baba-mwajuma
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 6,049
- 12,773
Hata hio ya kuchanganya Matunda Mzungu kadanganya, kuna Matunda Ukichanganya yana Madhara,Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.
Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhira ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.
Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili, ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).
Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".
"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
View attachment 3310073
Japan University of osaka, moja Ya vyuo Bora zaidi Duniani (Kipo Top 100) na Queens land Australia (Nacho kipo top 100).Amesoma wapi
Mshangazi wewe ni dactar pia bila shaka...Maongezi ya Prof. hayalengi watu kama wewe ambao mnafanya kazi za kutumia nguvu mashambani (au wale ambao wanashughulisha mwili mara kwa mara). Wewe hata ukila mapapai matatu kwa siku, yanabadilika tu kuwa energy na unayatumia kwenye kazi unazofanya.
Prof. ni mtaalamu wa moyo uko sahihi, na hakuna afya ya mwili bila afya ya moyo.
Sukari za aina zote kama hazitatumika kama energy zikishachakatwa kwenye umengenywaji, end product yake ni fat, ambayo itaenda kutunzwa kwenye mwili, utanenepeana, utapata fatty liver, utakuwa na high cholestrol, utajaa mafuta kwenye mishipa ya damu na matatizo mengineyo mengi.
Umesema vizuri kwenye kula kwa kiasi. Kuchanganya matunda hakuna madhara ya moja kwa moja, ila ukishachanganya most likely utakula mengi kuliko ukila moja na utakula yenye viwango tofauti tofauti vya sukari. Fructose, sukari inayotokana na matunda inachakatwa na ini, small amounts kutoka kwenye matunda hazina shida kabisa ila ukiwa na tabia ya kuzidisha bila kujua, tegemea matatizo.
Shida ya magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na ulaji wa hovyo ni slow progression conditions, inaweza kuchukua miaka 10-20 tokea umeanza kutengeneza tatizo mpaka utakapoona symptoms. Kuna sababu kwanini watu wengi Tanzania wanakufa in their 60's. Mara nyingi shida ya afya utakayoipata ukiwa na miaka 50 au 60, imetokana na ulivyoishi ukiwa na miaka 20, 30, na 40. The body keeps a count, Again, za kuambiwa changanya na zako!
Cc:
Hassanjk
Poor Brain
Prof.Janabi akiambiwa uongo wake na Mkali wa Bio-Chemistry View attachment 3309840hivi kumbe na ngozi nyeupi Wanaujinga, yaani mtu anapinga Hoja kwamba ni uongo halafu anakubali ni ukweli ๐๐๐๐
Mkuu ukila kipande kidogo Cha embe ukala kipande kidogo Cha papai au ndizi na mwingine Akala embe Zima au ndizi nzima je nani atakuwa amezidisha hicho kiwango unachosema?Au tunashadadia kwa vile amesema mzungu? Ina maana Tanzania hatuna wasomi waliokuwa wanafahamu hizo hoja anazokuja nazo mzungu? Ni vipi kama Janabi alikuwa anazungumzia hakuna ulazima wa kuchanganya matunda kama kote unaweza kupata fructose, maltose na sucrose? Hatuoni kama ukiyachanganya unaweza kuzidisha kiwango kinachojitajika na mwili? Wacha nisubiri wanafunzi wa Prof. Janabi wanavyoweza kumnasua mwalimu wao katika hili!
Huna akili. Poor brain as you call yourselfSio anachanganya ila ni vile anarahisisha communication...
Hv unajua kumuelekeza mtu ambaye ajasoma hayo mambo deep zaidi ni kupoteza muda ndio maana kuna mda anaongelea juu juu tu...
Kuna vitu ana skip ili kutokupoteza mda..
Mtu na uprofessa wake kusema ashindwe kujua ishu ya sugar seriously
Janabi is a fraud. Alifeli biochemistry somo ambalo ni basic science katika medicine. Janabi sio nutritionist anaingilia sehemu asioyoijua. Kimsingi Janabi hajanyooka kishuleshule. Ni vile mfumo unambeba alafu watu wanahofia kumcrash waziwazi lakini katika medicine ni takataka.Au tunashadadia kwa vile amesema mzungu? Ina maana Tanzania hatuna wasomi waliokuwa wanafahamu hizo hoja anazokuja nazo mzungu? Ni vipi kama Janabi alikuwa anazungumzia hakuna ulazima wa kuchanganya matunda kama kote unaweza kupata fructose, maltose na sucrose? Hatuoni kama ukiyachanganya unaweza kuzidisha kiwango kinachojitajika na mwili? Wacha nisubiri wanafunzi wa Prof. Janabi wanavyoweza kumnasua mwalimu wao katika hili!
Ongea fact acha kukalili vya vijiweni...Huna akili. Poor brain as you call yourself
"Kukalili" au Kukariri? Kama kuandika tu ni mtihani siwezi kukuelewesha. I rest my case. StupidOngea fact acha kukalili vya vijiweni...
Sawa ngoja waje wa paqwa ji"Kukalili" au Kukariri? Kama kuandika tu ni mtihani siwezi kukuelewesha. I rest my case. Stupid
Tunarudisha "shukrani" kwa Dokta.Ningetamani sana kama Janabi angejibu uongo wake kwa maelezo kama hayo ya huyo jamaa.
Mi najiuliza kwanini wana mnadi Afrika nzima? Akishinda tunapata faida gani, kuna upigaji au kujipendelea ?
Na gharama za kumzungusha Afrika nzima zinatoka mfuko gani nchi hii? ni zake binafsi au za umaa?
CAG atueleze mwakani tulitumia Bilioni ngapi kumnadi Janabi Afrika na tumepata faida gani au hasara kiasi gani.
Hajui bio chemistry yule mzee, anawambia watu wanywe kijiko kimoja cha ujii๐, wakati mtu mume, anatakiwa ale calories si chini ya 2700 Sasa pigia kijiko kimoja ninkama mls 20 ivi, si ni bangi hiyo
Jamaa alipita na chuma chetu, baada ya KAZI akagenda Macca hija kujitakasa! Shame!Mwamba Traore nae akae makini Janabi sio mtu poa
Janabi kichwani mweupe ndio maana sasa kwasababu tunaumwa ndio tutume ujinga kutatua shida zetu?Dr Janab ni Binadamu na muda mwingine anafanya makosa, Yes
ila inatakiwa apewe sapoti na wapatikane wakina Janab wengi
Mchango wake katika mambo ya lishe na kupunguza magonjwa yasiyoambukiza ni mkubwa
Kwa mtu ambaye ameshadeal na changamoto hizi atakubali kisukari, presha, kansa, magonjwa ya moyo, figo, stroke nk yapo juu sana
Kwa Bahati mbaya haya magonjwa kwa asilimia kubwa yanasababishwa na ulaji ovyo na sisi tumezoea kula ovyo
Shida ya wabongo hatuappreciate juhudi zake ila tunasubiri sehemu ya kukosoa tu
HAKUNA NJIA YA KUPUNGUZA/KUEPUKA MAGONJWA YA MOYO/YASIYOAMBUKIZA ISIPOKUWA LAZIMA TUANZE NA LISHE/ULAJI
Shida mnajifanya ujuaji huku sio wafuatiliaji wa mamboJanabi kichwani mweupe ndio maana sasa kwasababu tunaumwa ndio tutume ujinga kutatua shida zetu?
Hako kajamaa kama kakolowizadi vile.Watakunja ngumi mpaka wachoke tu. Janabi mwenyewe inasemekana wala siyo daktari bingwa wa moyo kaunga unga tu kozi wala hazieleweki. Sasa amekomaa na mambo ya lishe wakati wala siyo uwanja wake wa kitaaluma. Ndo maana anaishia kushushuliwa kwa kutulisha matango pori ๐๐๐
View attachment 3309869
Usibishane na vilaza...waache na tope zao kichwani.....Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.
Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhira ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.
Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili, ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).
Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".
"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
View attachment 3310073