya majadiliano juu ya mkataba wa TICTS.

Majadiliano hayo yalifanyika kati ya Serikali na Mamlaka ya Bandari kwa upande mmoja na kampuni ya Hutchinson Port ya Hong Kong (mwenyehisa kwa wingi TICTS). Matunda ya majadiliano hayo ni kupatikana kwa mkataba mpya kati ya Mamlaka ya Bandari na TICTS wenye masharti ya manufaa kwa nchi yetu

Pia,Prof. Kabudi amekuwa akikodiwa na Kampuni mbalimbali za Mawakili hapa nchini kuhudhuria na kusimamia usuluhishi na uamuzi wa migogoro ya kimataifa. Kwake,majadiliano ni jambo la kawaida. Hata Mabaraza ya Migogoro ya Kimataifa yanamfahamu.

Tena,majadiliano kati ya Serikali na Barrick yataratibiwa na Sheria mpya za Rasilimali za taifa zilizotungwa mwaka huu. Ni Prof. Kabudi ndiye aliyesimamia mchakato wote wa kutungwa kwa Sheria hizo. Hivyo,atakuwa uwanja wa nyumbani.

Hadi hapo,ni wazi kuwa Prof. Kabudi ana uzoefu na umahiri wa majadiliano na utetezi wa maslahi ya Taifa letu. Yeye,si kwa kusomea,ana umahiri na uzoefu wa mambo ya kibiashara na hata ya kisiasa. Mwandishi Raphael Mgaya namfahamu tangu akiwa anaitwa Bahati Tweve. Najua kuwa alishindwa kuwa Mhandisi na kufanikiwa kuwa Mwanasheria mwaka 2006. Kama Mwanasheria,alipaswa kutafiti kabla ya kuandika. Hakuna mashaka juu ya uwezo wa Prof. Kabudi

Prof. Kabudi si mpenda promo. Anaamini kuwa 'kizuri chajiuza,kibaya chajitembeza'!
 
.

Tena,majadiliano kati ya Serikali na Barrick yataratibiwa na Sheria mpya za Rasilimali za taifa zilizotungwa mwaka huu. Ni Prof. Kabudi ndiye aliyesimamia mchakato wote wa kutungwa kwa Sheria hizo. Hivyo,atakuwa uwanja wa nyumbani.'!
.
.
.
Kwan haya mazungumzo yanahusisha kuvunja mkataba uliopo na kuingia mkataba mwingne mpyaa!?? Maana nnavyofahamu mm kama bush lawyer ni kwamba sheria mpya hazitahusu mikataba inayoexist ila tu ile itakayoingiwa baada ya sheria hizo kuwepo...
.
Kama ndivyo sheria mpya zitawezaje kuratibu mikataba ya zaman iliyoingiwa na kina mangungo chin ya sheria za zaman!???
.
Naomba kutolewa tongotongo hapa
 
bwana Petrol E
nakuona unajitahidi sana kumutetea Prof kabudi. nakumbuka nilipoleta uzi wangu unaosema prof kabudi hafai kuwa mwenyekiti wa kamati ya makinikia ulizuiliwa kwa muda baadae nikaona uzi wako wa kumutetea kisha na uzi wangu ndiyo ukaluhusiwa. sijui kwa nini unamtetea sana but naomba nikupe hoja chache hapa
1. kuna commercial production industry na polcy industry. kabudi hajawai kuendesha any commercial productional industry kama unabisha lete ushahidi huo
2. mifano yote unayoeleza inahitaji busara zaidi na siyo elimu ya uzoefu hakuna hata swala moja alilotatua ambalo linahitaji maauzi ya hasara na faida hata moja. migogoro ya kisiasa na utungaji wa sera za mazingilia aziwezi kumuweka mtu imala kusimamia mabishano ya masilahi ya fedha
3. sheria unayoisifia kaitunga inamatatizo mengi ya kufukuza wawekezaji. tena siyo wakuja tu hata wandani(wazawa). inasumbua sheria hii. wewe unamsifia eti yupo uwanja wa nyumbani?. kile alichokiweka kwenye sheria yenyewe hata hakijui maana yake. hii ni kwa sababu siyo practically trained huyo prof wako katika sekta ya madini.
4. prof kabudi is only academician expert kwingine hakuna kitu.
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom