Prof. Ibrahim Lipumba yuko wapi jamani?

Mkuu Tanzaniaist,
Nime-edit title, badala ya kuandikwa "amekitekeleza" nimebadili na kuwa "amekitelekeza!" Nafikiri ndio Kiswahili sanifu!
 
..Prof.Lipumba huwa anakumbuka siasa wakati wa uchaguzi mkuu tu.
 
Ipo siku na wengine nao watakimbia tu..... njaa kitu kingine bana! jamaa ana kibarua kinachomlipa vizuri akae CUF pana nini?
 
Hata angekuepo mambo yangekuwa hayahaya.naskia anaongoza chama kupitia Facebook
 
Hata mimi nahisi ataibukia wakati wa uchaguzi, nasikia kaenda kukusanya nondo za ushindi. This time hashindwi mtu!
 
ushauri wako ulichelewa,huwezi kuzungumzia kufunga zizi wakati ng;ombe washatoka
 
Bwana Yesu asifiwe..
Kama kiongozi wao haonekaniki,members wake hawawezi kujiendesha na chama hakina muda mrefu kitakufa
 
Safari hii anataka kufata nyayo za mrema ktk ubunge,anataka kwenda kugombea ubunge kawe
 
Lipumba ni international figure, as much as anahitajika CUF anahitajika pia kwa faida ya Ulimwengu mzima..

Yuko anasaidia binadamu wengine duniani, CUF ni taasisi inajiendesha vema
 
Chama chenyewe kishaozeshwa kwa ccm so haina shida kiviile
 
Mwenyekiti wa chama cha CUF aka CCM B profesa Lipumba hivi yuko wapi? maana chama chake kinazidi kuelekea shimoni,ndoa waliyofunga na CCM inazidi kuwaumiza na wamekataa kutoa talaka wakisema kuwa nyie CUF ndo mlilazimisha kuolewa.Rudi mwenyekiti uone jinsi Ismail Jussa alivyojigeuza katibu mkuu wa CCM B.
 
Hajaondoka na ofisi yupo Makamu mwenyekiti sijui anaitwa Alhaji nani vile....?
 
Wacha wafu wazike wafu wao.

Katibu yupo ikulu nanakula bata mwacheni lipumba ale vitu vilivyopimwa.
Kama ni lichama alishahangaika nalo vya kutosha kwa kufikiri ni chama cha siasa kama kilivyoanzishwa na mapalala kumbe kilishatekwa na maalim ili kimrudishe serikalini na lengo limeshatimia.

Lipumba mtaalamu wa uchumi amewaachia kina nape na uchumi wao unaopaa kwenye makaratasi acha ale bata na wenye akili wenzake kina obama.
 
Prf.Lipumba yuko nchini Marekani. Alishinda na kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wachumi wanaoshughulikia uchumi wa dunia na shirika la NED la Marekani. Hawa ni baadhi tu ya lulu tulizotunukiwa nchini Tanzania na tukashindwa kuzitumia,tunakalia siasa za majitaka zinazotuongezea umaskini kila kukicha.

Profesa Lipumba anajulikana kimataifa kwa mchango na uwezo wake kama mchumi aliyebobea kuliko anvyojulikana hapa Tanzania. Shame on this country and its people!

Imagine mtu kama huyu angekuwa Rais wa nchi yetu,tungepiga hatua kubwa kiasi gani kiuchumi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…